Rafiki yangu mpendwa,
Huwa tunajenga tabia, halafu tabia zinatujenga, chochote ambacho unafanya sasa, ni tabia ambayo umejijengea siku za nyuma.
Mafanikio au kushindwa kwako ni matokeo ya tabia zako. Kama ukiwa na tabia bora utafanikiwa na ukiwa na tabia mbovu utashindwa.
Moja
ya tabia muhimu unazopaswa kujijengea ili uweze kufanikiwa ni tabia ya
kujisomea, ambayo itakupa maarifa bora na utakapoyatumia utaweza kupiga
hatua zaidi.
Wengi wamekuwa wanasema wangependa sana kusoma
vitabu, lakini hawana muda wa kufanya hivyo. Na mimi nimekuwa nawaambia
siyo kweli kwamba hawapati muda, ila tu hawajaamua kusoma vitabu.
Hebu
niambie unapataje muda wa kula milo mitatu kila siku, kuoga, kufuatilia
habari na hata kulala? Ni kwa sababu vitu hivyo umevipa kipaumbele na
vimeshakuwa tabia kwako.
Kadhalika kwenye usomaji, ukiupa kipaumbele na kujenga tabia, utakuwa msomaji mzuri sana.
Kwa
upande wa kipaumbele hilo lifanye kwa kujiwekea ratiba nzuri, kila siku
tenga muda wa kujisomea, unaweza kuanza na nusu saa au saa moja na pia
unaweza kwenda mpaka masaa mawili na zaidi.
Kwa upande wa
kuijenga tabia ya kujisomea, hapa tunakwenda kujifunza hatua nne za
kutumia kujenga tabia hii. Karibu ujifunze na uchukue hatua na utaweza
kuwa msomaji mzuri na kunufaika na maarifa unayoyapata.
( 1 ).TENGENEZA MWONEKANO.
Sisi
binadamu huwa tunafanya kile ambacho tunakiona, kile tusichokiona huwa
hatuhangaiki nacho, huwa hata hakipati nafasi kwenye fikra zetu.
Hivyo ili mipango ya kusoma ipate nafasi kwenye fikra zetu, lazima tutengeneze mwonekano wa yale yanayohusiana na kusoma.
Kitu
cha kwanza kufanya ni kuwa na kitabu popote pale unapokuwepo, na
usikiweke kwenye begi lako, bali kishike mkononi. Kwa kuwa umebeba
kitabu, ni rahisi kukifungua na kusoma kurasa chache pale unapopata
muda, kuliko ukiwa huna kitabu.
Unafikiri kwa nini unashika simu
yako muda mwingi? Ni kwa sababu uko nayo. Ukikaa kwenye foleni kidogo tu
unatoa simu na kuangalia, sasa badili hilo kwa kuwa na kitabu.
Najua kuna vitabu vya nakala tete, lakini katika kujijengea tabia ya kusoma, kuwa na nakala ngumu na tembea nayo popote.
Njia
nyingine ya kutengeneza mwonekano ni kuwa na maktaba ndogo nyumbani
kwako. Kama nyumbani kwako una tv, basi pia unapaswa kuwa na vitabu, na
viweke pembeni ya tv yako. Kwa kuiona tv ambayo inakuvutia kuangalia,
pembeni yake utaviona vitabu ambavyo vitakukumbusha lengo lako la kusoma
zaidi.
Je umekuwa unatumia simu ukiwa kitandani? Kama jibu ni
ndiyo, basi ni kwa sababu unaenda na simu hiyo kitandani. Hapa pia kuna
fursa ya kutumia mwonekano kusoma zaidi. Badala ya kwenda kitandani na
simu, wewe nenda na kitabu. Soma kurasa chache kabla ya kulala. Na hata
wale ambao usingizi unawasumbua, ukienda na kitabu kitandani utapata
usingizi haraka sana.
Tengeneza mwonekano ambao unakufanya ukione kitabu kila wakati na hilo litakusukuma kusoma zaidi.
( 2). TENGENEZA MVUTO.
Huwa
tunafanya kile ambacho kinatuvutia kufanya, hivyo kwenye kujenga tabia
ya kusoma vitabu, ufanye usomaji kuwa na mvuto kwako.
Zipo njia mbalimbali unazoweza kuzitumia kutengeneza mvuto kwenye usomaji.
Anza
kwa kuweka kusoma kama kigezo cha wewe kufanya kile ambacho unapenda
kufanya. Mfano kama unapenda sana kuangalia tv, basi weka lengo kwamba
utaweza kuangalia tv kama tu utakuwa umesoma kurasa 5 za kitabu. Hili
linafanya usomaji uwe na mvuto kwako, kwa sababu unakupeleka kufanya
kile unachopenda kufanya.
Njia nyingine unayoweza kutumia
kutengeneza mvuto kwenye usomaji ni kujiunga na watu ambao ni wasomaji.
Unapowaona wengine wanasoma, na wewe unasukumwa kusoma pia. Unapoona
wengine wameshirikisha vitabu walivyosoma, na wewe unapata mvuto wa
kusoma ili ushirikishe pia.
Tumia kila fursa unayoipata kuufanya
usomaji uwe na mvuto kwake, kiwe kitu ambacho unapendelea kukifanya
kabla ya kufanya vitu vingine.
( 3 ). UFANYE USOMAJI KUWA RAHISI.
Kitu
chochote ambacho kina mlolongo mrefu huwa hatukipendi, na hivyo
hatukifanyi. Kitu chochote ambacho kinahitaji nguvu au kinaumiza huwa
tunakwepa kukifanya.
Hivyo ili kujijengea tabia ya kusoma vitabu,
rahisisha usomaji wako, ufanye usomaji kuwa rahisi, kwa kupunguza
milolongo na kuondoa kazi au maumivu kwenye usomaji.
Punguza
milolongo kwa kujiwekea masharti machache, kwamba ukipata muda ambao ni
kuanzia dakika 5 na kuendelea, basi utafungua kitabu na kusoma, na hapo
kitabu umekibeba muda wote. Usijiambie ni mpaka uwe umekaa, uwe na vitu
gani ndiyo usome, wewe jiambie unapopata muda utafungua kitabu na
kusoma, kisha fanya hivyo.
Ondoa ugumu kwenye usomaji kwa
kuyafanya mazingira kuwa rahisi kusoma. Kama umetenga ratiba ya kusoma
kwa umakini, basi hakikisha unakuwa kwenye mazingira ambayo yanachochea
hilo. Kuwa eneo tulivu na simu yako iwe kwenye ukimya. Ukipata dakika 10
za kusoma eneo ambalo husumbuliwi, utajifunza mengi kuliko saa nzima ya
kusoma eneo ambalo unasumbuliwa na kukatishwa mara kwa mara.
Tumia
teknolojia kurahisisha usomaji wako. Kama unasoma nakala tete, unaweza
kuboresha zaidi usomaji wako kupitia programu mbalimbali. Mfano kuweka
lengo la kufikia kurasa fulani, kukumbushwa kuhusu mpango wako wa kusoma
na hata kuchukua kumbukumbu kwa urahisi wakati wa kusoma.
Angalia ni vitu gani vinakupa ugumu kwenye kusoma sasa, kisha ondoa ugumu huo na utaweza kujijengea tabia nzuri ya usomaji.
SOMA; Kama Unataka Kufanikiwa 2020 Achana Na Malengo Na Kazana Na Kitu Hiki Kimoja.
( 4 ). PATA UFAHARI KUPITIA USOMAJI WAKO.
Sisi
binadamu huwa tunafanya kile ambacho kinatupa raha, na kuepuka kile
ambacho kinatupa maumivu. Hivyo ili uendelee kufanya kitu, lazima kiwe
kinakupa raha.
Na hivyo ndivyo ilivyo kwenye usomaji, hakikisha
usomaji wako unakupa raha na hapo utasukumwa kusoma zaidi. Zipo njia
mbalimbali za kupata raha kupitia usomaji.
Washirikishe wengine
kile ambacho umejifunza. Unaposoma kitabu, chagua mambo yasiyopungua
kumi ambayo unaweza kuwaambia watu umejifunza kwenye kitabu hicho.
Washirikishe kwenye maongezi, kwa maandishi na njia nyinginezo.
Weka
orodha ya vitabu ulivyosoma na washirikishe wengine. Nafikiri utakuwa
umeona jinsi ambavyo mwisho wa mwaka kila mtu anaorodhesha vitabu
alivyosoma, na jinsi watu wanavyowasifia kwa kuweza kusoma vitabu hivyo
vingi. Litumie hili kwa manufaa yako pia, na usisubiri mpaka mwaka
uishe, wewe unaweza kufanya kila siku, kila wiki, kila mwezi na
kadhalika. Cha kufanya, piga picha kitabu unachosoma kisha weka kwenye
mitandao unayotumia na waambie watu unasoma kitabu hicho. Watajitokeza
watu wa kukusifia na hilo litakufanya ujisikie vizuri. Pia kila wiki au
mwezi unaweza kuorodhesha vitabu ulivyosoma na watu wanavyokusifia au
kujadili kunakufanya ujisikie vizuri na uendelee kusoma zaidi.
Njia
nyingine ya kujisikia vizuri kwenye usomaji ni kutoa nukuu na mifano
kutoka kwenye vitabu unavyosoma wakati wa maongezi. Unapokuwa unaongea
na wengine au kujadiliana mtandaoni na kwingineko, jenga hoja zako kwa
mifano na nukuu kutoka kwenye kitabu ulichosoma. Hii itakufanya ujisikie
vizuri kwa ubora wa hoja utakazokuwa umeshirikisha.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Sunday, January 12, 2020
Wednesday, January 8, 2020
Tuesday, January 7, 2020
Sunday, January 5, 2020
Saturday, January 4, 2020
VITU 02 VYA KUFANYA ILI UWE NA MAISHA MAREFU
Ili uweze kuwa na maisha marefu na kuepuka kufa
kabla ya muda wako, kuna vitu viwili muhimu sana unavyopaswa kuvifanya.
( 1 ). ISHI KWA MATUMAINI.
Lazima
uwe na matumaini makubwa kwenye maisha yako, lazima uwe na kitu kikubwa
unachokifanyia kazi, kinachokupa matumaini kwamba maisha ya kesho
yatakuwa bora kuliko maisha ya leo. Haijalishi ni hali ngumu kiasi gani
unayopitia, unapokuwa na matumaini ya kitu bora zaidi siku zijazo,
unapata nguvu ya kuendelea kupambana na maisha yako kuendelea.
Matumaini
yanajengwa kutoka kwenye maana ya maisha ambayo mtu unakuwa nayo, kwa
kujua kusudi lako hapa duniani, kisha kuwa na maono na ndoto kubwa
ambazo unazifanyia kazi. Kwa kujua kwamba kuna kitu umeletwa kufanya
hapa duniani, na kuona jinsi ambavyo kinawagusa wengine, unakuwa na
matumaini makubwa.
Na
hata kama hujajua maana au kusudi la maisha yako, basi jiwekee lengo
lolote kubwa ambalo litakusukuma sana kulifikia, kisha jikumbushe lengo
hilo kila siku na amini utalifikia.
Wapo
watu wengi ambao walijiwekea malengo makubwa, wakajituma sana na
kuyafikia, lakini baada ya kufikia malengo hayo wakafariki dunia. Hii ni
kwa sababu kufanyia kazi lengo ndiyo ulikuwa msukumo mkubwa kwao,
lakini baada ya kufikia lengo wakakosa msukumo na hivyo kukaribisha
kifo.
Usikubali
kukaribisha kifo rafiki yangu, kila wakati jua maana na kusudi la
maisha yako, kuwa na maono makubwa unayotaka kufikia na jiwekee malengo
makubwa. Na kila unapofikia lengo ulilojiwekea, weka lengo jingine kubwa
zaidi ya hilo. Maisha yako yakikosa mahali pa kupata matumaini,
yanakuwa mafupi.
( 2 ). KAMWE USIKATE TAMAA.
Haijalishi
umekutana na nini, haijalishi unapitia hali gani, usikubali kabisa
kukata tamaa, wala usiruhusu fikra hasi na za wasiwasi kuingia kwenye
akili yako. Kila wakati jikumbushe kusudi la maisha yako, kumbuka maono
yako na malengo uliyojiwekea na hilo litaondoa hali ya kukata tamaa.
Dunia
haitakupa kila unachotaka kwa wakati unaotaka wewe. Utaweka mipango
yako vizuri, lakini matokeo utakayokuja kupata yatakuwa ya tofauti
kabisa. Utakuwa na mategemeo fulani, lakini utakachokuja kupata ni
tofauti kabisa na mategemeo yako. Hivyo hakikisha hali hizo unazopitia
hazikukatishi tamaa, chukulia ni sehemu ya kawaida ya maisha na endelea
kuwa na matumaini kwamba kesho itakuwa bora kuliko leo, kisha nenda
kachukue hatua ili hiyo kesho iwe bora kweli.
Winston
Churchill ni mmoja wa watu walioweka juhudi kubwa na kuiwezesha vita
kuu ya pili ya dunia kumalizika. Moja ya kauli zake ambayo aliiamini
sana ilikuwa ni hii; “Never give in. Never give in. Never, never, never,
never—in nothing, great or small, large or petty—never give in, except
to convictions of honour and good sense. Never yield to force. Never
yield to the apparently overwhelming might of the enemy.” Akimaanisha
kawe usikate tamaa, kamwe, kamwe, kamwe, kwa chochote kikubwa au kidogo
bali kwa yale yaliyo sahihi. Kamwe usikatishwe tamaa na nguvu ya adui.
Jiambie
leo na jikumbushe hili kila siku; KAMWE SITOKATA TAMAA. Na ukiweza
kuishi hali hii kila siku, basi utakuwa na maisha marefu.
Ili
usikate tamaa zingatia haya; kuwa na maono makubwa, amini kwenye maono
hayo, usitake dunia iende kama unavyotaka wewe, pokea kila kinachokuja
kwako na kitumie vizuri na usiwe mtu wa kulalamika au kulaumu wengine.
Subscribe to:
Posts (Atom)