BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Saturday, June 15, 2019
Friday, June 14, 2019
KILA HATUA UNAYOPIGA HUZALISHA KIKWAZO
Kwenye fizikia, kuna kanuni tatu kuu za mwendo ambazo mwanasayansi Isaac Newton alizigundua.
Kanuni ya kwanza inasema kitu kilichopo kwenye mwendo kinaendelea kuwa kwenye mwendo mpaka nguvu ya nje itakapotumika kukizuia.
Kanuni ya pili inasema nguvu ya kitu kilichopo kwenye mwendo inategemea uzito wake na mwendokasi wake.
Na kanuni ya tatu inasema kila mwendo huwa unazalisha upinzani.
Ni
kanuni ya tatu ambayo tunakwenda kuijadili hapa kwenye dakika moja ili
uelewe kwa nini baadhi ya vitu vinatokea kwenye maisha yako na hatua
sahihi kwako kuchukua.
Kila mwendo unaoanzisha, kuna mwendo mwingine utakaoanzishwa kuzuia mwendo huo.
Unapojaribu kwenda mbele, kuna mtu atajitokeza kukurudisha nyuma.
Hii ndiyo inasababisha mafanikio kuwa magumu. Kwa
sababu siku unayoamua kwamba unataka kufanikiwa, zitaibuka kila aina ya
nguvu kukupinga, kutaibuka kila kikwazo kwenye njia yako ya mafanikio.
Unapojua
hili, unajipanga kwa upinzani kwa kila hatua unayopanga kupiga na
hujidanganyi kwamba mambo yataenda vizuri yenyewe kama wengi
wanavyofanya.
Usishangae pale ambapo marafiki ulionao sasa watageuka kuwa maadui zako pale unapotangaza kwamba unataka kufanikiwa sana. ulipokuwa
kawaida mlikuwa marafiki, unapopanga kupiga hatua zaidi wanakuwa
maadui, hiyo ni kanuni ya asili, huwezi kupingana nayo.
Usikubali
kipingamizi chochote kikuzuie wewe kupiga hatua zaidi kwenye maisha
yako, jua kwa kila hatua utakayopanga kuchukua kuna kipingamizi
kitaibuka na hivyo jiandae kukivuka.
KILA MTU ATAKUFA , NI BORA UULIWE NA KAZI !
Kila mtu atakufa, hilo halina ubishi. Hii ni hukumu uliyoipata siku unayozaliwa, ambacho hujui ni siku gani hukumu hiyo itakamilika.
Lakini kuna kitu kingine muhimu sana kuhusu kifo ambacho wengi tumekuwa hatukitafakari, ambacho tukikielewa kitatusaidia sana.
Kila mtu kuna kitu kitakachomuua. Ndiyo, kuna kitu ambacho kitakuua, yaani kitachangia kwenye kifo chako.
Kuna ambao ulevi utawaua, kwa kuendekeza sana ulevi mwili unachoka na kupata magonjwa ambayo yanachangia kifo chao.
Kuna ambao chakula kitawaua, kwa kushindwa kula kwa nidhamu wanakuwa na afya mbovu ambayo inaleta magonjwa yanayowaua.
Kuna
ambao wasiwasi na hofu vitawaua, kwa kuwa na wasiwasi na hofu mara zote
kunaufanya mwili uwe haifu na hivyo kushindwa kuhimili magonjwa
mbalimbali.
Kuna
ambao mapenzi yatawaua, kwa kushindwa kudhibiti hisia zao za mapenzi na
ngono wanajikuta kwenye hatari zinazoondoa maisha yao.
Kuna
ambao kazi zitawaua, kwa kuweka muda na nguvu zao nyingi kwenye kazi
zao kunachosha miili yao na kuibua magonjwa yatakayowaua.
Kuna
ambao uvivu utawaua, kwa kukaa muda mrefu na kutokuwa na majukumu
makubwa, mwili unakuwa mzembe na kushindwa kupambana na magonjwa na hilo
kupelekea kifo.
Ndugu yangu, hakuna atakayetoka hapa duniani akiwa hai, na kila mtu kuna kitu ambacho kitamuua.
Wito wangu kwako, chagua sumu yako vizuri, kile ambacho kitakuua, basi kiwe na maana kwako na hata wengine pia. Kuliko uuliwe kwa pombe, ulevi au ngono, ni bora uuliwe na kazi, maana kazi hiyo itakuwa na maana kwako na kwa wengine pia.
TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA SANA
(1). HAMASA.
Sifa
ya kwanza ambayo watu waliofanikiwa wanaitaka kuwepo kwenye kile
wanachofanya na chenye maana kwao ni hamasa. Wanapokuwa na nafasi ya
kuchagua kipi cha kufanya, wale waliofanikiwa sana wanachagua kile
ambacho wana hamasa kubwa ndani yao ya kukifanya.
Kitu
hicho wanakuwa wanakipenda kutoka ndani ya mioyo yao na hivyo kusukumwa
kukifanya vizuri kuliko wengine. Wanakuwa tayari kukifanya muda wote
bila ya kuchoka na hawaangalii sana ni kiasi gani wanalipwa katika
kukifanya.
Unapofanya
kile unachopenda kufanya, kile ambacho una hamasa kubwa ndani yako
kukifanya, unakuwa hufanyi kazi, bali unafanya maisha na hivyo nafasi ya
wewe kufanikiwa inakuwa kubwa zaidi.
Kila
siku jiulize swali hili muhimu; ni kitu gani kinanipa hamasa kubwa
kwenye maisha yangu, kazi yangu na biashara yangu? Kisha nenda kafanye
hicho, utazalisha matokeo bora zaidi kuliko wengine na hilo
litakuwezesha kufanikiwa zaidi.
Mahusiano
ya kijamii ni muhimu sana kwenye maana ya maisha. Wale wanaokuwa
wametengwa na watu wengine huwa wanaripoti maisha yao kupoteza maana.
Maana ya maisha yetu ni matokeo ya vile ambavyo wengine wanapokea kile
tunachofanya.
Watu
waliofanikiwa sana wamekuwa wakichagua kwa umakini watu wanaojihusisha
nao kwenye kazia au biashara wanazofanya. Wanafanya kazi au biashara
zinazowawezesha kutengeneza mahusiano bora na wale ambao wanawapenda,
wale ambao tabia walizonazo zinaendana nao.
Watu
waliofanikiwa pia huwa wanapenda kuzungukwa na watu wanaowapa
changamoto ya kupiga hatua zaidi. Hivyo wanafanya kazi au biashara
ambayo wamezungukwa na watu wanaofanikiwa na wanaopiga hatua kufanikiwa
zaidi. Watu hawa wanakuwa msukumo kwao kupiga hatua zaidi.
Usikubali
kufanya kazi au biashara ambayo wengi unaoshirikiana nao hamuendani
kitabia wala kimtazamo, itakuwa kikwazo kikubwa kwako kufanikiwa. Lakini
pia kazana kuzungukwa na watu ambao wanakusukuma uwe bora zaidi,
zungukwa na watu ambao wanapiga hatua zaidi ili iwe chachu kwako kupiga
hatua zaidi.
Mahusiano
yako na wengine kwenye kazi au biashara unayofanya yanapokuwa mabovu,
maisha yako yanakuwa mabovu pia na hilo linachangia maisha yako kukosa
maana.
( 3 ).KURIDHIKA.
Maisha
yanakuwa na maana pale ambapo kile unachofanya kinakuridhisha, pale
moyo wako unaporidhika na kile unachofanya unafurahia maisha yako na
kuona yana maana kubwa.
Watu
waliofanikiwa sana wamekuwa wanachagua kufanya kazi au biashara ambayo
inawapa hali ya kuridhika, na hilo limekuwa linawawezesha kufanikiwa
zaidi kupitia kile wanachofanya.
Kuridhika kwenye kile tunachofanya kunachangiwa na vitu viwili;
Moja
ni ukuaji binafsi. Huwa tunaridhika pale ambapo kile tunachofanya
kinatusukuma kukua zaidi ya pale tulipo sasa. Kama unajiona ukipiga
hatua kadiri unavyokwenda, unaridhika zaidi.
Mbili
ni mchango kwa wengine. Huwa tunaridhika pale ambapo kile tunachofanya
kinakuwa na mchango kwa wengine. Pale wengine wanapotushukuru kwa kile
tunachofanya, tunaridhika sana.
Hivyo
chagua kazi au biashara ambayo inakupa nafasi ya kukua zaidi, ambayo
unapiga hatua kadiri unavyokwenda na siyo kudumaa au kushuka chini. Pia
kazi au biashara hiyo iwe inagusa maisha ya wengine, inaongeza thamani
kwa wengine na kuwafanya kuwa bora kuliko walivyokuwa. Watu hao
wanapokushukuru kwa mchango ambao umekuwa nao kwao, unaridhika sana na
maisha yako yanakuwa na maana.
( 4 ). UMUHIMU.
Kila
tunachofanya au kinachotokea kwenye maisha yetu, huwa tunakilinganisha
na maeneo mengine ya maisha yetu. Kama kitu hicho kinaendana na maeneo
mengine ya maisha yetu, basi tunaona maisha yetu yanakuwa na maana
kubwa. Lakini kama kinachotokea hakiendani na maeneo mengine ya maisha
yetu, maana inakosekana.
Watu
waliofanikiwa sana wamekuwa wanachagua kufanya vitu ambavyo ni muhimu
kwao, ambavyo vinaendana na haiba zao, sifa zao na hata maeneo mengine
ya maisha yao.
Kama
mtu anajichukulia kuwa mwaminifu, kazi au biashara inayojenga mazingira
ya uaminifu inakuwa muhimu zaidi kwake na kuleta maana kwake. Lakini
mtu huyo akafanya kazi ambayo haina uaminifu, anaweza kupata fedha,
lakini ndani yake atakosa maana, kwa sababu kile anachofanya hakiendani
na vile yeye alivyo.
Chagua
kufanya kazi au biashara ambayo inaendana na wewe, ambayo inatumia na
kukuza zile sifa binafsi zilizopo ndani yako na pia inachangia katika
kuyakamilisha maisha yako. Yaani ukiangalia kila unachofanya,
kinachangia maisha yako kukamilika.
Rafiki,
hizo ndiyo sifa nne za kuangalia wakati unachagua kazi au biashara ya
kufanya ili iwe na maana kwako na uweze kufanikiwa zaidi.
Kama
tayari upo kwenye kazi au biashara ambayo unaona haina maana kwako, una
hatua mbili za kuchukua ili uweze kupata maana na kufanikiwa zaidi.
Hatua
ya kwanza ni kutafuta maana kwenye kazi au biashara hiyo. Huenda
hujapata maana kwa sababu hujaitafuta, umekuwa unafanya tu kwa mazoea
siku zote na hivyo hujawahi kutafakari na kuona maana. Anza kwa
kuangalia sifa hizi nne kwenye kile unachofanya, jiulize ni kitu gani
kinakupa HAMASA sana kwenye kazi au biashara unayofanya. Angalia wale
ambao UNAHUSIANA nao kupitia kazi au biashara hiyo na ona ni watu gani
bora zaidi unaoweza kutengeneza nao mahusiano. Tafuta KURIDHIKA kwa
kukua zaidi na kufanya maisha ya wengine kuwa bora kupitia kazi au
biashara unayofanya. Na mwisho angalia ni jinsi gani kazi au biashara
hiyo ina UMUHIMU kwenye maisha yako, angalia inayakamilishaje maisha
yako kwa kuendana na sifa zako nyingine.
Hatua
ya pili ni kuondoka kwenye kazi au biashara hiyo na kwenda kufanya ile
yenye maana kwako. Kama umejifanyia tathmini na hujaweza kupata maana
kwenye kazi au biashara unayofanya sasa, kuendelea kubaki hapo
hakutaleta maana kwenyewe. Badala yake chukua hatua ya kuondoka kwenye
kazi au biashara hiyo na kwenda kufanya ile ambayo ina maana kwako. Hata
kama hutaweza kuondoka kwa haraka, lakini lengo linapaswa kuwa
kutengeneza maisha yenye maana.
Thursday, June 13, 2019
Subscribe to:
Posts (Atom)