BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Saturday, May 4, 2019
KILA BIASHARA INA CHANGAMOTO ZAKE . USIPUUZE AU KUKWEPA IKABILI KILA CHANGAMOTO INAPOJITOKEZA.
Ni changamoto zipi unazokutana nazo na unazoweza kukutana nazo mbeleni?
Kila
biashara ina changamoto zake, hakuna biashara isiyokuwa na changamoto
kabisa. Lakini watu wengi huwa hawapendi kukutana na changamoto, na
hivyo huwa hawapo tayari kuzikabili.
Wanachofanya
wafanyabiashara wengi pale wanapokutana na changamoto ni kuzipuuza au
kuziacha wakiamini zitaondoka zenyewe. Changamoto hizo huwa haziondoki,
badala yake zinakua na kuota mizizi, na hizo ndiyo huja kuua biashara.
Unapaswa
kujua zipi changamoto kubwa zinazoikabili biashara yako sasa na hata
siku za mbeleni. Kisha kuwa na mkakati sahihi wa kukabiliana na kila
changamoto pale inapojitokeza. Usijaribu kupuuza au kukwepa changamoto,
badala yake ikabili kila changamoto inapojitokeza, na siyo tu utaitatua,
bali pia utapiga hatua zaidi kwenye biashara yako.
KUWA NA MKAKATI WA MASOKO YA BIASHARA YAKO.
Upi mkakati wa masoko unaofanyia kazi wa biashara yako ?
Biashara
ni wateja, bila ya wateja, haijalishi una bidhaa au huduma bora kiasi
gani, huna biashara. Na njia pekee ya kuwaleta wateja kwenye biashara
hiyo ni mkakati wa masoko.
Wafanyabiashara
wengi wadogo huwa hawajisumbui kabisa na masoko. Huwa wanaendesha
biashara zao kwa mtazamo wa kizamani kwamba ukijenga biashara wateja
watakuja wenyewe. Lakini zama hizi ambazo wafanyabiashara ni wengi,
hakuna mteja atakayekuja kwako, bali unapaswa kuwatafuta wateja.
Unawatafuta wateja kupitia mpango mkakati wa masoko unaokuwa nao kwenye biashara yako.
Hii
ni kusema kwamba ili biashara yako ifanikiwe, lazima iwe na mkakati wa
masoko, ambao unawatambua wateja wa biashara hiyo, kuwafikia kule waliko
na kuwashawishi kununua.
Mkakati wako wa masoko unapaswa kuzingatia vitu vinne muhimu sana;
- Kuwatabua wateja sahihi wa biashara yako, wale ambao wanaweza kunufaika na bidhaa au huduma unazotoa.
- Kutambua vitu vitatu vinavyokutofautisha wewe na wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara kama yako. Kama huna utofauti wowote na wafanyabiashara wengine, hakuna sababu ya mteja kuja kwako.
- Mchakato sahihi wa ufanyaji wako wa biashara, jinsi mteja anavyohudumiwa na hatua zote zinazochukuliwa kwenye biashara yako.
- Uhakika unaowapa wateja wako. Wateja wamepata fedha zao kwa shida, hawataki kuzipoteza, hivyo wanahofia sana kufanya manunuzi mapya. Unapaswa kuwapa uhakika kwamba wakinunua kwako hawapotezi fedha bali wanapata thamani.
Tengeneza
mkakati wako wa masoko ambao unajumuisha vitu hivyo vinne na utaweza
kuwafikia wateja wengi na kuwashawishi kununua kwako.
WEKA MALENGO YA MUDA MREFU ( MIAKA MITANO , KUMI ........... !! ) YA BIASHARA YAKO.
Ni lengo lipi kubwa unataka kufikia ndani ya miaka MITANO , KUMI ? YA BIASHARA YAKO ?
Kabla sijaendelea hapa, hebu tafakari hilo swali na jipe majibu sahihi. Ni
lengo lipi kubwa unalofanyia kazi ambalo unataka kulifikia miaka MITANO , KUMI ijayo? Watu wengi wanaweza kushangaa unapangaje miaka kumi ijayo, wengi
kupanga mwaka mmoja tu ni shida.
Huwezi
kufanikiwa kwenye biashara kama huna malengo ya muda mrefu. Na hata
kinachofanya wafanyabiashara wengi kukimbizana na fursa mpya
zinazojitokeza ni kwa sababu hawana malengo yoyote ya muda mrefu, hivyo
chochote kinachojitokeza wanaona ni sahihi kwao kukimbizana nacho.
Unapaswa
kuwa na lengo kuu la miaka MITANO , KUMI ijayo ya biashara yako, wapi unataka
kufika na kwa kiwango gani. Lengo hili ndiyo litakusukuma kila siku,
ndiyo litakuwa mwongozo wako na ndiyo litaathiri kila maamuzi
unayofanya.
Kama huna lengo la miaka MITANO , KUMI ijayo ya biashara yako, hujajitoa kufanikiwa kweli kwenye biashara hiyo. UNATANIA NDUGU ! BADILIKA ! NA AMKA !
WEKA KIPAUMBELE KIKUU CHA BIASHARA YAKO .
JIULIZE Kipi kipaumbele kikuu cha biashara Yangu ?
Hakuna
kitu kinachowapoteza wafanyabiashara wengi kama fursa mpya na nzuri
zinazojitokeza kila wakati. Iwapo mfanyabiashara atakuwa mtu wa
kukimbizana na kila fursa inayojitokeza, hawezi kufanikiwa kabisa kwenye
biashara.
Hii
ni kwa sababu fursa mpya huwa ni nyingi na haziishi, na ili upate
mafanikio kwenye jambo lolote, unahitaji kuweka muda na kazi.
Jukumu
lako kama mfanyabiashara ni kuweka kipaumbele kikuu cha biashara yako,
yaani ni aina gani ya biashara utafanya na kisha kuachana na kelele
nyingine zozote.
Ukishachagua
biashara utakayofanya, funga masikio kuhusu biashara nyingine
zisizoendana na biashara hiyo. Hata uambiwe kuna biashara mpya na yenye
faida kubwa, usidanganyike kuondoka wenye vipaumbele vyako na kwenda
kwenye biashara hiyo mpya, utajipoteza mwenyewe.
Ukichagua
nini unataka na kuweka nguvu zako zote kwenye kitu hicho, lazima
utakifikia. Lakini ukigawa nguvu zako kwenye kila kitu kipya
kinachojitokeza, unajizuia mwenyewe kufanikiwa.
Kama
biashara uliyoanzisha imekuwa na unaona fursa ya kuingia kwenye
biashara nyingine, fanya hivyo kwa mipango na maono yako na siyo kwa
kusukumwa na tamaa zako na za wengine.
JENGA MISINGI MIKUU YA BIASHARA YAKO.
JIULIZE SWALI HILI WEWE MFANYABIAHARA . Ipi ni misingi mikuu ambayo inaendesha biashara yako?
Kama unataka kujenga nyumba basi msingi ni sehemu ya
kuweka umakini mkubwa. Kadhalika kwenye biashara, unapaswa kujenga
msingi imara kama unataka biashara yako ifanikiwe.
Hatua
ya kwanza kwenye maono ya biashara ni kuainisha misingi mikuu ambayo
inaendesha biashara hiyo. Hizi ni kanuni na maadili ambayo kila
anayekuwa kwenye biashara hiyo anapaswa kufuata, ukianza na wewe mmiliki
wa biashara.
Misingi
hii ni muhimu kwa sababu inaongoza jinsi maamuzi yanavyofanywa kwenye
biashara. Pia inawavutia watu sahihi na kuwaondoa wale wasio sahihi.
Unapaswa
kuwa na misingi imara ya maadili ya kuendesha biashara yako, ambapo
maamuzi yote yataongozwa kwa misingi hiyo. Pia utaajiri, kutunza na hata
kufukuza wafanyakazi kwa kutumia misingi hiyo.
Friday, May 3, 2019
Subscribe to:
Posts (Atom)