Katika tembea tembea yangu
huku uswahilini kwetu MWANANYAMALA B KWA
MAMA ZAKARIA , KATA YA
MAKUMBUSHO , jijini DAR ES SALAAM , TANZANIA niliwaona
WANAUME kadhaa wakifanya
KAZI katika kitu
kilichoonekana kuwa ni
Msingi wa nyumba
kubwa ambapo WANAUME
hawa walikuwa wakifanya
kazi ya KUPANGA
MATOFALI .
Nilijaribu kumwuliza mmoja wa WANAUME hao : “
UNAFANYA NINI ?” Alijibu :
“ KWANI HUONI ?
NAPANGA MATOFALI . Niliuliza
swali hilo hilo
kwa MWANAUME mwingine
:
“ MIMI ? AHAA , NAFANYA KAZI
HAPA KUJITAFUTIA RIZIKI.”
Mtu wa
tatu naye alinijibu :
“ KWA NINI , BWANA ,
NASAIDIA KUJENGA OFISI
NZURI KATIKA JIJI
LETU.” Yupi kati
ya wanume hawa
unadhani anaelekea kuwa
na maisha ya
hali ya juu ?
Kabla hujayafanya
maisha yako kuwa
ya MALENGO na
FURAHA , lazima ujue JAMBO
fulani kuhusu wewe
mwenyewe , kwamba KWA NINI
UWE NA UFANYE
KAMA UNAVYOFANYA. Ni
kitu gani hasa
kinachokufanya uwe tofauti na
wakati mwingine MCHOYO , pengine kuwa
mtu mzuri na
anayekubalika ? ILI MRADI
TU , KWA NINI
UWE ULIVYO ?
MWANASAIKOLOJIA mmoja maarufu
amekadiria kwamba ni
asilimia ndogo sana
ya watu ulimwenguni
wana MALENGO yao , Waliosalia WANABURUZWA TU ! kama
ALICE akiwa nchi
ya ajabu .
“ NIFUATE
BARABARA IPI ? “
ALICE alimwuliza PAKA
CHESHIRE.
“ INATEGEMEANA NA
UNAKOKWENDA , PAKA alijibu.
“ LAKINI , “ALICE ALISEMA , “ SIJUI NINAKOTAKA
KWENDA.”
Ndipo PAKA akasema:
“ HAKUNA TATIZO
KWA NJIA YOYOTE
UTAKAYOFUATA.”
ANGALIZO:
Ni jambo muhimu sana
kuwa kila mmoja
asitofautiane na njia
ya MAISHA anayofuata. Kusita kutoa
uamuzi , kukosa FURAHA
na KUTORIDHIKA ulimwenguni , kwa kiasi
kikubwa husababishwa na
kukosa MALENGO.
Unataka MAFANIKIO , kila mmoja
anataka MAFANIKIO. Kila mtu
huelewa MAFANIKIO kama
kitu ambacho ni
tofauti kwa wengine
ina maana KUPATA
FEDHA NYINGI SANA. KWA
MIMI ina maana
MJI wenye MKE
aliyeridhika na MTOTO
mwenye FURAHA , pamoja
na FEDHA ZA
KUTOSHA zinazoweza KUNIPATIA
MAHITAJI MUHIMU.
Umekwishapiga PICHA
kichwani mwako kuhusu
maana ya MAFANIKIO
kwako. MAFANIKIO katika
MAISHA hutokea tu
baada ya kuweka
MALENGO katika
MAISHA ambayo unayajenga. Wakati umejiwekea
MWELEKEO wako , MAISHA
YANA MAANA. HUCHUKUA UMUHIMU
MPYA. Hujisikii tu kuwa
MAISHA ni majaribio
yasiyo na maana
na vikwazo vyenye
kiasi kidogo cha
FURAHA kilichotupwa kwako
kukuzuia KUJINYONGA.
WANASAYANSI
wametangaza kuwa mwili
wa binadamu una
mabilioni ya chembecheme
ambazo zinaishi katika
mambo matatu:--
(a).
Kemikali iliyo katika
Chakula unachokula.
(b).Homoni zilizopo
katika mfereji wa
damu.
{c). Ujumbe
wa fahamu unaotuma
wewe mwenyewe.
SIRI YA
MAFANIKIO IPO HAPA NDUGUN YANGU : Unapotuma ujumbe
wako kupitia kituo
cha kurushia MATANGAZO---UBONGO -- ndipo
unapohuishwa , unatiwa NGUVU. Kama wewe
ni mtu unayependa
kusema : “ SIWEZI , SIWEZI , “ ndipo
WAZO hilo linasafirishwa kwenye
chembechembe katika mwili
wako na zinaambizana kuwa :
“
HATUWEZI , BOSI AMESEMA HATUWEZI , HIVYO HATUWEZI . TUPO CHINI
YA MAMLAKA YAKE .”
Kama una
mtazamo mbaya kuhusu
MAISHA , chembechembe zako
nazo huwa na
mwelekeo huo. Mara unapofikiria
vinginevyo , unashangaa kwa nini
NGUVU zako zimeongezeka
ghafla.
WANASAYANSI wamefanya
UTAFITI wa kutosha
kuhusu jinsi mwanadamu
alivyo na jinsi
alivyoumbwa . Matokeo ya
ucunguzi wao kuhusu
sababu za TABIA
YA MWANADAMU yanafurahisha sana.
UGUNDUZI wao
ni kuwa NGUVU
ambayo huzunguka katika
mawimbi yaendayo kasi ,
hutokea mwilini. MAISHA yote
ni NGUVU na
unaweza kuilekeza NGUVU
kwenye mwili wako
kama unavyopenda. Ni
juu yako kuyafanya
MAISHA yawe kama
unvyopenda kwa sababu
WEWE NDIYE MWAMUZI
WA MWISHO NA
DEREVA WA ROHO
YAKO.
Makala hii
imeandikwa na MWL.
JAPHET MASATU, anapatikana
kwa Call /WhatsApp + 255 716
924136 / + 255 755 400 128,
EMAIL: japhetmasatu@yahoo.co.m. Ni
mwanafunzi wa CHUO
KIKUU HURIA , TANZANIA, KINONDONI
, DAR ES
SALAAM ,2015.
No comments:
Post a Comment