BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Wednesday, January 8, 2020
Tuesday, January 7, 2020
Sunday, January 5, 2020
Saturday, January 4, 2020
VITU 02 VYA KUFANYA ILI UWE NA MAISHA MAREFU
Ili uweze kuwa na maisha marefu na kuepuka kufa
kabla ya muda wako, kuna vitu viwili muhimu sana unavyopaswa kuvifanya.
( 1 ). ISHI KWA MATUMAINI.
Lazima
uwe na matumaini makubwa kwenye maisha yako, lazima uwe na kitu kikubwa
unachokifanyia kazi, kinachokupa matumaini kwamba maisha ya kesho
yatakuwa bora kuliko maisha ya leo. Haijalishi ni hali ngumu kiasi gani
unayopitia, unapokuwa na matumaini ya kitu bora zaidi siku zijazo,
unapata nguvu ya kuendelea kupambana na maisha yako kuendelea.
Matumaini
yanajengwa kutoka kwenye maana ya maisha ambayo mtu unakuwa nayo, kwa
kujua kusudi lako hapa duniani, kisha kuwa na maono na ndoto kubwa
ambazo unazifanyia kazi. Kwa kujua kwamba kuna kitu umeletwa kufanya
hapa duniani, na kuona jinsi ambavyo kinawagusa wengine, unakuwa na
matumaini makubwa.
Na
hata kama hujajua maana au kusudi la maisha yako, basi jiwekee lengo
lolote kubwa ambalo litakusukuma sana kulifikia, kisha jikumbushe lengo
hilo kila siku na amini utalifikia.
Wapo
watu wengi ambao walijiwekea malengo makubwa, wakajituma sana na
kuyafikia, lakini baada ya kufikia malengo hayo wakafariki dunia. Hii ni
kwa sababu kufanyia kazi lengo ndiyo ulikuwa msukumo mkubwa kwao,
lakini baada ya kufikia lengo wakakosa msukumo na hivyo kukaribisha
kifo.
Usikubali
kukaribisha kifo rafiki yangu, kila wakati jua maana na kusudi la
maisha yako, kuwa na maono makubwa unayotaka kufikia na jiwekee malengo
makubwa. Na kila unapofikia lengo ulilojiwekea, weka lengo jingine kubwa
zaidi ya hilo. Maisha yako yakikosa mahali pa kupata matumaini,
yanakuwa mafupi.
( 2 ). KAMWE USIKATE TAMAA.
Haijalishi
umekutana na nini, haijalishi unapitia hali gani, usikubali kabisa
kukata tamaa, wala usiruhusu fikra hasi na za wasiwasi kuingia kwenye
akili yako. Kila wakati jikumbushe kusudi la maisha yako, kumbuka maono
yako na malengo uliyojiwekea na hilo litaondoa hali ya kukata tamaa.
Dunia
haitakupa kila unachotaka kwa wakati unaotaka wewe. Utaweka mipango
yako vizuri, lakini matokeo utakayokuja kupata yatakuwa ya tofauti
kabisa. Utakuwa na mategemeo fulani, lakini utakachokuja kupata ni
tofauti kabisa na mategemeo yako. Hivyo hakikisha hali hizo unazopitia
hazikukatishi tamaa, chukulia ni sehemu ya kawaida ya maisha na endelea
kuwa na matumaini kwamba kesho itakuwa bora kuliko leo, kisha nenda
kachukue hatua ili hiyo kesho iwe bora kweli.
Winston
Churchill ni mmoja wa watu walioweka juhudi kubwa na kuiwezesha vita
kuu ya pili ya dunia kumalizika. Moja ya kauli zake ambayo aliiamini
sana ilikuwa ni hii; “Never give in. Never give in. Never, never, never,
never—in nothing, great or small, large or petty—never give in, except
to convictions of honour and good sense. Never yield to force. Never
yield to the apparently overwhelming might of the enemy.” Akimaanisha
kawe usikate tamaa, kamwe, kamwe, kamwe, kwa chochote kikubwa au kidogo
bali kwa yale yaliyo sahihi. Kamwe usikatishwe tamaa na nguvu ya adui.
Jiambie
leo na jikumbushe hili kila siku; KAMWE SITOKATA TAMAA. Na ukiweza
kuishi hali hii kila siku, basi utakuwa na maisha marefu.
Ili
usikate tamaa zingatia haya; kuwa na maono makubwa, amini kwenye maono
hayo, usitake dunia iende kama unavyotaka wewe, pokea kila kinachokuja
kwako na kitumie vizuri na usiwe mtu wa kulalamika au kulaumu wengine.
Subscribe to:
Posts (Atom)