- Ipo njia moja ya kupata chochote unachotaka na njia hiyo ni kuomba. Ombeni na mtapewa ni siri muhimu ya mafanikio kwenye biashara. Kama kuna kitu unataka, omba, na wengine watakuwa tayari kukupa. Huwezi kupata kitu bila kuomba.
- Unapoomba kazi, badala ya kutuma maombi kama wengine wanavyofanya, tafuta mikutano na wahusika wa eneo unalotaka kufanya kazi. Kwa kutumia mtandao wa kijamii wa LinkedIn, unaweza kukutana na mtu yeyote na ukaongeza nafasi zako za kupata kazi unayotaka.
- Biashara ni watu, haijalishi unajua nini, bali unamjua nani na nani anakujua wewe. Hivyo kazana kukuza zaidi mtandao wako wa watu unaowajua na wanaokujua.
- Mchukulie kila mtu unayekutana naye kama mtu mashuhuri, jua ni mtu muhimu, muoneshe umuhimu na watu watapenda kukutana na wewe. Ili kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kutengeneza marafiki wengi.
- Kutana na watu, furahia na jifunze. Weka kipaumbele chako katika kujenga mahusiano imara kwenye biashara yako na kazi yako, fanya kile ambacho unapenda ukiwa umezungukwa na watu unaowapenda. Pia jifunze kupitia wale ambao unafanya nao kazi na wanaokuzunguka.
- Kuwa mtu wa shukrani, kila unapokutana na mtu, au mtu anapokufanyia kazi, chukua muda wa kumwandikia ujumbe wa shukrani, inaimarisha zaidi mahusiano yako.
- Wale uliosoma nao shule moja au chuo kimoja ni watu muhimu sana kwenye mafanikio yako. Kuwa nao karibu na tengenezeni mahusiano bora, kila mtu anaweza kunufaika kupitia kazi za wengine. Kama hakuna umoja wa wale mliosoma pamoja, una fursa nzuri ya kuuanzisha.
- Wafuatilie watu baada ya kukutana nao. Unapokutana na kujuana na mtu mara ya kwanza, endelea kuwafuatilia kwa mawasiliano, hili linaimarisha mahusiano mnayokuwa mmeanzisha.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Thursday, June 27, 2019
MAHUSIANO NI MUHIMU KULIKO BIDHAA KATIKA BIASHARA
Wednesday, June 26, 2019
Tuesday, June 25, 2019
SABABU TANO ( 5 ) ZINAZOUA BIASHARA NYINGI KUKUA
(1). MMILIKI WA BIASHARA.
Mmiliki
wa biashara ni kikwazo cha kwanza kabisa kwenye ukuaji wa biashara.
Pale ambapo biashara inamtegemea mmiliki wa biashara hiyo kwenye kila
kitu haiwezi kukua. Kama mwanzilishi wa biashara ndiye anayetegemewa
kufanya kila kitu kwenye biashara, biashara haiwezi kukua.
Ili
biashara kukua lazima mmiliki aweze kujitofautisha na kujitenganisha na
biashara hiyo. Ajenge biashara ambayo inaweza kujiendesha yenyewe bila
ya uwepo wake.
Biashara
inakua kwa kutengeneza wateja wapya kila wakati. Biashara nyingi
zimekuwa hazina mfumo mzuri wa kutengeneza wateja wapya kila wakati.
Hivyo wanaendelea kuwa na wateja wale wale na hilo linakuwa kikwazo
kikubwa kwenye ukuaji.
Ili biashara ikue lazima iwe inatengeneza wateja wapya kila wakati. Wateja wapya ndiyo wanaoleta ukuaji wa biashara.
( 3 ). KUKOSA WAFANYAKAZI BORA.
Wafanyakazi
wa biashara ndiyo wanaoweza kuikuza au kuiangusha. Biashara nyingi
hazina wafanyakazi sahihi na hilo limekuwa linazizuia biashara hizo
kukua.
Wafanyabiashara
wengi hawana mfumo mzuri wa kuajiri watu sahihi kwenye biashara zao na
hilo limekuwa linawagharimu kwenye ukuaji. Ili biashara ikue, inahitaji
kuwa na wafanyakazi bora ambao wanaweza kutekeleza majukumu yao vizuri.
( 4 ). MZUNGUKO HASI WA FEDHA.
Fedha ndiyo damu ya biashara, mzunguko wa fedha ukiwa vizuri biashara inakua, ukiwa vibaya biashara inakufa.
Biashara nyingi zinazokufa zina mzunguko hasi wa fedha, ikiwa na maana kwamba matumizi ya biashara ni makubwa kuliko mapato.
Ili
biashara ikue, inahitaji kuwa na mfumo bora wa kudhibiti mzunguko wa
fedha ili uwe chanya. Mapato yawe makubwa kuliko matumizi.
( 5 ). MAUZO YASIYOTOSHELEZA.
Mauzo
ndiyo injini au moyo wa biashara. Mauzo ndiyo yanayosukuma mzunguko wa
fedha kwenye biashara. Bila ya mauzo hakuna biashara.
Biashara nyingi zimekuwa hazina mauzo ya kutosheleza kuzalisha mapato yanayoiwezesha biashara hiyo kujiendesha kwa faida.
Biashara hizo hazina mfumo bora wa masoko ambao unawezesha mauzo kuwa mazuri na yanayoiwezesha biashara kujiendesha yenyewe.
Rafiki,
hizi ndizo sababu tano kubwa zinazozuia biashara nyingi kukua,
ukizikabili sababu hizi tano, biashara yako itaweza kukua sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)