BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Ili kufanikiwa huhitaji kufanya kila kitu au kujua kila kitu. Badala
yake chagua eneo lako ambalo unaweza kufanya vizuri, kisha kazana
kufanya vizuri, kuwa bora kuliko wengine wote na utaweza kufanikiwa
zaidi. Kadiri unavyochagua vizuri eneo lako na kuweka juhudi kubwa,
ndivyo unavyotumia nguvu zako na umakini wako vizuri.
Jifunze kutofautisha kati ya mawazo na mawazo mazuri, bidhaa na bidhaa
bora, uwekezaji na uwekezaji mzuri. Asilimia 90 ya vitu vyote
unavyokutana navyo, siyo muhimu, yaani ukiachana navyo hutakosa
chochote. Ni asilimia 10 tu ndiyo muhimu, jua hiyo asilimia kumi na
ukazane nayo huku ukipuuza mengine yote.
Kuwa na kiasi, haijalishi umefanikiwa kiasi gani, miaka 200 ijayo,
huenda hakuna atakayejua hata kama uliishi hapa duniani. Kila unapoanza
kujiona wewe ni muhimu kuliko wengine, kumbuka kitakachotokea miaka 200
ijayo, dunia itakuwa imekusahau kabisa. Ishi maisha yenye maana kwako na
siyo maisha ya kujionesha na kutaka wengine waone wewe ni muhimu kuliko
wao.
Kuna orodha nyingi za watu waliofanikiwa, kuanzia ndani ya nchi mpaka
dunia nzima. Lakini jinsi mafanikio hayo yanavyopimwa inaweza isiwe
sahihi kwako. Mafanikio ya kweli kwako ni mafanikio ya ndani yako,
ambayo siyo rahisi kupimwa kwa nje. Mafanikio ya ndani utayapata kwa
kuweka juhudi kwenye yale maeneo uliyochagua, kuweka umakini wako kwenye
mambo yaliyo ndani ya uwezo wako na kuachana na mengine yote. fedha,
madaraka na umaarufu ni vitu vya nje, ambavyo huwezi kuvidhibiti,
unachoweza kudhibiti ni hatua unazochukua. Kazana kuwa bora kila siku na
weka juhudi zaidi kwenye kile ulichochagua kufanya.
Mzazi ana nafasi kubwa sana katika kuendeleza kipaji cha mtoto
Kipaji ni uwezo wa
kuzaliwa nao wa kufanya jambo fulani kwa ngazi ya juu bila kufundishwa
au baada ya kufundishwa kidogo tu. Kipaji kinaweza kuwa cha kimwili au
cha kiakili lakini pia kinaweza kuendelezwa au kudumazwa.
Mzazi ni
mtu wa kwanza anayeweza kutambua uwezo ama kipaji cha mtoto wake. Hata
hivyo ana fursa ya kuendeleza au kutokukiendeleza kipaji cha mtoto.
Baadhi
ya wazazi hutambua vipaji vya watoto mapema na kuanza kuviendeleza kwa
kuwapatia nyenzo mbali mbali ambazo huwasaidia katika kuboresha uwezo
walio nao.
Lakini pia wapo wazazi ambao wanamalengo yao juu ya ni
kitu gani wanapenda watoto wao wafanye. Ama yamkini hawana ufahamu wa
nini cha kufanya ili kumwendeleza mtoto mwenye kipaji .Hata hivyo vipo
baadhi ya vipaji ambavyo wazazi huona ni upotevu tu wa maadili mfano
kuimba na kucheza mziki.
BBC imezungumza na mama Ritha, mama mwenye watoto wanne. Anasema
kwa kiasi kikubwa baadhi ya wazazi na hata yeye mwenyewe kipindi cha
nyuma walikwamisha sana watoto sababu walikuwa hawatambui kama kipaji
pia ni njia salama ya kumwezesha mtoto kimaisha. "Wazazi wengi
huwa hawajuagi tena zamani tulikuwa tunaona watoto wanapotea kabisa. Mi
binti yangu wa kike alikua anapenda kuandika nyimbo za wasanii wa
marekani na hata za kwake mwenyewe kwenye daftari lake afu kukiwa na
sherehe yeye ndo mwimbaji. Nikaona anapotea nlikua na mchapa na
nlimwambia akifika chuo kikuu ndo afanye uo mziki lakini si nyumbani
kwangu maana hata baba yake alikuwa hapendi kabisa," Mama Ritha
anaiambia BBC Hata hivyo ameongeza kuwa wazazi pia huwanyima fursa
za kujifunza watoto kwani kila akishika kitu mzazi hupiga kelele mtoto
aache kwa madai kwamba ataumia. Hata hivyo wapo baadhi ya watoto ambao wamepewa msaada mkubwa na wazazi wao katika kuboresha na kuendeleza vipaji vyao.
BBC imezungumza na mwanadada mpambaji Plaxeder Jumanne au baby
precious kama anavyojulikana katika kazi zake za upambaji, anasema mama
yake ndio mtu wa kwanza kumshauri ageuze kipaji chake kuwa biashara huku
akimnunulia vifaa orijino vya urembo.
"Mie nlikuwa nawachukua
watoto wenzangu nawapamba nlikua napenda sana urembo kama mama yangu.
Hata nilipo kuwa nikaanza kuwapamba watu. Nilikuwa natumia vifaa feki
hivi vya bei rahisi lakini mama yangu alianza kwa kuninunulia vifaa
orijino kabisa. Na huwezi amini nilikua nampamba yeye na kumfuta kabla
sijapata wateja tena nimejifunza kufunga maremba ya kinaijeria kichwani
kwa mama na alikuwa ananisaidia sana, sasa hivi nasafiri hadi mikoani na
kupamba watu mbali mbali hadi watu maarufu na nimepata pesa nikanunua
vifaa vingi sana Orijino," Plaxeda anaiambia BBC.
Hata hivyo
manadada huyo anasema kwa sasa mama yake ametangulia mbele za haki tangu
mwaka jana ila bado anamshukuru kwa sababu hivi sasa kazi ya upambaji
inampa pesa kuliko ajira yake na imemwezesha kufungua biashara zingine.
"Mimi
sijajitangaza sana ila kupitia vifaa alivyonianzishia navyo mama yangu
nikawa napamba hadi maharusi na wasimamizi wao. Na kipaji hiki kimenipa
pesa ninafanya biashara ya kutengeneza nywele hasa mawigi na pia
kufungua biashara ya nguo. Mama yangu angekuwepo angefurahi sana ila
naamini anaona. Nimewaremba baadhi ya wasanii wa Tanzania. Safari ndo
inaanza," Plaxeder anaiambia BBC.
Mwanaharakati wa masuala mbali mbali ya kibinadamu Shahista Alidina
maarufu kama Shaykaa, anasema baadhi ya wazazi hupenda kutimiza ndoto
zao kupitia watoto na mwishowe huwakwamisha.
"Unakuta mzazi kama
alishindwa kuwa mwanasheria au daktari kama alivyotaka huko nyuma
atataka mtoto wake afuate ndoto hiyo. Hawataki kuwapa uhuru watoto
wafuate wanavyopenda. Unakuta kipaji cha mtoto kinaweza mletea kipato
cha kutosha tu ila mzazi anampa mtoto shinikizo la kufaulu tu shule awe
namba moja, mbili au tatu na ndiomaana unaona watoto wengine hadi
wanajiua. Wanawanyima fursa watoto kufanya vitu wanavyovipenda," Shaykaa
anaiambia BBC.
Hata hivyo anaongeza kuwa kunachangamoto nyingine
kwa wazazi kupangia kazi watoto kuwa hii ni ya wanawake au hii ni ya
wanaumena kujenga uoga kwa watoto na kuwanyima fursa ya kujituma zaidi.
"Kusoma
kwa mtoto ni muhimu ila kuna muda wa ziada na kuna maisha nje ya
darasa. Unakuta mtoto wa kike anapenda kucheza mpira, lakini mzazi
atapinga kuwa huu ni mchezo wa wanaume mwanamke hatakiwi, sasa hapo moja
kwa moja mzazi atakuwa ameua kabisa kipaji cha mtoto kama mtoto atakosa
fursa ya kujiendeleza huko mbele," anasema Shaykaa Mwanaharakati huyo pia amewaasa wazazi kuhakikisha wanawasaidia watoto kujiendeleza kijamii.
"Mtoto
ni muhimu awe na maisha yake pia, na tutambue kuwa na wao ni binadamu
wala si wafungwa. Ni muhimu ndio kufuata dini na misingi bora ya maisha
pamoja na mila na desturi lakini tusisahau kuwa mtoto anapofikia umri wa
kujielewa anahaki ya kufanya maamuzi kuwa anapenda nini ilimradi ni
jambo jema kisheria, kidini, kiafya na kijamii. Tuwe marafiki kwao
lakini tusiwapotoshe watoto wetu, Shaykaa anaiambia BBC.
Simu yaweza kumsaidia mtoto kujifunza lakini bado nimuhimu kwa mzazi kuwa makini
Hivi karibuni
imekuwa kawaida sana kumkuta mtoto anatumia simu ya mkononi ya mzazi
wake na mara nyingine wanatumia bila hata kupata ridhaa ya mzazi
mwenyewe.
Baadhi ya watoto huonyesha utaalamu wa hali ya juu katika kufungua kurasa mbalimbali za simu hizo.
Na inadaiwa kuwa kuna watoto ambao huwa wanajifunza mambo mengi kupitia simu za mkononi. Hata
hivyo si wazazi wote ambao hukubali simu zao zitumiwe na watoto, baadhi
huwa wakali na kuweka kila aina ya nywila ingawa wengine huwa hawaoni
shida kuwapatia watoto wao simu punde tu wanaporejea kutoka kwenye
majukumu yao ya kila siku.
Baadhi ya wazazi huwa wanaona kuwa simu ndio njia pekee inayoweza
kuwafanya watoto wao watulie na wao wapate muda wa kupumzika ama hata
kufanya shughuli zao za nyumbani.
Je,kuna faida yeyote endapo mtoto atatumia simu? BBC
imezungumza na baadhi ya wazazi ili kufahamu ni kwa kiasi gani watoto
wao hutumia simu zao na wanawadhibiti vipi vitu anavyoangalia mtoto?
"Kwa
kweli simu yangu hata sina uhuru nayo huwa nikifika tu nyumbani wanangu
huwa wananipokea kwa mbwembwe zote na cha kwanza kubeba ni simu na
nikihitaji lazima niwaombe wao. Simu ikiita utakuta wao ndio
wanapokea,mara nyingi wanaangalia video za kartoon au za watoto wenzao
zilizopo you tube," Mama Brian anaeleza
Baadhi ya watoto hutambua hadi nywila za simu za wazazi wao
Alex Kayetta ambaye ni baba wa mtoto mmoja, anasema simu yake huwa haimiliki punde tu anapofika nyumbani , "Mwanangu
akishashika simu yangu yani kuipata lazima nimbembeleze, na akichukua
mara nyingine huwa lazima nimtafute alipo ,kuna siku nilimkuta amejificha
ndani ya beseni akicheza michezo ya kwenye simu'game' nikampiga
picha".
Freddie Kyara ni mwanasaikolojia kutoka nchini Tanzania
ambaye anaeleza kuwa hali hii huwa inafanana na jinsi mzazi anapokua
kwenye simu muda mrefu na hupoteza fursa ya kuwa karibu jamii na ndivyo
hivyo inavyotokea kwa mtoto.
Na kwa upande wa mtoto kutumia simu huwa kuna madhara pia "Kukua kwa
mtoto kunahitaji awe na mbinu za kijamii, kama vile kucheza na watoto
wenzake na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wenzake, lakini siku
hizi unaweza kukuta mtoto anashindwa kucheza na watoto wengine kwa
sababu amezoea yeye rafiki yake ni simu tu.
Ubunifu wa mtoto
unaweza kupungua. Sisi wakati tunakuwa hatukuwa tunajua habari za simu,
ilikuwa ni kucheza mpira na kujishughulisha na shughuli mbalimbali za
nyumbani na hali hiyo ilitufanya tuweze kujenga urafiki na watu na kujua
tabia za watu tofautitofauti.
Mtoto anaweza kujifunza pia kwenye
simu lakini lazima uthibiti uwepo kwa sababu sio kila kilichopo kwenye
simu kina maudhui mazuri kwa watoto na wanapaswa kutengewa muda" Kyara
,mtaalamu wa saikolojia alieleza.
Hata hivyo jumbe mbalimbali zimekuwa zikisambaa kuonya madhara ya
mionzi ya simu kwa watoto wadogo na kudai kuwa umri sahihi wa kupewa
simu ni kuanzia miaka kumi na sita. Jambo ambalo Daktari Fredrick
Mashili anasema madhara ya namna hiyo huwa inategemeana zaidi na umri wa
mtoto japo kwa upande mwingine macho yanaweza kupata shida ingawa
hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha madhara hayo ya mionzi.
"Kuna
wasiwasi kwamba mtu akianza kutumia simu mapema anaongeza muda wa
kuyashughulisha macho yake katika mionzi kwa muda mrefu zaidi kitu
ambacho si kizuri kwa afya ya macho," Dkt.Mashili alieleza.
Linapokuja swala la fedha, kila mtu ana namba na viwango vyake. Kwa
sababu tunatofautiana ndoto, kazi/biashara, kipato, mitindo ya maisha na
hata mazingira, matokeo yetu ya kifedha hayawezi kulingana.
Hivyo kujipima hatua ulizopiga kifedha kwa kuwatumia wengine ni
kujiumiza na hata kujirudisha nyuma, kwa sababu kuna namba nyingi ambazo
utakuwa huzijui kuhusu wengine. Kwa mfano unaweza kumwona mtu kwa nje
anaonekana kuwa na vitu vinavyoashiria ana fedha nyingi, lakini kumbe
vitu vyote hivyo amepata kwa mkopo ambao ataulipa maisha yake yote. Pia unaweza kumwona mtu ukafikiri hayupo vizuri kifedha kwa mwonekano
wake wa nje, kumbe anafanya uwekezaji ambao baadaye utamwezesha kufikia
uhuru wa kifedha.
Kwa kuwa ni vigumu kupima hatua ulizopiga kifedha kwa kuwatumia watu wengine, unahitaji kujitumia wewe mwenyewe.