MWANADAMU mara nyingi
amekuwa akifanya makosa
kwa kudhani FURAHA
ndiyo hitaji muhimu
sana katika MAISHA , badala ya
KUFAHAMU jinsi ya
KUTAWALA MAISHA.
Ni vigumu
kueleza maana ya FURAHA kwani
ni zawadi muhimu
kwa kila mtu. Huepuka uchambuzi
wa mwanasayansi , sawa na
inavyoepuka maelezo ya
MWANAFALSAFA.
Kila siku
FURAHA huwa ni
jambo la ziada
ambalo huongezwa kwenye
MAISHA , ni kama sukari
inavyoongezwa kwenye maisha
mazuri , ni tuzo inayotolewa
kutokana na juhudi
kubwa.
Si maumbile. Mtu mwenye
afya nzuri ambaye
pia ana maumbile
mazuri , anaweza asiwe
ameridhika na kasha
kukosa FURAHA ambako
kunaweza kutokana na
mashambulizi ya matatizo.
Kuwa na
afya nzuri haimaanishi
uhakika wa kuwa
na FURAHA. Kinyume na
hivyo , hata wakati mtu
ni mgonjwa au
wakati mazingira kwa
nguvu zote hujikusanya
na kumwangamiza mtu , bado
anaweza akaifahamu FURAHA.
FURAHA si
kumiliki , tunaweza kumiliki ulimwengu
wote , lakini tukakosa FURAHA
kabisa. Haipatikani katika MAFANIKIO , kwani unaweza
kufikia MALENGO yako
yote , lakini ukakosa FURAHA. Unaweza kupata
UMAARUFU , BAHATI , na MAFANIKIO
, bado unaweza ukapungukiwa
zawadi ya FURAHA.
Si matatizo
yanayowafanya watu wasiwe
na FURAHA , mtu anaweza
kuangalia jinsi matumaini
na matakwa yake
yalivyokosa MAFANIKIO ,
bado moyoni akawa
na FURAHA.
FURAHA
NI NINI ? FURAHA ni
hali ya mtu.Si
jambo ambalo linatokea , ila
ni majibu ya
kile kinachotokea yanayoonesha
kiasi cha FURAHA au
HUZUNI. MAZINGIRA hayana uwezo
wa kuharibu utulivu
wa mawazo yetu , ila
kama tunayaruhusu.
MATUKIO ni
mambo ya nje. FURAHA ni
jambo la kiundani.Si
kitu kinachotokea pekee ,
bali ni majibu
ya tukio fulani
la kiundani.
FURAHA ni
likizo ya mawazo ,
burudiko la moyo
au roho.Ni UHURU
WA MAISHA usio
na bei. Haina kitu
kinachoweza kufidiwa badala
yake. Malipo yote ambayo
mwanadamu huyatafuta ni
njia tu ya
mwisho huo.
Makala hii imeandikwa
na MWL JAPHET
MASATU , anapatikana kwa
EMAIL , japhetmasatu@yahoo.com.
Mobile : + 255 716 92 4136
WhatsApp + 255 755 400 128.
No comments:
Post a Comment