Njia Rahisi Itakayokusaidia Kukabiliana Na Rafiki Hasi Kwenye Maisha Yako.
Kulingana na takwimu inaonyesha,
Wastani wa watu wanne (4) unaojihusisha nao kwa siku wana mitazamo hasi.
Unaye rafiki yeyote ambaye ni hasi?
Je, unaye rafiki ambaye ukikaa naye unaishia kujisikia vibaya?
Je, unaye rafiki ambaye anapenda kulalamika?
Je, unaye rafiki ambaye ukikaa naye unahisi kukata tamaa?
Je, unaye rafiki anayeamini kutowezekana kuliko kuwezekana?
Kama umejibu ndio ,
Kabla ya kujifunza njia rahisi itakayokusaidia kukabiliana na rafiki hasi.
Tuangalie kwanza utofauti uliopo kati ya matajiri na masikini wanavyojihusisha na rafiki hasi.
Matajiri huwa wanajenga mahusiano na watu wenye mitazamo chanya na waliofanikiwa.
Watu wanaoamini kwenye uwezekano na wanaohamasisha na kutoa matumaini.
Masikini huwa wanajenga mahusiano na watu wenye mitazamo hasi na walioshindwa.
Watu waliokata tamaa na wanaoamini haiwezekani na wanaondoa matumaini.
Watu wanaokuzunguka wanayaathiri sana maisha yako.
Pale ulipo kimaisha sasa ni wastani wa walipo wale unaotumia nao muda wako mwingi.
Matajiri wanajua ili wawe matajiri na wabaki kwenye utajiri, wanapaswa kujihusisha na watu matajiri.
Hivyo marafiki zao huwa ni matajiri wenzao, tena wale waliowazidi utajiri.
Masikini hubaki wakiwa wamezungukwa na masikini na hilo kuwafanya wabaki kwenye umasikini wao.
Ili ufikie utajiri, chagua kujenga mahusiano na watu matajiri au wanaoelekea kwenye utajiri.
Pia lazima uwapunguze watu hasi kwenye maisha yako,
Wale ambao ukikaa nao unaishia kujisikia vibaya na kukata tamaa.
Zungukwa na watu chanya,
Ambao ukikaa nao unajisikia vizuri na kupata hamasa na matumaini ya kupata utajiri zaidi.