Tuesday, January 29, 2019

KILA MJASIRIAMALI ANAPENDA KUFANIKIWA SANA !! LAKINI --------------------!!

Kila mtu anatamani biashara anayoifanya ifanikiwe, kila mtu anatamani akiingia kwenye ujasiriamali mambo yake yanyooke sana na yawe ya mafanikio makubwa. Hiki ndicho kitu ambacho watu wengi sana wanapenda kiwe kwenye maisha yao.
Hata hivyo uelewe hivi, unapochagua kuingia kwenye biashara, ujue kabisa umechagua kabisa kuingia kwenye ulimwengu wa wapambanaji haswa, yaani ulimwengu wa ujasiriamali. Hivyo, unapoingia kwenye dunia ya ujasiriamali kuna mambo lazima uyajue kwanza.
Pasipo kuyajua mambo hayo, nakuhahakikishia kabisa, utakwama sana na itafika mahali utajiona wewe si kitu na si lolote.

Saturday, January 26, 2019

VITABU VIZURI VYA KUSOMA.

---The Monk who sold his Ferrari – Robin Sharma. Katika kitabu hiki, Sharma ananifundisha kuwa mafanikio ya nje hayana maana ikiwa mafanikio ya ndani (i.e. mwili, roho, na nafsi) hayajakaa sawa. Pia siri ya furaha si ngumu. Ni kutafuta kile unachokipenda kukifanya, kisha elekeza nguvu na maisha yako yote katika kukifanya hicho tu. Ukijijua, umeyajua maisha.

-----How to live on 24 hours a day - Arnold Bennett. Jamaa huyu ananifundisha kuwa, muda wa ziada kufanikisha mipango ya mafanikio unaweza kupatikana: mwanzoni mwa siku, kwa kuamka mapema, njiani kuelekea kazini, njiani kurudi nyumbani baada ya kazi, masaa ya jioni, mwisho wa wiki.

----Who Moved My Cheese? - Spencer Johnson. Kitabu kinaeleza kwa njia ya simulizi njia ya ajabu ya kushughulika na mabadiliko katika kazi na katika maisha. Kwa hiyo, mkao sahihi kwenye maisha ni kukubali kwamba mabadiliko yapo, yatarajie, fuatilia mabadiliko, endana na mabadiliko, badilika na yafurahia mabadiliko.

-----The Law of Success – Napoleon Hill. Ni hizi sarafu ndogondogo tunazozidharau na kuzipuuza zingeweza kutuletea uhuru wa kifedha kama tungedumu katika tungeziweka akiba na kuwekeza. “The nickels, dimes and pennies which the average person allows to slip through his fingers would, if systematically saved and properly put to work, eventually bring financial independence.”

---- How to achieve total success in life – Dr. C.S. Chopra. Kwa habari ya mafanikio, Chopra naye anakazia umuhimu wa kuanza na picha ya mwisho unakotaka kufika kisha kujenga mfumo wa kufika huko.

VITABU VIZURI VYA KUSOMA.

  1. )The Law of Success – Napoleon Hill. Nimejifunza na nafanyia kazi suala la kuweka lengo kuu la maisha (definite chief aim).
  2. You’re born an original, don’t die a copy – John Mason. Kubwa ninalofanyia kazi kutoka kitabu hiki ni namna ya kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi wakati wote. Mason anasema hatma ya mwanadamu imo katika maamuzi anayoyafanya
  3. Goals – Brian Tracy. Ananifundisha kuwa, malengo lazima uyaandike kila siku bila kuacha hata siku moja. Pia kuwa na dira (vision) ya maisha yangu. Yaani ule kutazama miaka mingi mbele kwa yale unayotaka yatokee na kufanya vitu fulani sasa vinavyokupeleka kwenye ile picha kubwa ya maisha unayoyajenga.
  4. Timiza Malengo Yako – Joel Arthur Nanauka. Nanauka ananifundisha kuwa, kwenye uwekaji malengo, pamoja na kuhakikisha kwamba yako SMART na yameandikwa, lakini lazima lengo kubwa kiasi cha kwamba ukiwaamba watu wakucheke, wahisi umechanganyikiwa. Kama hujachekwa na kushangawa, lengo bado halijawa kubwa ipasavyo. Pia lengo lazima liwekewe mpango wa utekezaji
  5. The magic of thinking $uccess – Dr. David J. Schwartz. Kitabu hiki kinanifundisha kuwa, mafanikio katika jambo lolote yanaanza kwanza kwa kujua kwa hakika kwamba ni nini unahitaji kwenye jambo hilo. Kama hujui unakokwenda, huwezi kufika wala huwezi kupotea. Safari pia haitakuwa na maana. Ndiyo maana lazima kwanza ujue unachohitaji, kisha mengine yafuate.
  6. A setback is a setup for a comeback – Willie Jolley. Katika kitabu hiki, nilijifunza kuwa, fursa yoyote ile imefungashwa kwenye changamoto. Hakuna fursa ya waziwazi, zote zinafikiwa kwa kuingilia mlango unaotwa changamoto.
  7. The impossible is possible – John Mason. Mason katika kitabu hiki ananifundisha kujipambanua. Yale wengine wanayosema hayawezekani, mimi nayafanya. Ni marufuku kufuata mkumbo. Tai huruka peke yao, lakini kunguru huruka katika makundi.
  8. The Power of your subconscious mind – Dr. Joseph Murphy. Nilijifunza kuwa, subconscious mind (akili isiyofikika) ni kama shamba. Usipopanda mazao ya kuliwa, yataota magugu au mimea mwitu. Subconscious mind haiwezi kukaa bure. Kwa hiyo kila mwanadamu (kwa kujua ama kutokujua; kwa kukusudia au kutokukusudia) anapanda mbegu (mawazo) kwenye subconscious mind yake kila siku kwa kadri ya mwelekeo wa tabia zake kimawazo. Hivyo apandacho mtu (kwenye subconscious mind yake), ndicho avunacho kwenye matokeo ya nje. Ili subconscious mind ituhudumie kwa usahihi, lazima tuilishe kwa usahihi pia. Mbegu zetu sasa (mawazo) na ziwe amani, furaha, matendo ya haki, nia njema na mafanikio.
  9. As a man thinketh – James Allen. Namheshimu sana Allen. Kwa ufupi kabisa, nimejifunza kuwa Hali ya nje ya mtu kimazingira, ni dhihiriko la hali yake ya ndani kimawazo. nakazana kuwaza kwa usahihi na najifunza kila siku ili kuboresha hali yangu ya ndani kwanza ili nichochee ubora wa hali yangu ya nje kimazingira.
  10. The science of getting rich – Wallace D. Wattles. Huu ni msaafu wangu wa kuongoza maisha. Ujumbe nilionao kutoka kwenye kitabu hiki ni kuwa, utajiri unapatikana kwa sayansi kamili kama zilivyo sayansi zingine – siyo ajali, bahati wala uchawi wowote. Kikubwa ni kuwaza kwa namna Fulani na kuweka mawazo hayo kwenye vitendo. Dunia haijawahi kupungukiwa na chochote. Hivyo yatupasa tuwaze katika utele, siyo katika uhaba. Fursa za mafanikio hazina kikomo, hakuna mtu mmoja (na pengine hatatokea) wa kumzuia mwingine kufanikiwa.
  11. The secret code of success – Noah ST. John. Kinachowanyima watu mafanikio ni kushindwa kutekeleza (ACTION) matumaini yao halisi, ndoto, na matarajio. Linapokuja suala la mafanikio, akili ya kufikika (conscious mind) si mahali sahihi kuanzia. Sehemu muafaka ya kuanzia ni kwenye subconscious mind maana 90% ya tabia zetu zinatoka huku.
  12. Secrets of the Millionaire Mind – T. Harv Eker. Mafanikio katika jambo lolote yanahitaji kubadili hali ya ndani kwanza kimtazamo ili kubadili matokeo kwa nje kimazingira. Waliofanikiwa kifedha wana picha ya tofauti sana ndani mwao kuhusu fedha ukilinganisha na picha walizo nazo watu maskini na wenye kipato cha kati.
  13. Acres of Diamonds - Russell H. Conwell. Najifunza kupitia simulizi ya jamaa aliyeamua kuuza shamba lake na kusafiri nchi za mbali kwenda kutafuta almasi – bahati mbaya hakuzipata na alifia huko. Huku nyuma, jamaa aliyenunua shamba lake, aligundua lile shamba lilikua limejaa almasi na alichimba akapata nyingi sana. Kwa hiyo, mtu ukiwa na ndoto ya mafanikio, nirahisi kuangalia nje kwa kuamini huko ndiko ndoto yako itatimia, lakini ukweli ni kwamba lazima tuanzie pale tulipo, akilini mwetu, mazingira yetu, na vile tulivyonavyo.
  14. Tatizo si raslimali zilizopotea – Godius Rweyongeza. Huyu Mtanzania kijana ananifundisha kuwa thamani ya mtu inapimwa kwa kile anachotoa si kile unachopokea. Kila mwanadamu angejijua mipaka ya uwezo wake, hakika tusingekuwa hapa leo.
  15. I can, I must, I will – Reginald Abraham Mengi. Kutoka kwa mzee Mengi, napigana Kukataa Hofu ya kushindwa. Hii ni moja ya vitu vikuu vya awali kabisa vinayotufanya watanzania wengi kushindwa kuingia kwenye Biashara. Mengi anasema, tunakosa the “I can” attitude.
  16. Why “A” students work for “C” students and “B” students work for the government – Robert T. Kiyosaki. Nimejifunza kuwa, tunakoelekea watakaoimudu dunia ni wale watakaokuwa na taarifa sahihi, na kuwa tayari kubadirika kadri dunia inavyobadirika na siyo kukinzana na mabadiriko.
  17. Before you quit your job – Robert T. Kiyosaki. Kiyosaki katika kitabu hiki ananifundisha mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza safari ya ujasiriamali. Kuna habari ya dhamira, uongozi na timu ya watu. Hizi nguzo tatu, zinabeba ndani mambo matano: mtiririko wa fedha, mawasiliano, mifumo, masuala ya kisheria, na bidhaa. Mtu anapaswa kuwa tayari kwa changamoto zote zijazo. Japo anasema ujasiriamali siyo wa kila mtu, lakini anasisitiza kuwa mtu yeyote anaweza kuwa mjasiriamali.
  18. Increase your financial IQ – Robert T. Kiyosaki. Akili ya fedha si tu kuzalisha fedha zaidi, lakini pia kuzilinda zisipotee, kuzibajeti, kuifanya fedha izae kwa kuwekeza n.k., na kuhakikisha una taarifa sahihi za fedha wakati wote.
  19. Kuna uhusiano kati ya fedha yako na hali yako ya kiroho – Christopher Mwakasege. Fedha ina nguvu kuliko roho kwa mujibu wa maandiko ya biblia kwenye Matayo 6: 21 yanayosema, “Maana pale ilipo hazina yako ndipo utakapokuwa moyo wako”. Mwakasege ananifundisha kuwa, haiwezekani kuapata uhuru wa kiroho vizuri pasipo kwanza kuwa na uhuru wa kifedha. Kwa hiyo, fedha/utajiri ni muhimu sana ili kustawi kiroho.
  20. How to Raise your Own Salary – Napoleon Hill. Hapa najifunza kuwa, watu wenye mafanikio daima wanafanya kazi wanayopenda kufanya. Masaa si kitu kwao. Wanaona furaha katika kufanya kazi yao. Umaskini ni tabia. Mtu yeyote akikubali hali ya umaskini, hali hii ya akili inakuwa tabia. Mtu anakubali umasikini kwa kutokuweka mpango wa kupata utajiri.

KANUNI MUHIMU YA MAFANIKIO KWENYE BIASHARA.

Nakushirikisha kanuni muhimu sana ya mafanikio kwenye biashara, ambayo ukiifuata kwenye biashara yako, utapiga hatua sana.
Kanuni hiyo inasema; eneo sahihi, muda sahihi, suluhisho sahihi, mawasiliano sahihi, hatua sahihi, malipo sahihi, rudia.

  1. )ENEO  SAHIHI.
Kuna biashara nyingi ambazo zinaanzishwa maeneo ambayo siyo sahihi, unakuta biashara ni nzuri, lakini kwa ilipo haina wateja. Unapawa kuanzisha biashara kwenye eneo sahihi, eneo ambalo wateja wapo ili uweze kuendesha biashara.

  1. )MUDA  SAHIHI.
Kuna biashara ambazo zinaanzishwa kwenye eneo sahihi, lakini kipindi ambacho zinakuwa zimeanzishwa siyo sahihi. Labda watu wanakuwa hawajaielewa biashara hiyo, au siyo msimu wa watu hao kutumia kitu kinachouzwa. Unapaswa kuanzisha biashara kwa wakati sahihi.

  1. )SULUHISHO  SAHIHI.
Unaweza kuanza biashara eneo sahihi na lenye wateja wenye uhitaji, lakini usiuze kama kile unachouza hakiwasaidii wateja kutatua tatizo walilonalo. Biashara yako inapaswa kutatua tatizo sahihi la mteja.

  1. MAWASILIANO  SAHIHI.
Unaweza kuwa na biashara uliyoanzisha eneo sahihi, ukawa na suluhisho sahihi kwa wateja wako na bado usiuze, kama hautakuwa na njia sahihi ya kuwasiliana na wateja wako. Ili watu wajue na kununua unachouza, lazima uwasiliane nao, lazima uwe na mpango wa masoko ambao unawafikia wateja wa biashara yako na wanajua kuhusu uwepo wako na wananufaikaje na kile unachouza.

  1. )HATUA   SAHIHI.
Hatua unazochukua kwenye biashara yako ni muhimu sana. Ili biashara ikue na kuleta faida, lazima uchukue hatua kubwa, kuwafikia wengi na kuwapa huduma bora kabisa. Kama unafanya biashara kwa ukawaida, huendi hatua ya ziada, usitegemee matokeo makubwa kutoka kwenye biashara hiyo. Kwenye biashara na kwenye maisha kwa ujumla, unapata kile unachotoa.

  1. ).MALIPO  SAHIHI.
Unaweza kuwa na biashara sahihi, eneo sahihi, suluhisho sahihi na wateja wananunua sana. Lakini malipo yasipokuwa sahihi, hutaweza kupiga hatua. Kama unauza bei rahisi ili wengi wanunue, na unapata faida ndogo, hutaweza kutoa huduma bora na hata kupiga hatua kutakuwa kugumu. Lazima uipangilie biashara yako kwa namna ambayo malipo unayopata yanakuwezesha kuendesha maisha yako na hata kutoa huduma bora zaidi kupitia biashara hiyo.

  1. ).RUDIA.
Ukishaanzisha biashara inayokidhi vigezo vyote hivyo sita, hapo sasa unayo biashara, unayo mashine ya kuchapa fedha. Sasa ukishakuwa na mashine ya kuchapa fedha unahitaji nini tena? Ni kurudia huo mchakato kila wakati. Kila siku boresha biashara yako kwenye maeneo hayo, na pia angalia fursa nyingine ambapo unaweza kutumia kanuni hiyo kuanzisha na kukuza biashara mpya.

Thursday, January 17, 2019

EPUKA MABISHANO KWA KUFANYA HIVI.

Hakuna kitu kinachochukua muda wako na nguvu zako kama mabishano.

Mabishano ya aina yoyote ile ni gharama kwako na hakuna chochote unachonufaika nacho.

Na ipo njia rahisi sana ya kukuwezesha kuepuka kila aina ya mabishano.
 
Njia hiyo ni kukubaliana na watu waliojiandaa kubishana. Waambie wapo sahihi na kile wanachoamini na kusimamia ndiyo kweli. Hapo hawatakuwa tena na cha kubishana na wewe na kila mtu ataendelea na yake.
 
Lakini kama unataka ubishani uibuke, ambao hautaisha, mwambie mtu hayupo sahihi, mwambie amekosea na hapo utaibua ubishani usio na kikomo. Tena pale unapogusa kile ambacho mtu anaamini kweli, atatafuta kila njia ya kukitatua.
 
Kubaliana na watu haraka na endelea na mambo yako ambayo ni muhimu zaidi kuliko mabishano ambayo hayana manufaa yoyote kwako.
 
Kubaliana na watu na hawatakuwa na sababu ya kubishana na wewe. Na unapokubaliana nao haimaanishi kwamba wapo sahihi, ila hutaki kusumbuana nao. Ndani yako unaweza kujua kabisa kwamba hawapo sahihi, lakini huwaambii hilo maana ubishi utakaoanza hautakuwa na kikomo.

SHERIA YA ASILI: ( LAW OF NATURE )--UTAVUNA ULICHOPANDA.

Asili ina tabia ya kutoa hukumu yake hapo hapo, inatoa majibu mara moja.
Unapotenda dhambi, au kufanya kile ambacho wewe mwenyewe unajua siyo sahihi, utaanza kujisikia vibaya wewe mwenyewe. Na chochote utakachopata, hutaweza kukifurahia kama kitu ulichopata kwa uhalali.
Na zaidi ya hayo, asili lazima itakufanya ulipe kila unachofanya. Kanuni ya asili ni kulipa kila kinachofanywa, kwa kiwango kile kile.
Ukifanya wema, wema unarudi kwako kwa kiwango kile kile. Ukifanya uovu, uovu unarudi kwako kwa kiwango kile kile. Huwezi kutoroka hili, huwezi kuizidi asili akili.
Chagua kuishi kwa misingi sahihi, chagua kufanya kilicho sahihi mara zote, siyo kwa sababu unaogopa moto baadaye, bali kwa sababu unajua kila kitu kitalipwa sasa bila ya kuchelewa.

Monday, January 14, 2019

UFUNGUO MKUU WA MAFANIKIO.

  1. Huhitaji kutafuta nguvu nje yako, nguvu tayari zipo ndani yako. Unachohitaji ni kujua nguvu ulizonazo na kuweza kuzitumia. Kila binadamu ana nguvu kubwa ya kiroho ndani yake, na nguvu hii ya kiroho ipo ndani ya fikra zake. Kama akiweza kuzitumia vizuri fikra zake, zitampa chochote anachotaka.
  2. Magumu tunayokutana nayo kwenye maisha ni kwa sababu ya kutokujua nini hasa tunachotaka na pia kutokujua kile kilichopo ndani yetu. Ukishajua kilichopo ndani yako na ukajua kwa hakika nini unataka, na ukapeleka fikra zako kwenye hayo, hakuna kitakachokushinda.
  3. Usilalamikie chochote kinachotokea kwenye maisha yako, kwa sababu umekisababisha mwenyewe na nguvu ya kukibadili ipo ndani ya fikra zako. Fikra zako ndiyo kisababishi, na yale yanayotokea kwenye maisha yako ni matokeo. Hivyo kama hujayapenda matokeo, badili kisababishi ambacho ni fikra zako.
  4. Dunia inaendeshwa kwa upacha, kwenye dini kuna Mungu na shetani, kwenye sayansi tuna chanya na hasi, kwenye falsafa tuna wema na uovu. Lakini yote haya ni hali ya fikra zetu. Kama fikra zikisimamiwa vizuri zinaleta matokeo mazuri, kama zisiposimamiwa zinaleta matokeo mabaya.
  5. Tunaishi kwenye zama za fikra, zama za ubunifu. Wanaofanikiwa ni wale ambao wanaweza kutumia fikra zao vizuri. Kwa sababu dunia imekuwa na vitu vile vile miaka yote, bali wale waliotumia fikra zao vizuri ndiyo wamenufaika zaidi na dunia. Kwa mfano umeme tulionao sasa duniani hauna tofauti na umeme uliokuwepo miaka 200 iliyopita. Lakini leo tuna vitu vingi zaidi vinavyotumia umeme kuliko miaka 200 iliyopita kwa sababu watu wametumia vizuri fikra zao na kuja na vitu vipya.
  6. Zipo njia kuu mbili za kuendeleza na kutumia vizuri fikra zetu. Njia hizo ni umakini na msisitizo. Unaposisitiza fikra zako kwenye kitu kimoja, na umakini wako wote ukawa pale, fikra zina nguvu ya kukupa kile unachotaka. Ukikosa sifa hizo mbili, fikra zako zitakuwa zinahamahama na hutapata unachotaka.
  7. Baada ya kuweka umakini na msisitizo wa fikra zako kwenye kile unachotaka, unapaswa kuwa na taswira ya unachotaka na kuiweka taswira hiyo kwenye fikra zako. Pata picha ya kile unachotaka, kama vile tayari umeshakipata, jione ukiwa ndani ya kitu hicho. Kwa kutengeneza taswira hii, akili yako ya ndani itaona ndiyo maisha yako na kutengeneza maisha ya aina hiyo zaidi.
  8. Kusudi kuu la maisha ni kukua na kuongezeka. Na dunia nzima kwa asili inakua na kuongezeka. Angalia kila kiumbe, kuanzia miti, wanyama na hata samaki, wanaendelea kuzaliana na kukua zaidi. Hivyo ili kufanikiwa kwenye maisha, unapaswa kuwa na fikra za ukuaji.
  9. Tabia uliyonayo siyo kwa bahati mbaya, bali umeijenga wewe mwenyewe kwa juhudi kubwa sana. Umekazana wewe mwenyewe kujenga tabia zote ulizonazo, kwa kuanzia kwenye fikra zako, kwa namna unavyojitambulisha ndani yako. Hivyo ili kubadili tabia, anza kubadili fikra zako na weka juhudi kujenga tabia mpya.
  10. Hakuna uhaba kwenye dunia, bali kuna utele. Dunia ina kila kitu kwa wingi kadiri watu wanavyohitaji. Na hata vikipungua basi itatengeneza zaidi kadiri watu wanavyohitaji. Hivyo hupaswi kufikiri kwenye uhaba bali kwenye wingi, hupaswi kuona mwingine akifanikiwa basi wewe unashindwa. Dunia ina rasilimali za kumtosha kila mtu kufanikiwa.
  11. Maisha yanaendeshwa kwa sheria na kanuni fulani, ukizijua na kuziishi utafanikiwa. Lakini usipozijua basi zitakuumiza. Kwa mfano dunia ina nguvu ya mvutano, ambayo inavuta kila kitu kwenye dunia. Kama hujui kanuni hii na ukajaribu kuruka kama ndege, utaanguka kwenye dunia na kuumia sana. Kanuni ipo pale na kama huijui inakugharimu.
  12. Unahitaji vitu vitatu ili kuweza kunufaika na nguvu ya fikra iliyopo ndani yako. Moja unahitaji kujua kwamba una nguvu ndani yako, mbili, unahitaji kuwa na uthubutu wa kujaribu kuitumia nguvu hiyo na tatu unahitaji kuwa na imani ya kutumia nguvu hiyo.
  13. Sisi binadamu siyo viumbe wa mwili ambao tuna roho, bali sisi ni viumbe a kiroho ambao tuna mwili. Roho ndiyo inayoongoza maisha yetu na ndiyo yenye nguvu ya fikra. Mtu anapofariki, kinachoondoka ni roho, mwili unabaki pale na unakuwa hauna nguvu ya kufanya chochote. Hivyo kama unataka kujiendeleza, endeleza roho yako, endeleza fikra zako na hizi zitakupa unachotaka.
  14. Ulimwengu mzima ni kitu kimoja na tunaongozwa na nguvu moja. Kila kitu kwenye ulimwengu, ukikiangalia kwa undani unagundua ni nguvu ama nishati. Jua ni nishati ya mwanga na jito, ambayo ikifika kwenye mimea inabadilika na kuwa nishati ya kikemikali, mimea ikiliwa na wanyama nishati hiyo inahamia kwa wanyama. Kila kitu kwenye dunia ni nishati, hata sisi binadamu, ukivunja miili yetu mpaka kwenye ngazi ya seli, unagundua sisi ni nishati. Hivyo ulimwengu mzima ni kitu kimoja, nishati.
  15. Kukua ni kupoteza, kupata kipya ni kupoteza cha zamani, hii ni kanuni muhimu sana kwenye mafanikio. Hakuna kiumbe anayekua na kubaki na vitu vya zamani, na huwezi kupata kitu kipya kama bado unang’ang’ana na vya zamani. Ili ukue unahitaji kupoteza kile ambacho tayari unacho sasa. Matatizo mengi ambayo watu wanayapata ni kutokana na kung’ang’ana na vitu vya zamani.
  16. Ipo kanuni kuu ya maisha kwamba kila kitu kinazaliwa, kinakua, kuzalisha na kufa. Na kanuni hii inaenda kwa mzunguko. Kwa mfano kwetu sisi binadamu, kila baada ya miaka saba, maisha yetu yanabadilika kabisa na kuwa mapya. Miaka saba ya kwanza ni ya utoto, miaka saba inayofuatia ni ya kuanza kujifunza majukumu, saba inayofuata ni ya kuanza ukuaji wa utu uzima. Miaka saba mingine ni kufikia ukuaji kamili, inayofuatia ni ya kuzalisha na kuwa na mali na familia. Miaka saba inayofuata, 35 mpaka 42 ni kipindi cha mabadiliko makubwa kimaisha. Inafuatiwa na miaka saba mingine ya kujijenga upya kwenye utu uzima.
  17. Vitabu vya dini vinatuambia kwamba binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Na hili lina maana kwamba tunazo sifa za uungu ndani yetu. Sifa hizi zipo kwenye fikra, mungu ana sifa ya kuumba na fikra zetu pia zina sifa ya kuumba. Kadhalika kwenye nguvu na ujuzi, fikra zetu zinajua mengi na zina nguvu kubwa. Tukiweza kuzitumia tunaweza kufanya makubwa sana.
  18. Usichotumia unakipoteza. Wengi hujiuliza kama fikra zetu zina nguvu sana kwa nini wengi hawazitumii. Sababu kubwa ni kwamba wengi hawajui kama wana nguvu kubwa kwenye fikra zao, na usichokijua huwezi kukitumia, na usichotumia unakipoteza. Hivyo hatua ya kwanza ya kutumia nguvu zako ni kujua zipo, na kuanza kuzitumia.
  19. Hofu ni matumizi mabaya ya nguvu ya fikra zako. Kwa kuwa na hofu unatumia fikra kutengeneza yale ambayo hutaki yatokee na kwa kuwa fikra zina nguvu, zinaleta hayo hayo unayofikiria. Hivyo unapaswa kuondokana kabisa na kila aina ya hofu, kwa kujua nguvu kubwa iliyopo ndani yako ya kukuwezesha kufanya chochote.
  20. Jukumu lako kuu kwenye maisha, na biashara pekee ambayo inalipa ni kufikiri. Wale wanaoweza kufikiri kwa kutumia akili zao ndiyo wanaokuja na vitu vipya na njia mpya za kufanya vitu na wananufaika sana. tumia nguvu yako ya fikra kufikiri na utaweza kufanya makubwa.
  21. Unapofikiri, unapaswa kufikiri mawazo makubwa sana. Ukifikiri kidogo nguvu iliyopo ndani yako inaleta matokeo madogo. Ukifikiri makubwa nguvu hiyo inaleta makubwa. Usiogope kufikiri makubwa, una nguvu ndani yako ya kupata chochote unachofikiri.
  22. Kinachotutofautisha ni kanuni ya mtetemo (law of vibration). Tumeona kwamba kila kitu duniani ni nishati, je nini kinakutofautisha wewe binadamu na mti? Ni kanuni ya mtetemo. Wewe ni binadamu kwa sababu seli zako zina mtetemo tofauti na za mti. Na hata nishati inapobadilika kutoka mfumo mmoja kwenda mwingine, kinachobadilika ni mtetemo wake. Hata baina ya watu, wale wanaofanikiwa ziadi wana mtetemo wa juu kuliko wale wanaoshindwa. Fikra zetu zinaendana na mtetemo, hivyo tunapokuwa na fikra za juu tunavutia mtetemo wa juu. Unaweza kufananisha nguvu hii ya mtetemo na kutafuta mawimbi ya redio, unasikia redio fulani pale unapofikia kwenye mawimbi yake.
  23. Kanuni kuu ya mafanikio ni HUDUMA. Tunafanikiwa kwa kadiri tunavyowahudumia wengine, tunapata kadiri ya tunavyotoa. Hivyo kama unataka zaidi, unapaswa kutoa zaidi, kama unataka kufanikiwa zaidi unapaswa kuwahudumia wengi zaidi na kwa ubora zaidi.
  24. Ili kuwa huru na ili kupata chochote unachotaka, unapawa kuujua ukweli. Kumbuka kauli inayosema IJUE KWELI NAYO ITAKUWEKA HURU. Watu wengi hawapo huru kwa sababu hawajui ukweli, na usipokuwa huru huwezi kuwa na mafanikio. Ujue ukweli kwa kujua nguvu kubwa iliyopo ndani yako na pia kwa kujua umoja wa dunia, kwamba kila kitu ni nishati na tunavuta vile vitu ambavyo vipo kwenye mtetemo wa fikra zetu.