Ndugu yangu, mdau wangu kama kuna kitu kimoja
unachopaswa kukikataa kwa mwaka 2019 basi ni kukiri umasikini. Usikiri
kwa kinywa chako kwamba wewe ni mtu masikini au mtu mnyonge, utaendelea
kubaki kwenye hali hiyo.
Hata kama huna fedha, usijiite masikini,
badala yake jiite tajiri mafunzoni. Tumia kauli chanya kuhusu fedha na
utajiri na hilo litakaribisha fedha kwako zaidi na zaidi.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE. JIFUNZE ---ELIMIKA --CHUKUA HATUA---FANIKIWA
Friday, January 4, 2019
EPUKA KAULI HII MWAKA MPYA 2019 , " KAZI YA FEDHA NI MATUMIZI / KUTANUA / PONDA MALI KUFA KWAJA " ILI UWE NA MAFANIKIO MAKUBWA KIFEDHA KWAKO.
Hivi ndivyo wengi wanavyotengeneza mahusiano yao na fedha, wakizipata watazitumia mpaka ziishe ndiyo waweze kutulia.
Hupaswi kutumia kila fedha unayoipata mpaka iishe, na kwa hakika unapaswa kuweka akiba na kuwekeza kabla hata hujaanza kutumia fedha uliyonayo.
Acha kujiambia kazi ya fedha ni matumizi, au kutumia kauli kama tumia fedha ikuzoee. Kila fedha unayopata weka fungu fulani pembeni kwa ajili ya akiba na uwekezaji kabla hujaanza kutumia.

EPUKA KAULI HII MWAKA MPYA 2019, " FEDHA NI NGUMU " ILI UWE NA MAFANIKIO MAKUBWA KIFEDHA KWAKO.
Kamwe usikiri kwamba fedha ni ngumu
kupatikana au inabidi uumie ndiyo uipate. Jua fedha ni mabadilishano ya
thamani, angalia thamani unayoweza kuitoa kwa wengine na wao watakupa
fedha.
Ukikiri fedha ni ngumu, utakata tamaa na kushindwa kutoa thamani kwa wale wenye uhitaji.
Kiri fedha ni matokeo ya thamani na kazana kuzalisha thamani zaidi ili kupata fedha zaidi.
Ukikiri fedha ni ngumu, utakata tamaa na kushindwa kutoa thamani kwa wale wenye uhitaji.
Kiri fedha ni matokeo ya thamani na kazana kuzalisha thamani zaidi ili kupata fedha zaidi.
EPUKA KAULI HII MWAKA MPYA 2019, " FEDHA SIYO KILA KITU " ILI UWE WA MAFANIKIO MAKUBWA KIFEDHA KWAKO.
Usemi huu ni maarufu sana kwa wengi,
hasa masikini, kwamba usijisumbue sana na fedha kwa sababu fedha siyo
kila kitu. Hii kauli siyo sahihi kwa asilimia 100, ni kweli kuna vitu
muhimu kwenye maisha ambavyo tunavipata bura, kama hewa tunayopumua.
Lakini ukiwa mgonjwa na huwezi kuvuta hewa mwenyewe, utauziwa hewa hiyo
kwa bei ya juu sana.
Usitumie kauli hii ya fedha siyo kila kitu, kiri kwamba fedha ina mchango mkubwa sana kwenye maisha yako na kazana kuipata ili maisha yako yawe bora.
Vitu kama mahusiano yako na wengine unaweza kuona havihitaji fedha, lakini unapokuwa huna fedha ndiyo unagundua ni vigumu kiasi gani kuendesha mahusiano yako na wengine.

Tuesday, January 1, 2019
MAMBO 18 YA KUFANYA KILA SIKU ILI KUPATA MAFANIKO MAKUBWA SANA.
1. Amka asubuhi na mapema sana, angalau masaa mawili kabla ya muda wako wa kuanza kazi.
2. Unapoamka cha kwanza kufanya shukuru, kwa sala au tahajudi.
3.
Andika malengo yako makubwa kila siku unapoamka, malengo ya mwaka,
miaka 5, miaka 10 na hata miaka 50. Lazima uwe na malengo ya aina hii.
4. Ipangilie siku yako kabla hujaianza, weka vipaumbele vyako kwa siku husika, viwe kati ya 3 mpaka sita. Andika kabisa nini utafanya na kwa muda gani wa siku hiyo.
5.
Soma kitabu au pata maarifa yoyote chanya na ya hamasa kabla hujaianza
siku yako. soma angalau kurasa kumi za kitabu kila siku.
6. Fanya mazoezi ya viungo kabla ya kuianza siku yako, mazoezi bora kabisa ni kukimbia.
7. Epuka habari au kitu chochote hasi muda wa asubuhi. Usisikilize redio, wala kuangalia tv au kusoma magazeti.
8. Unapoingia
kwenye kazi au biashara yako, fuata vipaumbele ulivyoweka vya kufanya
kazi, na unapokamilisha jukumu weka alama ya vema kisha nenda kwenye
jukumu jingine.
9. Fanya jambo moja kwa wakati, usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja, unapoteza nguvu na umakini.
10. Unapofanya kazi, akili na mawazo yako yote yawe kwenye kile unachofanya, usiwe unafanya kazi huku unafikiria vitu vingine.
11. Kula
kwa afya, punguza sana vyakula vya wanga na sukari, kula matunda na
mbogamboga kwa wingi na kunywa maji mengi zaidi, angalau lita tatu kwa
siku nzima.
12.
Ondoka kwenye mitandao yote ya kijamii unayotumia kama haikuingizii
fedha moja kwa moja. Sheria ya kutumia mitandao ya kijamii iwe hii, iwe
inakuingizia fedha moja kwa moja. Kama hakuna fedha inayoingia kupitia
mitandao hiyo, achana nayo mara moja.
13. Acha kabisa kutumia kilevi cha aina yoyote ile, kuanzia pombe, sigara, madawa ya kulevya na hata viburudisho kama kahawa.
14. Kwenye
kila kipato unachoingiza, sehemu ya kumi ya kipato hicho usitumie kwa
namna yoyote ile, hicho ni kipato ulichojilipa na utakitumia kwa
kuwekeza kwa ajili ya baadaye.
15. Imarisha
sana mahusiano yako na watu wote wa karibu kwako, kuanzia familia yako,
ndugu, jamaa na marafiki na pia wale unaohusiana nao kwenye kazi au
biashara.
16. Imalize
siku yako kwa kutafakari yale uliyofanya, matokeo uliyopata, makosa au
changamoto ulizokutana nazo na namna unavyoweza kufanya kwa ubora zaidi
siku inayofuata.
17. Lala mapema ili uweze kuamka mapema, kama hufanyi kazi za usiku, saa nne inapaswa kukukuta kitandani ukiwa umeshalala.
18.
Tumia neno HAPANA mara nyingi uwezavyo, neno hapana ndiyo litakupa
uhuru wako. Kama kitu hakikuwezeshi kufika kule unakotaka kufika, sema
hapana bila ya kuona aibu.
Ndimi MWL JAPHET MASATU, DAR ES SALAAM , TANZANIA.
MOBILE PHONE: WhatsApp +255 716924136 / +255 755400128 / +255 688 361 539
EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Tuesday, December 25, 2018
WEKA MALENGO YAKO MWEZI DISEMBA KABLA MWAKA HAUJAANZA.
Watu wengi wanakosea kuweka malengo kwa
sababu wanayaweka kipindi ambacho siyo sahihi. Wakati wa mwaka mpya,
watu wengi huwa wanakuwa na hisia kali za upya wa mwaka na kwa kuwa kila
mtu anasema mwaka mpya mambo mapya, basi na wao wanajiunga na msafara
huo.
Wengi wanajikuta wanaweka malengo ambayo siyo yao, wanapoona wengine wameweka malengo fulani basi na wao wanaona wanapaswa kuwa na malengo ya aina hiyo. Kitu kinachowapelekea kushindwa sana kwenye maisha yao.
Wakati sahihi wa kuyaweka malengo yako kwa mwaka mpya ni kabla mwaka haujaanza. Hivyo mwezi huu wa disemba, tenga muda na ukae chini ili kuweka malengo yako kwa mwaka unaofuata. Kupitia tafakari ya mwezi ulioisha uliyofanya, kupitia vipaumbele vya mwaka ulivyojiwekea, unaweza kuweka malengo ambayo ni bora sana kwako.
Weka malengo yako ya mwaka mpya mwezi disemba na wakati wengine wanakimbizana na malengo mwanzo wa mwaka, wewe unakuwa upo kwenye utekelezaji.
HERI YA X--MASS NA MWAKA MPYA.

WEKA VIPAUMBELE ( PRIORITES ) MWEZI DISEMBA VYA MWAKA UNAOFUATA.
Kabla hujaweka malengo yoyote, anza
kwanza na vipaumbele. Watu wengi wanakosea kwenye kuweka malengo kwa
sababu hawajui na pia hawana vipaumbele kwenye maisha yao. Hilo
linawapelekea kuweka malengo ambayo hata hawajui wanayafikiaje, kwa
sababu yanakuwa hayaendani na hayajapangiliwa vizuri.
Chagua vipaumbele vichache kwa mwaka unaofuata, angalia yale maeneo ambayo ni ya muhimu zaidi kwenye maisha yako, ambayo ukiyasimamia vizuri na kuyafanyia kazi, utaweza kupata matokeo bora sana kwenye maisha yako.
Kwa kujua vipaumbele vyako, utaweza kuweka malengo ambayo ni sahihi kwako na yanafikika.

Subscribe to:
Posts (Atom)