Bila
shaka umekuwa ukijiuliza
kwanini watu wengine
wana bahati ? Ni matajiri wanafanikiwa
kimapato wana pesa? wana
mahusiano mazuri na
watu ? Wana kazi
nzuri ? Yaani
ni kama miguuni
mwao wanatembea na
bahati ! Kwanini isiwe mimi pamoja
na juhudi na uwezo
nilionao ? Nini tatizo
kwangu mimi ninayesoma
makala hii ? Je, ni
mipango ya mungu
au …… ? SOMA SIRI
YA MAFANIKIO HAPA
CHINI !
KWANINI WAO
WANA BAHATI ? NA
SI MIMI ?
Katika utafiti unaonyesha ya
kwamba , MTU ANAJITENGENEZEA BAHATI
MWENYEWE KULINGANA NA
JINSI ANAVYOFIKIRI , NA
JINSI ANAVYOTAZAMA MAMBO , NA
JINSI ANAVYOTENDA.
Pindi
utakapoanza kubadili jinsi
unavyofikiri na
jinsi unavyotazama mambo utaanza
kutengeneza bahati yako.
Ukitazama kukosa , mikosi , balaa , shida ndivyo
hivyo itakavyokuwa.Ukitazama kinyume
chake yaani kupata
au kufanikiwa, bahati nzuri , maisha mazuri , kupata pesa ni hivyo
hivyo itakavyokuwa.
Watu
wanaodai kuwa hawana
bahati ya kufanikiwa , hujikosesha wenyewe
bahati. Hukutana na fursa au nafasi
adimu na kuzipitiliza bila
kutambua. Watu wenye bahati
husimama mara moja
pindi wanapokutana na
kitu kipya mbele
yao.
Kwa
mfano , siku moja
unakutana na watu
usiowajua kabisa.Watu hao
wanazungumzia biashara fulani
yenye kuzalisha faida
kubwa. USIWAPUUZE ! Kaa kitako
karibu nao. Wasikilize kwa
makini .Wadadisi mengi kadiri
uwezavyo.Hivi ndivyo bahati
huanza. Hii ndiyo
fursa au
nafasi usiichezee kabisa
ndugu yangu.
Watafiti waligundua
kwamba watu wanaopata
bahati ni kwa
sababu HAWACHEZEI NAFASI
AU FURSA pindi
inpojitokeza hata kama ni
ndogo mithili ya
punje ya haradali. Na
siku zote hutarajia
kufanikiwa. Husema ………….ipo siku. Huamini
kuwa hawajaumbwa ili
wakose. Kwao kukosa ni chanzo cha
kupata.
Watu
wenye bahati ,yaani wale
wanaowaza kufanikiwa , maisha mazuri ,kupata pesa
badala ya kulaumu kwa
mambo yanayotokea katika
maisha ni wenye
kushukuru kwa yale
yanayotokea au kile
kilichotokea .Kwao glasi tupu
ni kama glasi
iliyojaa.
Jinsi
unavyofikiri na jinsi
unavyotazama mambo ndivyo
unavyotengeneza bahati. KILA SIKU
FUKIRIA KWAMBA UNA
BAHATI, UTAONA MAMBO YATAKAVYOBADILIKA ! UTAONA JINSI
UTAKAVYOVUTA MATUKIO YA
YENYE BAHATI .ITAZAME GLASI
TUPU KAMA ILIYOJAA.
Kumbuka wengi
wetu tunaamini bahati
hutengenezwa na waganga
wa kienyeji au
jadi. Mtazamo huo si
sahihi. Bahati haipatikani
kwa uchawi , wala mwujiza. Bahati ni
wewe ni jinsi
UNAVYOFIKIRI, UNAVYOTAZAMA
MAMBO NA JINSI
UNVYOTENDA.
Tambua unapokuwa
na AFYA una
neema , hivyo una bahati. Unapokuwa na
AKILI timamu una
neema, hivyo una fursa
pana sana ya
kupata bahati.UHAI ni
neema, unapokuwa unapumua pumzi, una
bahati , una bahati kubwa sana.
Unaitazama neema kinyume.Unaitazama miguu
kama si bahati, unaitazama mikono
kama si bahati , unayatazama macho
kama si bahati. Unazitazama neema
zote zilizo katika
mwili wako kama
si bahati.Badala yake ,
unatazama mtu mwenye
pesa nyingi kuwa
ana bahati. PESA
bila AKILI , bila AFYA
zitakuja ? Na hiki
ndicho kinachofanya baadhi
ya watu wanaiba , wanaua ili
wapate PESA.Hii ni
kwa sababu wanatazama
mambo kinyume.
Kitendo cha
kutambua kuwa , AKILI na
AFYA ni fursa
za bahati , jione ni
mwenye bahati kubwa.Na
ukisikia mtu yeyote
anakwambia ana mkosi , basi tambua
ana ukosefu wa
kutambua elimu hii , maana mkosi
ni ukosefu.
Bahati ina nafasi
katika mafanikio yetu,
lakini kwa wale
wapaniaji , wachapa kazi
na wenye
malengo. Binadamu
hupanga na kuamua
mwenyewe , awe mtu
wa namna gani.Huwa
tunageuka vipofu kabisa
tunapoingia kwenye kudhani
mganga fulani anaweza
kuongeza bahati zetu, kutufanya kupendwa
na wateja hata
kama tunawatukana wateja
hao au kutuwezesha
kupata dhahabu kwenye
shimo la udongo
wa kufinyangia vyungu.
Imani
kwamba kuna nguvu
ya nje ambayo
inaweza kumsaidia mtu
kupata bahati au
kufikia mafanikio bila
malengo na juhudi
yake ni yenye kupotosha
sana. Imani kwamba , kuna wenye
nota zenye kung”ara
kuliko wengine , hivyo hao
wanaweza kupata bahati
au mafanikio kirahisi
haina ukweli.
Tulilishwa imani
gani kuhusu sisi, kufikiri kwetu
kukawa kwa namna
gani na tukaweza kuwa
na malengo au
hapana maishani , huchangia sana kutufanya tuwe
na mafanikio au
tusiwe nayo. Lakini kuchagua
maisha tunayotaka kuishi , ndiyo muhimu zaidi.Tukijiuliza na
kutafuta maarifa , tataujua ukweli
na hata kama
tuliathiriwa na malezi ,
tutatoka tu kwenye
kiza.
Asante sana
mdau wangu kwa kusoma
makala hii muhimu
sana ili kubadili maisha
yako .Binadamu ni jinsi anavyofikiri . Imeandaliwa
na MWL JAPHET
MASATU , anapatikana kwa namba
0716 924136 / 0755 400128.
Kama una swali au
maswali kuhusu
mada hii uliza .
No comments:
Post a Comment