Rafiki,
kama kuna hatua moja ambayo unapasa kuichukua, hata kama utashindwa
kuchukua hatua nyingine zozote kwenye ulaji wako, basi ni kuachana
kabisa na sukari. Yaani acha kabisa kutumia sukari, na utaupumzisha
mwili wako na hali hii ya kutengeneza sumu ambazo zinakuchosha,
kukuletea magonjwa na hata kukuzeesha haraka.
Vyakula
vya sukari vya kuepuka ni kama ifuatavyo, sukari yoyote unayoongeza
kwenye chai au chakula, asali, miwa na juisi yake, matunda yoyote yenye
utamu wa sukari, soda, juisi za matunda hata kama ni asili, bia, mvinyo,
bidhaa zozote za kiwandani ambazo zimetengenezwa kwa kuongezwa sukari,
kama mikate, maandazi na chochote ambacho kimeongezwa sukari.
Pia
punguza sana matumizi yako ya vyakula vya wanga, kwa kula kiasi kidogo
sana na mara moja kwa siku, hasa mlo wa jioni au usiku. Sehemu kubwa ya
chakula chako inapaswa kuwa mafuta sahihi, protini na mbogamboga.
Nyongeza;
usidanganyike na vitu vitamu ambavyo unaambiwa havina sukari, mfano
soda za dayati, hizi zina kemikali ambazo ni sumu kwenye mwili wako kama
ilivyo sukari. Tofauti yake na soda nyingine ni kwamba hazipandishi
sukari kwenye damu, lakini bado ni sumu.
Najua
hili litakuwa limekustua sana, kwa sababu vyakula vingi hapo ndiyo
unatumia kila siku. Lakini kutumia kila siku au kuzoea haifanyi kuwa
sahihi. Tafiti za kisayansi na za lishe zinaonesha wazi kwamba mazoea
yetu kwenye ulaji ndiyo kikwazo kwetu kuwa na afya bora. Hivyo tunapaswa
kujifunza na kuchukua hatua sahihi ili tuwe na afya bora na maisha bora
pia.