Kiasi cha fedha unachotoa kwa wengine bila ya kutegemea kupata
chochote ni kiwango kingine muhimu sana cha kupima afya yako kifedha na
kujua hatua ulizopiga. Kwa kadiri unavyotoa zaidi ndivyo unavyoonesha
kwamba unaitumia fedha na siyo fedha inakutumia wewe.
Unahitaji kuwa na utaratibu wa kutoa fedha kuwasaidia wengine bila ya
kutegemea kulipwa fedha hizo. Kwa sababu tunatoshelezwa zaidi na utoaji
kuliko upokeaji.
Pia unapotoa fedha kwa wengine, unatengeneza pengo ambalo itabidi
lizibwe, hivyo unakuwa umejiweka kwenye nafasi ya kuongeza kipato chako
zaidi.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Friday, October 12, 2018
WEKA AKIBA ILI USIINGIE KWENYE MADENI MABAYA NA CHANGAMOTO ZA MAISHA.
Hichi ni kiwango kinachoonesha maandalizi yako uliyonayo sasa kwa upande wa fedha. Kadiri unavyokuwa na akiba kubwa kifedha, ndivyo unavyoweza kujilinda na dharura mbalimbali zinazoweza kukutokea. Akiba unayokuwa nayo ndiyo itakukinga usiingie kwenye madeni mabaya pale unapokutana na changamoto ambazo hukuzitegemea.
Kiwango sahihi cha akiba unayopaswa kuwa nayo ni ile inayoweza kutosheleza kuendesha maisha yako kwa miezi 6 mpaka mwaka mmoja hata kama utakuwa huna kipato kabisa katika kipindi hicho.
Kuza kiwango chako cha akiba na hili litakupa pumziko na kukuondolea wasiwasi kuhusu fedha kitu ambacho kitakuwezesha kufanya mambo yako kwa utulivu na ufanisi mkubwa.
EPUKA MADENI ILI KUEPUKA KUJIWEKA KWENYE WAKATI MGUMU KIFEDHA.
Kiasi cha fedha unachodaiwa na wengine kutokana na vitu ulivyonunua
bila ya kuwa na fedha ni kipimo cha maamuzi yako ya kifedha kwa siku za
nyuma. Kadiri madeni yako yanavyokuwa makubwa, ndivyo sehemu kubwa ya
kipato chako inavyoelekea kwenye kulipa madeni hayo na wewe kubaki na
kiasi kidogo ambacho hakiwezi kukutosheleza.
Unahitaji kutokuwa na deni binafsi kabisa, na madeni mazuri unayopaswa kuwa nayo ni yale yanayojilipa yenyewe. Madeni yanayojilipa yenyewe ni yale ambayo yanazalisha faida na faida hiyo unatumia kulipa deni. Haya ni madeni ambayo hayakuumizi.
Lakini madeni ambayo unalipa kwa fedha zako unazopata kwenye shughuli zako binafsi, ni utumwa ambao utakutesa kwa muda mrefu. Kama upo kwenye madeni ya aina hii kazana kuondoka na usiingie tena ili kuepuka kujiweka kwenye wakati mgumu kifedha.

WEKEZA SASA KWA AJILI YA BAADAYE , WAKATI UNA NGUVU ZA KUFANYA KAZI.
Kiwango ambacho umekiwekeza kwenye maeneo ambayo yanazalisha riba au
faida ni kipimo muhimu kwa maandalizi yako ya kifedha ya baadaye. Kama
hapo ulipo hujafanya uwekezaji wote kwa ajili ya baadaye, kama hujawa na
maandalizi ya kukuwezesha kuingiza kipato bila ya wewe kufanya kazi
moja kwa moja, huna maandalizi ya kifedha ya baadaye, na haupo eneo zuri
kifedha.
Unahitaji kufanya uwekezaji kwa ajili ya baadaye, kwa sababu utakuja wakati ambapo huna uwezo wa kufanya kazi kama unavyofanya sasa, lakini una mahitaji muhimu kwa maisha yako. Unapokuwa umewekeza na uwekezaji unazalisha, maisha yako yanakwenda vizuri.
Kiwango sahihi cha uwekezaji unachopaswa kuwa nacho ni kile ambacho kinazalisha faida au riba ambayo inakuwezesha wewe kuendesha maisha yako kwa kadiri ya mahitaji yako.

Wednesday, October 10, 2018
TATIZO NI TAFSIRI YA MATUKIO YANAYOTUTOKEA.
Watu wawili wanaweza kushindwa kwenye kitu kimoja, mmoja akachukulia
kushindwa huko kama kichocheo cha kufanya zaidi na akafanikiwa. Mwingine
anaweza kuchukulia kushindwa huko kama sababu ya kukata tamaa na
kushindwa kabisa.
Tukio ni moja, tafsiri tofauti na matokeo tofauti kabisa.
Siyo kinachotokea, bali namna unavyotafsiri kinachotokea ndiyo inaleta madhara kwako.
Kwenye Falsafa ya Ustoa pia kuna dhana inayoitwa upili wa udhibiti. Dhana hii inaeleza kwamba vitu vyote vinavyotokea kwenye maisha yako, vinagawanyika katika makundi mawili, kundi la kwanza ni vitu unavyoweza kuviathiri, hivi vipo ndani ya uwezo wako. Kundi la pili ni vitu usivyoweza kuviathiri, hivi vipo nje ya uwezo wako.
Hivyo unapokutana na chochote na ukajiambia ni kigumu au kinakushinda, huna haja ya kusumbuka, badala yake jiulize je kipo ndani ya uwezo wako au nje ya uwezo wako. Kama kipo ndani ya uwezo wako chukua hatua sahihi, kama kipo nje ya uwezo wako kikubali kama kilivyo au kipuuze. Hakuna namna bora ya kuendesha maisha yako kama hii, kwa sababu hakuna chochote kitakachotokea, ambacho kitakuvuruga kabisa.
Ndugu yangu , nikukumbushe tena ya kwamba kama unataka kuitawala dunia, kuna mtu mmoja unayepaswa kumtawala, na mtu huyo ni wewe mwenyewe. Hutaweza kujitawala wewe mwenyewe kwa mabavu au nguvu, badala yake utajitawala kwa kudhibiti mawazo yako na hisia zako.

JINSI YA KUJENGA IMANI KWA WATEJA WAKO KWENYE KILE UNACHOUZA.KUWA MUUZAJI MZURI.
Moja; penda kile unachofanya, usifanye kwa sababu ya fedha pekee, fanya kwa sababu unapenda kufanya, fanya kwa sababu unajali, fanya kwa sababu kuna mchango unaotoa kwa wengine.
Mbili; kuwa mtumiaji wa kwanza wa kile unachouza, hakikisha wewe mwenyewe unaweza kutumia, au unaweza kumshauri mtu wako wa karibu kabisa, unayempenda sana atumie. Kwa maneno mengine usiuze kitu ambacho wewe mwenyewe huwezi kutumia au huwezi kumpa mtu wako wa karibu atumie.
Tatu; toa uhakika wa unachouza na mpe mteja nafasi ya kurudisha iwapo alichonunua hakitamfaa au hakitafanya kazi kama alivyotegemea. Mfanye mteja aone hana cha kupoteza anaponunua kwako.
Nne; jua tatizo la mteja unalotatua na elezea kile unachouza kwa namna kinavyotatua tatizo hilo. Usieleze sifa za kitu pekee, bali eleza namna zinatatua tatizo la mteja wako.
Tano; usiwaseme vibaya washindani wako, usihangaike kuwashinda wengine, kama unachouza ni kizuri kweli, huna haja ya kuhangaika na wengine wanauza au kusema nini. Lakini kama huamini kwenye unachouza, itabidi uanze kuwakosoa na kuwasema vibaya wengine, ili kumfanya mteja wako aone wewe upo sahihi, lakini hata unapowasema vibaya wengine, mteja anajua kuna shida kwenye biashara yako.
Monday, October 8, 2018
KWANINI UISHIE KUPATA PESA YA KULA TUU ??? UHA HAKI YA KUPATA PESA YA KUTOSHA.
“Pesa ya kula ni sumu ya maendeleo na utajiri” – Cypridion Mushongi
Kila mmoja anajitahidi kutafuta pesa popote anakojua. Habari njema ni kwamba kila anayetafuta pesa hii ya KULA anapata. Lakini..
pamoja
na kuipata, wengi wamekuwa wakilalamika kuwa ni ndogo na kwamba
inatosha kula tu! Wengi wanatamani kupata pesa nyingi zaidi ya hiyo
wanayoipata kwasasa. Kwaujumla, wengi wanashangaa ni kwanini hawapati
pesa ya kutosha kuweza kufanya mambo makubwa zaidi ya KULA na kulipa ADA
za watoto.
Sababu mojawapo ya kushindwa kupata pesa ya kutosha ni malengo mahususi
tunayojiwekea kabla ya kutafuta pesa. Watu wengi wakiamka asubuhi,
malengo yao makubwa kabisa ni kutafuta pesa ya KULA, ADA na kujenga
NYUMBA ya makazi. Wengine akijikakamua kidogo analenga kununua GARI la
kutembelea. Malengo ya watu yanabainishwa kwenye maongezi yao ya
kawaida. Pindi ukiwasikiliza watu, utasikia wakiambizana kuwa “mimi natafuta pesa ya kula basi! Wengine utawasikia wakisema “natafuta pesa kwaajili ya watoto” wengine wamekwenda mbali na kusema kuwa wanatafuta pesa, “ili watoto wao angalau waweze kwenda choo”
Ni wazi kuwa maongezi ya namna hii, yanakupa jibu la moja kwa moja kuwa
watu wengi wana malengo ya kutafuta kiasi kinachotosha KULA, kulipa
KARO na kujenga NYUMBA ya makazi basi! kwamba zaidi ya hapo ni bahati
tu.
Wengi wa wale wanaolalamika kupata pesa kidogo ni wale walioweka malengo
ya kutafuta pesa ya KULA. Ukiweka malengo ya KULA, ujue malengo hayo ni
madogo sana na kwa vyovyote vile yatavutia pesa kidogo sana kwako. Mtu
yeyote mwenye malengo ya kupata pesa ya KULA, hawezi kuweka utajiri kama
kipaumbele chake. Na mwisho wake ujikuta hana ndoto yoyote ya
kutajirika maisha yake yote.
Ukweli ni kwamba, pesa ya KULA siku zote huwa ni ndogo japokuwa
inapatikana kila ikitafutwa. Pamoja na kupatikana kila siku, tatizo lake
ni moja; kwamba, ikishapatikana muhusika anakuwa tayari ana njaa na
hivyo kuitumia mara moja. Ikishaisha muhusika uenda kutafuta tena, na
huo ndio unakuwa mzunguko na mtindo mzima wa maisha ya kila siku.
Kujiwekea malengo ya kutafuta pesa ya KULA na ADA siyo jambo baya! Ubaya
unakuja pale utakapofanya suala la kutafuta pesa ya KULA kama lengo
lako kuu. Mara nyingi watu waliofanikiwa wanatushauri kuyaweka malengo
ya KULA na ADA ndani ya malengo makubwa zaidi (Utajiri). Tunahimizwa
kuachana na utamaduni wa kuweka KULA na ADA kama malengo makuu katika
maisha, kwasababu, kwa kufanya hivyo tutazidi kupoteza muda mwingi na
matokeo yake hututakaa tupate muda wa kufanya mambo makubwa.
Kwa mfano: “Ikiwa wewe unaishi DAR-ES-SALAAM na lengo lako kuu ni
kwenda KARAGWE, maana yake, inabidi ujipange kutafuta jinsi ya kupata
pesa itakayokuwezesha kufika KARAGWE. Pesa ya kufika KARAGWE
ikishapatikana, maana yake ni kwamba sehemu zote za njiani kabla ya
kufika mwisho wa safari yako kwa vyovyote vile, utafika sehemu zote za
njiani japo hilo halikuwa lengo lako kuu. Sehemu za njiani ambazo kwa
vyovyote vile lazima upite ni pamoja na Morogoro, Dodoma, singida,
Tabora, Kahama n.k. Sehemu zote hizi utaweza kufika kwa kutumia nauli
ile ile ya DAR-ES-SALAAM hadi KARAGWE”
Mfano huo hapo juu, unatufundisha kwamba tunahitaji kuweka juhudi na
maarifa yetu kwenye vitu vikubwa kama vile miradi ya maendeleo (majumba ya kupangisha, kilimo biashara, viwanda, biashara kubwa n.k).
Tukiwekeza akiri zetu kwenye mambo kama hayo ni wazi kwamba pesa ya
KULA na ADA za watoto zitapatikana humo humo ndani ya miradi hiyo. Kitu
cha msingi hapa ni kuhakikisha tunajizuia kufanya kazi ya kutafuta pesa
ya KULA na ADA kama malengo yetu makuu. Tusifanye KULA na ADA kuwa
mwisho wa safari yetu BALI suala la pesa ya kula na ADA liwe ni sehemu
za njiani kuelekea Kwenye ndoto kubwa (Utajiri).
Wito wangu kwako msomaji ni wewe kuiambia akili yako na nafsi yako
mwisho wa safari yako, yaani safari ya kuelekea kwenye maisha
unayotamani kuishi. Naamini ukiweza kuiambia ukweli akili na nafsi yako,
basi ujue hapo utakuwa umefikia hatua ya kutafuta pesa nyingi zaidi ya
hiyo ya KULA na kulipa ADA. Ili linawezekana, limewezekana kwangu,
limewezekana kwa wengine na hakuna sababu yoyote ya kutowezekana kwako.
Subscribe to:
Posts (Atom)