Linapokuja swala la fedha, kila mtu ana namba na viwango vyake. Kwa
sababu tunatofautiana ndoto, kazi/biashara, kipato, mitindo ya maisha na
hata mazingira, matokeo yetu ya kifedha hayawezi kulingana.
Hivyo kujipima hatua ulizopiga kifedha kwa kuwatumia wengine ni
kujiumiza na hata kujirudisha nyuma, kwa sababu kuna namba nyingi ambazo
utakuwa huzijui kuhusu wengine. Kwa mfano unaweza kumwona mtu kwa nje
anaonekana kuwa na vitu vinavyoashiria ana fedha nyingi, lakini kumbe
vitu vyote hivyo amepata kwa mkopo ambao ataulipa maisha yake yote.
Pia unaweza kumwona mtu ukafikiri hayupo vizuri kifedha kwa mwonekano
wake wa nje, kumbe anafanya uwekezaji ambao baadaye utamwezesha kufikia
uhuru wa kifedha.
Kwa kuwa ni vigumu kupima hatua ulizopiga kifedha kwa kuwatumia watu wengine, unahitaji kujitumia wewe mwenyewe.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Friday, October 12, 2018
UTOAJI WA FEDHA KWA WENGINE BILA KUTEGEMEA KUPATA CHOCHOTE NI MUHIMU SANA.
Kiasi cha fedha unachotoa kwa wengine bila ya kutegemea kupata
chochote ni kiwango kingine muhimu sana cha kupima afya yako kifedha na
kujua hatua ulizopiga. Kwa kadiri unavyotoa zaidi ndivyo unavyoonesha
kwamba unaitumia fedha na siyo fedha inakutumia wewe.
Unahitaji kuwa na utaratibu wa kutoa fedha kuwasaidia wengine bila ya kutegemea kulipwa fedha hizo. Kwa sababu tunatoshelezwa zaidi na utoaji kuliko upokeaji.
Pia unapotoa fedha kwa wengine, unatengeneza pengo ambalo itabidi lizibwe, hivyo unakuwa umejiweka kwenye nafasi ya kuongeza kipato chako zaidi.

WEKA AKIBA ILI USIINGIE KWENYE MADENI MABAYA NA CHANGAMOTO ZA MAISHA.
Hichi ni kiwango kinachoonesha maandalizi yako uliyonayo sasa kwa upande wa fedha. Kadiri unavyokuwa na akiba kubwa kifedha, ndivyo unavyoweza kujilinda na dharura mbalimbali zinazoweza kukutokea. Akiba unayokuwa nayo ndiyo itakukinga usiingie kwenye madeni mabaya pale unapokutana na changamoto ambazo hukuzitegemea.
Kiwango sahihi cha akiba unayopaswa kuwa nayo ni ile inayoweza kutosheleza kuendesha maisha yako kwa miezi 6 mpaka mwaka mmoja hata kama utakuwa huna kipato kabisa katika kipindi hicho.
Kuza kiwango chako cha akiba na hili litakupa pumziko na kukuondolea wasiwasi kuhusu fedha kitu ambacho kitakuwezesha kufanya mambo yako kwa utulivu na ufanisi mkubwa.
EPUKA MADENI ILI KUEPUKA KUJIWEKA KWENYE WAKATI MGUMU KIFEDHA.
Kiasi cha fedha unachodaiwa na wengine kutokana na vitu ulivyonunua
bila ya kuwa na fedha ni kipimo cha maamuzi yako ya kifedha kwa siku za
nyuma. Kadiri madeni yako yanavyokuwa makubwa, ndivyo sehemu kubwa ya
kipato chako inavyoelekea kwenye kulipa madeni hayo na wewe kubaki na
kiasi kidogo ambacho hakiwezi kukutosheleza.
Unahitaji kutokuwa na deni binafsi kabisa, na madeni mazuri unayopaswa kuwa nayo ni yale yanayojilipa yenyewe. Madeni yanayojilipa yenyewe ni yale ambayo yanazalisha faida na faida hiyo unatumia kulipa deni. Haya ni madeni ambayo hayakuumizi.
Lakini madeni ambayo unalipa kwa fedha zako unazopata kwenye shughuli zako binafsi, ni utumwa ambao utakutesa kwa muda mrefu. Kama upo kwenye madeni ya aina hii kazana kuondoka na usiingie tena ili kuepuka kujiweka kwenye wakati mgumu kifedha.

WEKEZA SASA KWA AJILI YA BAADAYE , WAKATI UNA NGUVU ZA KUFANYA KAZI.
Kiwango ambacho umekiwekeza kwenye maeneo ambayo yanazalisha riba au
faida ni kipimo muhimu kwa maandalizi yako ya kifedha ya baadaye. Kama
hapo ulipo hujafanya uwekezaji wote kwa ajili ya baadaye, kama hujawa na
maandalizi ya kukuwezesha kuingiza kipato bila ya wewe kufanya kazi
moja kwa moja, huna maandalizi ya kifedha ya baadaye, na haupo eneo zuri
kifedha.
Unahitaji kufanya uwekezaji kwa ajili ya baadaye, kwa sababu utakuja wakati ambapo huna uwezo wa kufanya kazi kama unavyofanya sasa, lakini una mahitaji muhimu kwa maisha yako. Unapokuwa umewekeza na uwekezaji unazalisha, maisha yako yanakwenda vizuri.
Kiwango sahihi cha uwekezaji unachopaswa kuwa nacho ni kile ambacho kinazalisha faida au riba ambayo inakuwezesha wewe kuendesha maisha yako kwa kadiri ya mahitaji yako.

Wednesday, October 10, 2018
TATIZO NI TAFSIRI YA MATUKIO YANAYOTUTOKEA.
Watu wawili wanaweza kushindwa kwenye kitu kimoja, mmoja akachukulia
kushindwa huko kama kichocheo cha kufanya zaidi na akafanikiwa. Mwingine
anaweza kuchukulia kushindwa huko kama sababu ya kukata tamaa na
kushindwa kabisa.
Tukio ni moja, tafsiri tofauti na matokeo tofauti kabisa.
Siyo kinachotokea, bali namna unavyotafsiri kinachotokea ndiyo inaleta madhara kwako.
Kwenye Falsafa ya Ustoa pia kuna dhana inayoitwa upili wa udhibiti. Dhana hii inaeleza kwamba vitu vyote vinavyotokea kwenye maisha yako, vinagawanyika katika makundi mawili, kundi la kwanza ni vitu unavyoweza kuviathiri, hivi vipo ndani ya uwezo wako. Kundi la pili ni vitu usivyoweza kuviathiri, hivi vipo nje ya uwezo wako.
Hivyo unapokutana na chochote na ukajiambia ni kigumu au kinakushinda, huna haja ya kusumbuka, badala yake jiulize je kipo ndani ya uwezo wako au nje ya uwezo wako. Kama kipo ndani ya uwezo wako chukua hatua sahihi, kama kipo nje ya uwezo wako kikubali kama kilivyo au kipuuze. Hakuna namna bora ya kuendesha maisha yako kama hii, kwa sababu hakuna chochote kitakachotokea, ambacho kitakuvuruga kabisa.
Ndugu yangu , nikukumbushe tena ya kwamba kama unataka kuitawala dunia, kuna mtu mmoja unayepaswa kumtawala, na mtu huyo ni wewe mwenyewe. Hutaweza kujitawala wewe mwenyewe kwa mabavu au nguvu, badala yake utajitawala kwa kudhibiti mawazo yako na hisia zako.

JINSI YA KUJENGA IMANI KWA WATEJA WAKO KWENYE KILE UNACHOUZA.KUWA MUUZAJI MZURI.
Moja; penda kile unachofanya, usifanye kwa sababu ya fedha pekee, fanya kwa sababu unapenda kufanya, fanya kwa sababu unajali, fanya kwa sababu kuna mchango unaotoa kwa wengine.
Mbili; kuwa mtumiaji wa kwanza wa kile unachouza, hakikisha wewe mwenyewe unaweza kutumia, au unaweza kumshauri mtu wako wa karibu kabisa, unayempenda sana atumie. Kwa maneno mengine usiuze kitu ambacho wewe mwenyewe huwezi kutumia au huwezi kumpa mtu wako wa karibu atumie.
Tatu; toa uhakika wa unachouza na mpe mteja nafasi ya kurudisha iwapo alichonunua hakitamfaa au hakitafanya kazi kama alivyotegemea. Mfanye mteja aone hana cha kupoteza anaponunua kwako.
Nne; jua tatizo la mteja unalotatua na elezea kile unachouza kwa namna kinavyotatua tatizo hilo. Usieleze sifa za kitu pekee, bali eleza namna zinatatua tatizo la mteja wako.
Tano; usiwaseme vibaya washindani wako, usihangaike kuwashinda wengine, kama unachouza ni kizuri kweli, huna haja ya kuhangaika na wengine wanauza au kusema nini. Lakini kama huamini kwenye unachouza, itabidi uanze kuwakosoa na kuwasema vibaya wengine, ili kumfanya mteja wako aone wewe upo sahihi, lakini hata unapowasema vibaya wengine, mteja anajua kuna shida kwenye biashara yako.
Subscribe to:
Posts (Atom)