Lakini
 pia biashara huwa inakuwa na tabia zake, ambazo zinaweza kuifanya 
ifanikiwe zaidi au kuizuia isifanikiwe. Tabia hizi za biashara huwa 
zinatokana na tabia ambazo mwanzilishi wa biashara hiyo anazo
Na
 hii ndiyo maana kwenye kila biashara kuna utaratibu na utamaduni fulani
 uliopo, ambao huwa ni mgumu sana kubadilisha. Hata wafanyakazi wapya 
wanapokuja kufanya kazi kwenye biashara hiyo, baada ya muda hujikuta 
wameshavaa utamaduni huo wa biashara.
Utaratibu
 na utamaduni uliojengeka kwenye biashara nyingi huwa ni matokeo ya 
tabia za mwanzilishi wa biashara, huwa siyo kitu ambacho kimetengenezwa 
kwa makusudi ambacho kinaweza kuwa na msaada kwenye biashara hiyo.
Hivyo
 unakuta biashara imejijengea tabia ambazo siyo nzuri na zinakuwa 
kikwazo kwa maendeleo ya biashara hiyo. Ukiangalia tabia za biashara 
hiyo, zinakuwa zinaendana sana na tabia za mwanzilishi wa biashara hiyo.
Mfano
 kama mwanzilishi wa biashara ni mzito kwenye kufanya maamuzi, basi 
ufanyaji wa maamuzi wa kila mtu kwenye biashara unakuwa ni mzito sana. 
Maamuzi hayafanyiki kwa wakati na biashara inazikosa fursa nzuri za 
kukua zaidi.
Kama
 mwanzilishi wa biashara hawezi kupangilia vitu vyake vizuri kwenye 
maisha yake binafsi, unakuta biashara nayo haina mpangilio mzuri, vitu 
vipo hovyo hovyo na hakuna utaratibu wowote unaotumika kwenye kufanya 
vitu.
Kama
 mwanzilishi wa biashara ana tamaa, biashara nzima inaendeshwa kwa 
tamaa, kila aliyepo kwenye biashara hiyo anakuwa na tamaa na kujali 
mambo yake zaidi kiliko ya biashara.
Hivyo
 popote ambapo biashara imekwama, kwa hakika ndipo ambapo mmiliki wa 
biashara hiyo amekwama. Biashara haiwezi kukua zaidi ya ukuaji wa 
mmiliki wa biashara hiyo.
