BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Wednesday, May 8, 2019
Tuesday, May 7, 2019
Sunday, May 5, 2019
CHANGAMOTO TANO ZINAZOKABILI KILA AINA YA BIASHARA.
Zipo
changamoto kubwa tano ambazo zinakabili kila aina ya biashara,
changamoto hizi tano ndiyo zinapelekea biashara nyingi kufa na hata
zinazopona kushindwa kukua zaidi.
(1). KUKOSA UDHIBITI .
Huna udhibiti wa kutosha kwenye muda wako, soko na hata biashara yako.
Badala ya kuiendesha biashara, biashara inakuendesha wewe.
(2). WATU.
Unavurugwa na wafanyakazi, wateja, wabia na hata wanaokusambazia huduma
mbalimbali. Watu hao hawaonekani kukuelewa na wala hawazingatii yale
unayowataka wazingatie.
(3). FAIDA. Faida unayopata haitoshi kuendesha biashara.
(4). UKOMO. Ukuaji
wa biashara yako umefika ukomo, kila ukikazana kuweka juhudi zaidi
hakuna ukuaji unaopatikana, unajikuta unachoka zaidi lakini hakuna cha
tofauti unachopata.
( 5 ). HAKUNA KINACHOFANYA KAZI. Umeshajaribu
mbinu mbalimbali za kuiwezesha biashara yako kukua na watu kukuelewa,
lakini hakuna hata moja ambayo imeleta matokeo mazuri. Unaelekea kukata tamaa na kuona labda biashara siyo bahati yako.
Changamoto
hizi tano zinaikabili kila aina ya biashara, lakini habari njema ni
kwamba, changamoto hizi siyo mwisho wa biashara, unaweza kuzivuka na
kuiwezesha biashara yako kukua zaidi kama utazingatia nguzo sita muhimu
za ukuaji wa biashara yako.
FANYA KAZI NJE YA BIASHARA YAKO.
Kama unataka kufurahia biashara yako, basi unapaswa kufanya kazi nje ya biashara na siyo ndani ya biashara. Kufanya
kazi ndani ya biashara ni pale ambapo unakuwa bize na shughuli za kila
siku za biashara hiyo, kuuza, kuwahudumia wateja na kuzalisha au kuandaa
bidhaa na huduma unazouza. Japokuwa
unaweza kuona hilo ni muhimu na hata kupenda sana kulifanya, linakuzuia
kuikuza zaidi biashara yako, maana unapofanya kazi ndani ya biashara,
unachoka sana na hupati nafasi ya kuona mbali zaidi ya kile unachofanyia
kazi kwenye biashara hiyo.
Kufanya
kazi nje ya biashara yako ni pale ambapo unaiangalia biashara yako kama
mtu baki, kuangalia kila kitu kinavyofanyika na kuona uimara na udhaifu
wako. Ni sawa na kupanda juu angani kisha kuangalia biashara yako kwa chini, na kutathmini kila kinapofanyika. Unapofanya
kazi nje ya biashara, hufikirii yale majukumu ya kila siku ya biashara,
bali unaangalia kule ambako biashara inakwenda na uwezo wa kufika huko.
Kama
unataka biashara yako ikue, lazima uweze kufanya kazi nje ya biashara
yako, uweze kuiangalia biashara kama mtu wa pembeni na kupata picha ya
pale ilipo sasa na inapoweza kufika.
WEWE NA BIASHARA YAKO NI VITU VIWILI TOFAUTI
Hiki ni kitu ambacho kila mfanyabiashara anapaswa kuambiwa, tena kupigiwa kelele kila mara mpaka aelewe. Kwa sababu kama wafanyabiashara wakielewa hili, nusu ya matatizo ya biashara yatatoweka yenyewe.
Sehemu kubwa ya matatizo ya biashara yanasababishwa na mfanyabiashara kufikiri yeye ni biashara yake, kitu ambacho siyo kabisa.
Biashara nyingi hazikui kwa sababu hakuna mpaka baina ya biashara na mmiliki wa biashara.
Mtu anaweza kutoa fedha kiholela kwenye biashara kwa sababu anaona
biashara ni yake. Kitu ambacho kinakuwa na athari kubwa sana kwenye
ukuaji wa biashara hiyo.
Ndugu ,
naomba nikusisitizie hili, na liandike mahali ambapo utaweza kulisoma
kila siku; WEWE SIYO BIASHARA YAKO, wewe na biashara yako ni vitu viwili
tofauti kabisa.
Wewe una maisha yako, ndoto zako na mahusiano yako, biashara ina maisha yake, ndoto zake na mahusiano yake. Kinachowaunganisha
wewe na biashara yako ni mtaji ambao umeuweka kwenye biashara hiyo,
mtaji huo umeikopesha biashara, na njia pekee ya kunufaika kupitia
biashara hiyo ni pale inaopata faida baada ya kufanyika kwa biashara.
Ukiweza
kuelewa hili, kwamba wewe siyo biashara yako, ukaiheshimu biashara yako
na kuiacha ikue bila ya kuiingilia, ukaiendesha kwa misingi ya ukuaji
wa biashara, utaiwezesha biashara hiyo kukua zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)