TUFANYE KAZI KWA BIDII ! HAPA KAZI TU !
TUMEPATA kusikia
mengi katika siku
zilizopita , na bado siku
hizi tunasikia
taarifa
za KUTOWAJIBIKA , ukosefu wa
KUJITUMA tabia ya
kupenda kitu fulani
bila kuwepo umuhimu
kwa upande wa
watu binafsi na
makundi. Hili linaweza kuwa
tatizo kubwa sana ,
kwani linaashiria tabia
inayoweza kuharibu sifa
nzuri ya maisha
yetu.
Kuongezeka kwa
matukio ya tabia
hiyo ni dalili
kwamba kuna UOZO
katika jamii ambao
inabidi tujaribu kuchukua
kila hatua na
kuutokomeza kabla haujaathiri MATUMAINI
yetu .
Tabia mbaya
hujitokeza kwa namna
nyingi. Kuna tabia ya
kutojali mambo ambayo
ni muhimu katika jamii. RUSHWA ni tatizo kubwa
katika sekta nyingi
za umma. Hali hiyo
haipo kwa watu
wa aina au
umri fulani tu katika jamii.
UKOMBOZI wetu ,
kitaifa, unategemea
uzalishaji mkubwa na KUFANYA KAZI KWA BIDII.
Kama ilivyo
kauli mbiu ya
Chama cha Mapinduzi (CCM ) katika uchaguzi
wa Raisi , wabunge na
madiwani mwaka 2015 inayosema ,
“ HAPA KAZI TU !
Ni kweli kabisa
“FANYA KAZI KWA
BIDII PAMOJA NA
UBUNIFU “ MABADILIKO NI
LAZIMA ! Na si
kinyume na hapo ! Hakuna
Mabadiliko kama
KAZI HAIFANYIKI KWA
UFANISI . Akili kichwani mwako ndugu
yangu. TAFAKARI ! Kinachoanza
ni KAZI alafu
MABADILIKO yanafuata. Kwa
mtazamo wa kisayansi ,lazima TUFANYE KAZI
KWA UFANISI. Simaanishi lazima
iwe kufanya kazi
saa nyingi au
kama mtumwa. Naamini kwa
kutumia njia na
mbinu nzuri , kuwa na MIPANGO mizuri, pamoja na
kuwa na ufanisi katika UBUNIFU
na uendeshaji wa
SHUGHULI ZA WANADAMU.
Utaratibu mzuri
ni kuwa kila
mtu lazima AFANYE KAZI
NZURI na kwa
matokeo makubwa. Hii haimaanishi
ni kwa wafanyakazi pekee , lakini na
UONGOZI pia uwe
wa KUJITUMA. Ni kwa
kuchukua hatua hizo
tu ndipo tutakapoona kuwa
MAISHA yetu yanakuwa
bora.
Vinginevyo , kama nchi
nzima haitajitoa kipekee
na kudhamiria KUFANYA
KAZI KWA BIDII , ndoto yetu
ya kuwa na
maisha mazuri itabakia
kuwa NDOTO.
Yote haya
yanatambulika kwa kufuata
kanuni. Hata hivyo , kipi ambacho
bado tunakitafuta ? Ni shauku
ya kupata MAFANIKIO
MAKUBWA , bila kuwa wazalishaji
wakubwa ? MOYO wa kutaka
KUPATA KILA KITU
BILA KUTOA KITU
NI TABIA YA
KUIKWEPA NA KUITOKOMEZA.
Nataka nieleweke
kwamba siwalaumu wazalishaji
wote wa nchi
hii. Ni mbali kabisa
na hilo.Wala sipendi
kuzungumzia yale yaliyokwisha dhihirika
ambayo sasa tunatakiwa
kuyatokomeza au kuangalia
madhara yake.
Kwanini hali
hii imeshamiri sana ? Kuna
majibu mengi , lakini nitayataja
mawili tu.
(a).Huenda vita
vya kiuchumi vya
karne mbili na
nusu za mwanzo
vimeyumbisha akili za
wanaume na wanawake
na kuharibu malengo
ya taifa.
(b).Kumekuwepo MITUME na
MANABII nchini ambao
walikuwa na mawazo
potofu kwamba KAZI
haikuwa muhimu na
juhudi hazikuhitajika dunia
mpya ambayo ingepatikana kwa
kulalama tu.
Yote haya ,
huenda yamechangia kuharibu
uwezo wa watu
wengi na kudhoofisha maamuzi
yao kwa kudidimiza
imani zao kwa
FALSAFA YA KUJITEGEMEA.
----Ni
SAIKOLOJIA ya mtu
binafsi pekee ambayo
inaweza kufufua moyo
wa mapambano , ubunifu wa
vitega uchumi na
kujishughulisha , hivyo
kuweza kufufua tena
uchumi na hali
nzuri ya maisha
kwa jamii.
----MOYO wa
kupenda kazi si
jambo la kulazimishwa.Ni muhimu
kwa mazuri ya
mwanadamu.Husababisha
burudani yake iwe
ya furaha na
hutafuta malengo katika
maisha yake.
----Inasikitisha kuona
kwamba watu WALEGEVU na
wenye tabia ya
kulaumu tu hawajabadilishwa kuwa
na FALSAFA YA
KUFANYA KAZI.
----- Kama nguvu na
msukumo mpya vingetumika kuwafanya
watu wafanye KAZI , UOZO ambao
upo katika jamii
ungetokomezwa ,ndipo watu wangekuwa
wepesi kutoa maamuzi.
----Ingawa mabadiliko
hayo hayawezi kufanywa
kama AJALI , yanaweza kukamilishwa
kwa kubadili MTAZAMO. LAKINI MAGEUZI
DAIMA HUANZIA KWA
MTU BINAFSI. Raisi
hawezi kutumia uchawi
na kusema “ haya
yatokee !” kama wananchi hawapendi
KUFANYA KAZI KWA
BIDII NA UFANISI.
Kama Taifa ,
lazima tupumue hewa ya
KUJIAMINI, kujenga moyo mpya
wa KUFANYA KAZI
ambao utajengeka kwa
watu wote , ndipo zama
mpya yenye MATUMAINI
itafunguliwa kwa wote .
HONGERA
RAISI WETU WA AWAMU
YA TANO , DR.
JOHN POMBE MAGUFULI
KWA KUWA NA KAULI
MBIU ‘ HAPA KAZI
TU “ TUNAFAHAMU UTENDAJI WAKO ! MUNGU AKUBARIKI SANA ! TUPO PAMOJA . WATANZANIA TUFANYE
KAZI KWA BIDII
NA UFANISI , TUMEKUWA
WAVIVU SANA NA WATU WA KULALAMIKA SANA.
MUNGU AWABARIKI WATANZANIA TUJITAMBUE NA TUFANYE KAZI KWA BIDII.
Makala hii imeandikwa na MWL JAPHET MASATU , anapatikana kwa E—MAIL , Japhetmasatu@yahoo.com. Mobile no: + 255 716 92 4136 WhatsApp + 255 755 400 128.