BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Thursday, July 9, 2020
JINSI YA KUENDANA NA MABADILIKO YA KIDUNIA YANAYOTOKEA KILA SIKU.
Wakati mwingine unapaswa kuelewa kwamba kile ambacho unakijua leo baada ya miaka mitano ijayo kinaweza kisiwe na faida tena au kinaweza kisilete matokeo yale ambayo mwenyewe unayapata kwa sasa. Nimesema hayo kwa sababu kwa hivi sasa mambo yanabadilika sana.
Ile dunia ya jana si dunia ya leo. Mambo kila kukiacha yanabadilika sana, watalamu nao hawalali kutwa wanaumizwa vichwa vyao kuweza kugundua mbinu mpya ambazo ni rahisi kwa mwanadamu kuweza kumrahisishia kazi mbalimbali.
Kama nilivyosema hapo awali kwamba dunia inakwenda kasi hivyo ili kuendana sawa na mabadiliko hayo ni kwamba hata wewe unapaswa kubadilika pia. Na njia pekee ambayo itakayokusaidia kwa namna moja ama nyingine kuwa bora zaidi kwenye kila eneo unalofanyia kazi ni kwamba unatakiwa kujiimarisha wewe mwenyewe kila siku.
Na njia pekee itakayokusaidia kuweza kujiimarisha ni kwamba unatakiwa kuhakikisha kwamba unaenda na mabadiliko yanayotokea kila siku, ni kujifunza mambo mapya kila wakati kwa sababu usipojifunza mambo mapya ni kwamba utapitwa na vingi.
Ni muhimu kuelewa kwamba kwenye kila sekta unayoifanyika kazi unapaswa kujifunza namna ambavyo utakuwa bora kila wakati. Kumbuka kujifunza hakuna mipaka hivyo ni muhimu sana kwako kuweza kujifunza mambo mbalimbali yatakayokusaidia kwa namna moja ama nyingine kuwa bora zaidi kwenye kile unachokifanya kila wakati kwani pindi utakaposhindwa kufanya hivyo ni kwamba hata wewe utapitwa na utashindwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia yanayotokea.
Kwa muktadha huo, unapaswa kila wakati uwekeze muda mwingi kwenye kujifunza vitu vipya kila siku. Kama wewe ni mkulima basi ni jifunze mbinu mpya kila siku zitakazokuwezesha kufanikiwa zaidi katika kilimo hicho, kama wewe ni mtalamu wa jambo fulani basi yakupasa kuweza kujipambanua zaidi kwa kujiwekeza kwenye kupata maarifa sahihi juu ya jambo hilo.
Ni muhimu kupata maarifa fulani kila wakati kwa sababu kwa sasa dunia inakwenda kasi sana hivyo bila kuwa na maarifa mapya ni kwamba utazidi kuwa mtu wazamani kila siku , kwani kila kitu ambacho kitakuwa kinafanywa na watu wengine kwako kitakuwa kigeni.
Mwisho naomba nitamatishe kwa kusema ya kwamba kila wakati ongeza ubobezi kwenye kila eneo unalofanyia kazi kwa sababu ubobezi humsaidia mtu kuweza kufanya jambo lililo bora zaidi, pia kila wakati unapaswa kuelewa kwamba ubobezi hupatikana kwa kuweza katika kujifunza vitu vipya kila siku ili uweze kuendana na mabadiliko ya kidunia.
JE , WAHITAJI KUFIKIA NDOTO ZAKO ? FANYIA KAZI MAMBO HAYA :--
Kila mtu anatamani kuzifikia ndoto za maisha yake ya mafanikio. Kwa sababu hiyo kila mtu huchukua hatua anazoziona yeye zinamfaa ili kutimiza malengo hayo. Je, ni wangapi wanajua kuwa huwa wanachukua hatua sahihi au la.?
Katika makala haya, ni lengo langu ni kukumbusha wewe, mambo ya msingi na kama utayazingatia mambo haya yatakusaidia wewe kuweza kukufikisjha kwenye ndoto zako za mafanikio. Je mambo hayo ni yapi?
1. Andika malengo yako.
Najua malengo yako unayajua vizuri tu, lakini kuna sababu muhimu sana kwa wewe kuyaandika malengo yako tena. Chukua kalamu na karatasi, na andika vitu vyote unavyotaka kuvifikia kwenye maisha yako.
Fikiria juu ya kitu ambacho unataka kufanya au unahitaji kukifanya. Inaweza kuwa kitu chochote kama malengo ya afya au malengo ya biashara yako. Orodhesha vitu vingi iwezekanavyo, lakini viwe vile unavyotaka kuvifanikisha.
2. Weka vipaumbele vya malengo yako.
Ndio, najua umeandika malengo mengi, lakini ukweli ni kwamba huwezi kuyatimiza yote. Ili uweze kuyafikia malengo hayo, yagawawe kwa kuzingatia vipaumbele. Unapaswa kujua, malengo yapi uanze nayo na yapi uyaache.
Kwa kuweka vipaumbele itakupa nguvu wewe, ya kuweza kuyafikia malengo yako kwa urahisi. Na ukishaweka vipaumbele, usibabaishwe na malengo mengine yatakayotokea hapa katikati, vipaumbele vyako vinatosha, vitekeleze kwanza.
3. Vunja vunja malengo yako.
Vunja kila lengo kuwa dogo ambapo unajua unaweza kutimiza kwa urahisi. Hakikisha pia unajipa muda wa wewe kutekeleza malengo yako kulingana na wakati uliokadiriwa wa mradi huo uliojiwekea.
Kwa mfano, ikiwa lengo lako ni kusoma kitabu. Usijilazimishe kusoma kurasa mia moja, kwa mara moja, soma kurasa chache na zielewe. Fikiri kama unataka kujifunza kuogelea, je! Ungeingia ndani ya bahari au ungeanza kwanza kujifunza katika dimbwi?
4. Amua kuwajibika.
Lengo kuu ni kuishi maisha bora ya kufikia malengo yetu na kufanya hivyo lazima tuchukue hatua moja kwa wakati mmoja na kwa hiyo tunahitaji msimamo thabiti. Je! Unahakikisha vipi malengo yako yanatimia?
Hapa hakuna ujanja, unatakiwa kuwajibika. Fanya kila linalowezekana kwa wewe kuamua kuwajibika ili kuhakikisha malengo yako yanatimia. Ukikubali kuwajibika nakupa uhakika unaweza kufanikiwa na kufika mbali kimafanikio.
Fanyia kazi mambo hayo na hakikisha unachukua hatua kuona ndoto zako zinatimia.
JE , UNATAKA KUACHA KAZI YA AJIRA ? KABLA YA KUFANYA HIVYO ZINGATIA HAYA KWANZA.
Jambo #1. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa ujue, jinsi ya kubadilisha bahati mbaya na kuwa bahati nzuri.
Kama hujui jinsi ya kubadilisha bahati mbaya, na kuwa bahati nzuri, usijaribu kuacha kazi utajiumiza sana. Ujasiriamali una mambo mengi sana ya changamoto.Hivyo kwa kadri unavyokutana na changamoto ngumu kabisa, unatakiwa ujue jinsi ya kuzibadilisha changamoto hizo na kuwa bahati nzuri. Kama ukishindwa, basi tulia na ajira.
Jambo # 2. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa kujua, ni shughuli zipi zinatengeneza biashara ya mafanikio.
Biashara haihusishi mauzo tu peke yake. Kama ndio umetoka kwenye ajira na una akili ya kuwaza mauzo peke yake, utakwama. Unatakiwa ujue biashara inahusisha mambo mengi.Zipo shughuli nyingi zinazotengeneza mafanikio ya biashara kama huduma kwa wateja, usafi, au mawasiliano mazuri na wateja. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa kuzingatia haya kwanza.
Jambo # 3. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa ujue, umuhimu wa kujiendeleza binafsi.
Kama utaingia kwenye ujasiriamali na umegoma
kujiendeleza, utashindwa sana, kwa sababu kwenye ujasiriamali zipo changamoto
nyingi na zinazotaka kichwa chako kiwe kizuri.Na kwa sababu ya changamoto hizo inatakiwa muda wote uwe bora na pia wanaokuzunguka wawe bora. Yote haya utayapata kwa wewe kuamua kujifunza na kujinoa.
Jambo # 4. Kabla hujaacha kazi, jifunze kidogo elimu ya uhasibu.
Kwa kujifunza elimu hii, itakusaidia sana kujua mtiririko
wa pesa katika biashara, pia itakusaidia kujua bajeti ya biashara na yako
kitaalamu zaidi, tofauti na ungekuwa hujui.
Kama kwako ni ngumu kujifunza elimu hii, basi, biashara ikikua kidogo, ajiri angalau mhasibu anayejua vizuri na uwe unamlipa. Hii itakusaidia kujenga biashara yako kwa mafanikio.
Hata kwa hatua unazochukua inatakiwa zidhihirishe kile kilicho moyoni mwako. Kama mafanikio moyoni huyaoni usijaribu kuacha kazi, maana hata kwenye ujasiriamali hutafanikiwa pia.
Kama utachagua kuuza bidhaa zako kwa bei ya juu, pia jifunze kutoa huduma bora. Kama huelewi hili vizuri, nenda kwenye hotel zinazotoa huduma kwa bei ya juu uone vizuri kile wanachokifanya ni nini kwenye biashara zao.
Tunaambiwa asilimia kubwa ya watu wengi huwa tunazaliwa hatujui kuuza. Hata hivyo unaweza kujifunza kuuza ili uwe mjasiriamali mzuri, vinginevyo utakwama. Anza kujifunza kuuza, utafanikiwa.
Kama kwako ni ngumu kujifunza elimu hii, basi, biashara ikikua kidogo, ajiri angalau mhasibu anayejua vizuri na uwe unamlipa. Hii itakusaidia kujenga biashara yako kwa mafanikio.
Jambo la #5. Kabla hujaacha kazi, kumbuka kuwa safari yako ya mafanikio inaanzia ndani ya moyo na roho yako.
Hapa kabla hujaacha kazi unatakiwa ujiulize, ndani mwako unaona mafanikio? Hii ikiwa na maana kwamba mafanikio yako lazima uyaone ndani kwanza kabla hayajaonekana kwa nje.Hata kwa hatua unazochukua inatakiwa zidhihirishe kile kilicho moyoni mwako. Kama mafanikio moyoni huyaoni usijaribu kuacha kazi, maana hata kwenye ujasiriamali hutafanikiwa pia.
Jambo #6. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa ujue, kitu chochote unachotaka kukiuza, kina bei tatu za msingi. Bei ya chini, bei ya kati na bei ya juu.
Kama utachagua kuuza kitu hicho kwenye bei ya chini, unatakiwa ujue pia dakika yoyote ataibuka mtu wa kushindana na wewe. Ili uwe mshindi katika kuuza kwa bei ya chini unatakiwa uwe na njia nzuri sana ya kuuza bidhaa yako.Kama utachagua kuuza bidhaa zako kwa bei ya juu, pia jifunze kutoa huduma bora. Kama huelewi hili vizuri, nenda kwenye hotel zinazotoa huduma kwa bei ya juu uone vizuri kile wanachokifanya ni nini kwenye biashara zao.
Jambo #7. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa kujua na kukumbuka, mauzo=kipato.
Kama utakuwa unataka kuacha kazi na ukajigundua kwenye mauzo haupo vizuri., nikwambie tu, jifunze kuuza kwanza, halafu ndo uache kazi. Kama huwezi kuuza, hiyo ni shida kwako kufanikiwa.Tunaambiwa asilimia kubwa ya watu wengi huwa tunazaliwa hatujui kuuza. Hata hivyo unaweza kujifunza kuuza ili uwe mjasiriamali mzuri, vinginevyo utakwama. Anza kujifunza kuuza, utafanikiwa.
Jambo # 8. Kabla hujaacha kazi, unatakiwa kujua vizuri jinsi ya kutumia pesa zako vizuri.
Ni wazi wajasiriamali walio wengi, hawajui jinsi ya kutumia pesa zao vizuri. Wanajikuta wanatumia tu pesa hawajui zitarudi vipi. Sasa usiingie kwenye mtego huo.Ili uwe mjasiriamali mwenye mafanikio, unatakiwa kujua kila shilingi ya pesa yako inakwenda wapi. Ukiona unafika sehemu unashangaa pesa zako zimeenda wapi, bado hujajua jinsi ya kuzitumia.
Jambo #9. Kabla hujaacha kazi, anzisha biashara ya pembeni kwa ajili ya kujifunza ujasiriamali.
Hakuna ambae anaweza akaendesha baiskeli pasipo kujifunza. Hata kwenye biashara mambo yako hivyo, unatakiwa uwe na biashara ya mazoezi kabla hujaacha kazi na kuingia kwenye ujasiriamali.Usije ukafanya kosa la kuacha kazi, wakati hata hujui ABC za ujasiriamali ziko vipi. Ukiwa unafanya biashara huku umeajiriwa, itakupa ukomavu wa wewe kufanikiwa kibiashara.
Jambo #10. Kabla hujaacha kazi, tafuta mshauri wa mafanikio/mentor.
Ni ngumu sana kwa wajasiriamali wengi, kuwa na mshauri wa mafanikio, lakini kabla hujaamua kuacha kazi, hakikisha una mshauri huyu wa mafanikio ambae atakuongoza katika njia sahihi.Kama unaona kumpata mshauri wako wa mafanikio ni ngumu, basi amua kufanya vitabu viwe ndo mshauri wako. Kwenye vitabu unatakiwa kujifunza sana na itakusaidia kufanikiwa.
Jambo #11. Kabla hujaacha kazi, tafuta mtandao wa wajasiriamali.
Usije ukakimbilia kwenye ulimwengu wa ujasiriamali, kama huna mtandao wa ujasiriamali. Kitendo cha kuwa na mtandao huu, kitakusaidia sana wewe katika safari yako ya kimafanikio.Inakubidi utafute mtandao, ambao kwako unaona unakufaa na kukusaidia. Kila wakati jumuika katika mikutano yao ili kupata uzoefu utakaokujenga, kukulea na kukusaidia kufikia malengo.
Jambo #12. Kabla hujaacha kazi, tazama mtazamo wako.
Ukijua hili, au ukaamua kuingia na mtazamo huu, wa kutambua changamoto za ujasiriamali, utakusaidia kupambana na changamoto zinazojitokeza.
Mwisho; kabla hujaacha kazi, unatakiwa uwe na imani sahihi kwenye ujasiriamali na kuielewa vizuri, misingi sahihi ya ujasiriamali.
Sunday, July 5, 2020
Saturday, July 4, 2020
Subscribe to:
Posts (Atom)