MAFANIKIO KATIKA
BIASHARA
Wafanyabiahara walioanza biashara
ndogo na kupata
mafanikio makubwa wamekuwa
watu wasiokatishwa tamaa wala
kurudishwa nyuma na
vikwazo. Badala yake wamekuwa
wakitumia MBINU zifuatazo
kupambana navyo :
KIKWAZO I :
MITAJI YA KUFANYIA
BIASHARA.
MBINU
ZITUMIWAZO NA WALE
WALIOPATA MAFANIKIO
{1}.
Kuanza biashara ambazo
hazihitaji mitaji mikubwa.
{2}.
Kutegemea mali kauli
na kujenga uaminifu
wa hali ya
juu katika kuilipia.
{3}.Kukopa kutoka
taasisi zinazotoa mikopo
midogomidogo { MFIs }
{4}.Kukopa na
kurudisha fedha haraka
ili kuweza kupata
mikopo mikubwa zaidi
mapema
{5}.
Kukopa kwa jamaa , marafiki ambao
wanawaamini
{6}.
Kuwa na
mahusiano ya karibu
na benki kila wakati
na kuhakikisha wanafahamu
maendeleo ya biashara
zao ili wakienda
kukopa wasiwe wageni.
{7}.
Kukopa benki wakati
ambao hali ya
fedha ni nzuri na
kurejesha mara kadhaa
ii kujijengea rekodi
nzuri.
KIKWAZO II:
KUPATA MASOKO
MBINU
ZITUMIWAZO NA WALE WALIOPATA
MAFANIKIO
{8}.Kuhakikisha kuwa
wanaridhisha wateja kwa
gharama yoyote , mfano
mnunuzi asiporidhika na
nguo aliyoshonewa
anashonewa nyingine.
{9}.Kuajiri wafanyakazi hodari sana
katika utoaji huduma
na kuwapa mishahara na
mazingira mazuri ya
kazi
{10}.
Kutangaza biashara kwa
njia ambazo hazigharimu sana , mfano
kutuma salamu kutoka kwenye
biashara kwa njia
ya redio / postcard.
KIKWAZO III :
KUPATA USHIRIKANO WA
MUME / MKE
MBINU
ZITUMIWAZO NA WALE
WALIOPATA MAFANIKIO
{11}.Kuwa muwazi
na mkweli, na kuhakikisha
kuwa mume / mke anafahamu
kila anachofanya.
{12}.Kukwepa kuonyesha
dalili zozote za
dharau kwa mume / mke.
{13}.Wengine wameamua
makusudi kabisa wenzi
wao wa ndoa
wasijihusishe katika biashara
zao , kwa
kuwa dira na
tabia zao katika
uendeshaji biashara ni
tofauti mno.
KIKWAZO IV :
KUCHANGANYA MAJUKUMU YA
ULEZI NA BIASHARA
MBINU
ZITUMIWAZO NA WALE
WALIOPATA MAFANIKIO
{14}.Kuwaonyesha watoto
kazi wanazofanya , ili
awapo kazini wawe
wanaelewa kinachoendelea
{15}.
Kucgagua shughuli moja
au chache ili
kuweza kumudu na
majukumu ya nyumbani.
KIKWAZO V :
RUSHWA NA USUMBUFU
WA MAOFISA WA
SERIKALI
MBINU
ZITUMIWAZO NA WALE
WALIOPATA MAFANIKIO
[16}.Kutokubali kuwa
legelege wanapoona wanaonewa.
{17}.Kuweka kumbukumbu
vizuri , na kuzitumia
kubishana na maofisa
wa kodi.
{18}.Kutumia wataalam
kuandaa mahesabu ya
biashara , na kuyatumia
kuonyesha kodi wanayopaswa kulipa.
Makala hii imeandikwa na MWL JAPHET MASATU + 255 716 924136 / + 255 755 400 128