Wateja wako wanapokaa na wewe kwa muda mrefu ndivyo
unavyonufaika zaidi. Hivyo unahitaji kuweka juhudi kuhakikisha wateja
wanabaki na wewe kwa muda mrefu. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia
ili wateja wakae na wewe kwa muda mrefu.
- Toa huduma bora sana kwa wateja wako, ambazo hawawezi kuzipata sehemu nyingine yoyote ila kwako tu.
- Kutengeneza mahusiano mazuri na wateja wako, wafanye wateja kuwa
rafiki kwako na kwa biashara yako, waone siyo tu wanakuja kununua, bali
wanakuja kwa rafiki yao, anayewajali na kuwapa kile kilicho sahihi kwao.
- Weka mbele maslahi ya wateja wako na siyo faida unayotaka kupata.
- Waelimishe wateja wako, washauri vizuri, hata kama utapoteza mauzo,
lakini hilo litawajengea imani zaidi na hivyo kuendelea kununua zaidi.
- Wafanye wateja wako kuwa mashabiki wa biashara yako.
Zipo hatua saba ambazo wateja wanapitia mpaka kufikia ngazi ya ushabiki.
Hatua ya kwanza ni wapitaji tu, wanaisikia au kiona biashara yako lakini hawajawahi kuuliza chochote.
Hatua ya pili ni wateja tarajiwa, wamesikia na wamefuatilia kutaka kujua zaidi kuhusu biashara yako.
Hatua ya tatu ni wanunuaji, hapa wamejua, wakafuatilia na wakajaribu kununua kile unachouza.
Hatua ya nne ni wateja, hapa mtu amejaribu kununua kwa mara ya
kwanza, na amerudi tena kununua. Mtu kununua mara moja haimfanyi kuwa
mteja, na wala haikufanyi wewe kuwa mjanja. Ni mpaka mtu atakaporudi
tena kununua ndiyo utajua umefanya kazi nzuri.
Hatua ya tano ni mwanachama, hapa mteja anakuwa mnunuaji wa mara kwa
mara na unaweza kumpa manufaa ya kadiri anavyonunua. Labda akifika
kiwango fulani anapata zawadi, au akinunua mara tano, ya sita anapata
bure. Hapa mwanachama anakuwa na kielelezo cha kuonesha idadi ya
manunuzi yake.
Hatua ya sita ni mtetezi wa biashara yako, hapa mteja anakuwa tayari
kuwaambia watu wengine kuhusu biashara yako, anatoa shuhuda kwa wengine
na hasiti kuwaalika wengi waje kununua.
Hatua ya saba ni shabiki kindakindaki, hawa ni wale wateja ambao
hawaambiwi chochote kuhusu biashara yako, yaani wao wameshachukulia
biashara yako kama sehemu ya maisha yako. Hawa ni wateja ambao
wanaiongelea biashara yako muda wote, na wakikutana na mtu ambaye
hanunui kwako wanaona anakosa kitu kikubwa sana.
Katika kuboresha thamani ya maisha ya wateja wako, kazana
kuwapandisha wateja wako ngazi mpaka wafikie kiwango cha watetezi na
mashabiki wa biashara yako.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
Kuna aina mbili za gharama ya kupata wateja wa biashara yako.
Aina ya kwanza ni GHARAMA ZINAZORUHUSIWA za kupata mteja. Hapa
unatumia gharama ambazo mteja akinunua mara moja basi gharama ile
inarudi. Chukua mfano umetengeneza tangazo ambalo limekugharimu tsh
100,000/= na tangazo hilo limewafikia watu 1000. Katika hao 1000 ndiyo
wamenunua. Na kwa kila unayenunua unapata faida ya shilingi elfu moja.
Inamaana kwa watu 100, faida unayopata ni tsh 100,000/= sawa sawa na
gharama ulizoingia kutoa tangazo. Hivyo hiyo ni gharama inayoruhusiwa ya
kupata mteja. Kama utaandaa tangazo kwa gharama kubwa kuliko faida
unayopata, hiyo sasa siyo GHARAMA INAYORUHUSIWA kupata wateja.
Aina ya pili ni GHARAMA UWEKEZAJI KWA WATEJA. Hapa unatumia gharama
kubwa, ambayo inakuletea wateja, lakini manunuzi ya mwanzo ya mteja
hayalipi gharama hiyo. Lakini kwa kuwa mteja ataendelea kununua, basi
huko mbeleni ile gharama inarudi. Hivyo hapa unakuwa umewekeza kwa
mteja, ukijua kwamba atafanya biashara na wewe kwa muda mrefu na gharama
zako zitarudi.
Kwa biashara ndogo, ni vyema kutumia gharama zinazoruhusiwa, kwa
biashara kubwa, ambazo zina rasilimali nyingi, zinaweza kuwekeza kwa
wateja na baadaye zikanufaika zaidi. Usikimbilie kununua wateja kabla
hujajua ni gharama kiasi gani unaingia na kama zinalipwa na idadi ya
wateja watakaonunua.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
Kazi kubwa ya kila biashara ni kununua wateja wa biashara hiyo. Sasa
ili biashara iweze kufanikiwa, lazima iweze kununua wateja bora kwa
gharama ambazo siyo kubwa. Kitu ambacho wafanyabiashara wengi siyo tu
hawakifanyii kazi, ila hata hawakijui.
Inawezekana upo kwenye biashara, lakini hujui kama biashara yako
inanunua wateja. Sasa nikuambie tu, kila biashara huwa inatumia fedha
kununua wateja, na biashara yako pia inatumia fedha kununua wateja.
Labda nikuulize swali, biashara yako inatumia gharama kiasi gani
kununua wateja? Na je gharama ambazo biashara yako inatumia kununua
wateja zinarudi? Najua maswali haya yanaweza kukuacha ukiwa umeduwaa kwa
sababu hujawahi kufikiria kuhusu kununua wateja.
Sasa kwenye kitabu nilichosoma ; BUYING CUSTOMERS,
kilichoandikwa na kocha wa biashara Bradley Sugars, mwandishi
ametushirikisha njia sahihi za kununua wateja bora wa biashara zetu na
kwa gharama nafuu ambazo biashara inaweza kumudu.
Kwa kuanza, kila biashara huwa inanunua wateja. Kila hatua unayotumia
kuwafanya wateja wajue kuhusu uwepo wa biashara yako, ni kununua
wateja. Kama umewahi kutangaza biashara yako, umewahi kuandaa
vipeperushi, kama umetengeneza bango, au kuuza vitu kwa pamoja kwa bei
ya punguzo, kama umewahi kupunguza bei ili mteja anunue, au kutoa zawadi
kwa mteja anayenunua. Kama umewahi kutoa usafiri kwa mteja, au
kumpelekea alichonunua, au kumwomba mteja wako akuletee wateja zaidi.
Zote hizo ni harakati za kununua wateja unazotumia kwenye biashara yako.
Sasa kuna ambazo zinakuletea wateja bora, nyingine hazikuletei wateja
wazuri. Nyingine ni za gharama kubwa kwako, nyingine ni za gharama
ndogo.
Kupitia kitabu cha BUYING CUSTOMERS, tunakwenda kujifunza jinsi ya kununua wateja bora kwa gharama nafuu kwenye biashara zetu.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
Njia hizi zinategemeana
na zinaenda kama ngazi, hivyo ili kunufaika lazima uzifanyie kazi kwa
pamoja.
Njia ya kwanza ni kuongeza idadi ya watu wanaoijua biashara yako. Na
hapa ndipo zoezi zima la kununua wateja linapofanya kazi. Kadiri watu
wengi wanavyojua kuhusu biashara yako, ndivyo inakuwa rahisi kwako
kuwageuza watu hao kuwa wateja. Kama watu 1000 ndiyo wanaojua kuhusu
uwepo wako, ukiongeza watu 100 unakuwa umeenda mbele zaidi.
Njia ya pili ni kuwageuza wanaojua kuhusu biashara yako kuwa wateja
halisi. Mtu kujua biashara yako haimaanishi ndiyo mteja wa biashara
hiyo. Mteja ni yule ambaye ametoa fedha na kununua kitu kwenye biashara
yako. ili kuongeza wateja wa biashara yako, unahitaji kuwashawishi wale
wanaojua kuhusu biashara yako wanunue kile unachouza.
Njia ya tatu ni kuwafanya wateja warudi kununua tena na tena. Kama
umetumia gharama kumfikisha mteja kwenye biashara yako, jua kabisa
akinunua mara moja ni hasara kwako. Unapata faida pale mteja anaponunua
tena na tena na tena. Na unachopaswa kujua ni kwamba, ni rahisi kumuuzia
mteja ambaye alishanunua kwako kuliko kumuuzia mteja mpya kabisa. Hivyo
weka juhudi katika kuwafanya wateja waendelee kununua kwako zaidi na
zaidi.
Njia ya nne; kuongeza kiwango cha manunuzi. Kama mteja akija kwako
ananunua kitu kimoja, unahitaji kumshawishi anunue kitu kingine ambacho
kinaendana na kile alichonunua. Hapo unaongeza mauzo na kuongeza faida
pia. Kwa mfano kama unauza vifaa vya ujenzi, akaja mteja kununua rangi,
unahitaji kumshawishi anunue na brashi za kupakia rangi na vitu vingine
vinavyoendana na hili. Kadhalika kwenye mavazi na hata vifaa vya
kielektroniki, mpe mteja wigo wa kununua vitu vinavyoendana na kile
anachotaka.
Njia ya tano ni kuongeza bei, hii ndiyo wengi huwa wanaikimbilia,
lakini ukitumia hizo nne na hii kwa pamoja, utanufaika sana. kwenye njia
ya tano, unaongeza bei ya kitu ili upate faida zaidi. Kama utafanyia
kazi hatua hizi tano kwa pamoja, ongezeko dogo, kama la asilimia 10
kwenye kila hatua, litaleta ongezeko la asilimia 61 kwenye faida. KAZI KWAKO NDUGU .
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
Ili biashara yako ifanikiwe, inahitaji kuweka mkazo kwenye maeneo haya matatu muhimu sana.
(1). THAMANI YA MAISHA YA MTEJA. Wafanyabiashara wengi
huwa wanamwangalia mteja kwa wakati ule anaokuja kununua tu. Huwa
hawaangalii thamani yake ya maisha. Kwa mfano kama mteja akija kununua
kwako mara moja, unapata faida ya shilingi elfu moja, ni rahisi kuona
elfu moja inakuja. Lakini chukua mfano kwamba mteja huyo ananunua kila
wiki, na anaweza kununua kwako kwa miaka mitano ijayo. Hii ina maana kwa
mwaka, anakuingizia faida ya 1000 x 52(idadi ya wiki za mwaka) ambayo
ni tsh 52,000/= na kwa miaka mitano; 5 x 52,000/= ambayo ni sawa na
260,000/=. Thamani ya maisha ya mteja wako huyo ni shilingi laki mbili
na elfu sitini, na siyo ile elfu moja unayoiona anapokuja. Je kwa kujua
hilo hutaongeza umakini zaidi kwa mteja huyu ili aendelee kuwa na wewe
kwa miaka hiyo mitano na hata zaidi?
(2).GHARAMA YA KUMPATA MTEJA. Hapa ndipo gharama za kununua
wateja wa biashara yako zinapoingia. Kabla hujachukua hatua yoyote ya
kuongeza wateja zaidi kwenye biashara yako, lazima ujiulize gharama
unayotumia inaleta wateja wangapi na kama gharama hizo zinarudi kupitia
mauzo. Upo usemi kwenye utangazaji wa biashara kwamba nusu ya bajeti ya
matangazo huwa inapotea, ila mtu hawezi kujua ni nusu ipi. Hii ina maana
kwamba, gharama nyingi watu wanazotumia kutangaza biashara zao
zinapotea, hazirudi kabisa kwenye biashara. Lazima ujue gharama zako na
zinarudije.
(3). KIWANGO CHA WATEJA WAPYA WANAOPATIKANA.
Unapotangaza biashara yako, watu wengi wanajua kuhusu uwepo wako.
Lakini watu kujua kuhusu biashara yako hakukunufaishi chochote. Ni mpaka
pale watu hao watakapochukua hatua ya kununua ndiyo biashara
inanufaika, kama gharama zimepigwa vizuri. Hivyo eneo la kuweka mkazo ni
kuongeza kiwango cha wanaojua biashara kuwa wateja wa biashara hiyo.
kadiri watu wengi wanaofikiwa na tangazo wanakua wateja, ndivyo gharama
za kupata wateja zinakuwa ndogo na faida inakuwa kubwa baadaye.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
Baada ya kutangaza biashara yako, utakuwa na watu wengi wanaojua
kuhusu biashara yako, hawa ni wateja tarajiwa. Sasa unahitaji kuwabadili
hawa na kuwa wateja halisi wa biashara yako. Kadiri unavyowageuza wengi
kuwa wateja halisi, ndivyo gharama ya kuwapata inakuwa ndogo na ndivyo
faida inakuwa kubwa kwako.
Kuongeza kiwango cha wateja wapya, fanya yafuatayo;
- Toa uhakika wa kile unachouza, mpe mteja uhakika kwamba kama
anachonunua hakitafanya kazi basi anaweza kurudisha na akapata kitu
kingine au akarudishiwa fedha zake.
- Tumia shuhuda za wateja walionunua kwako siku za nyuma na wakanufaika sana. shuhuda zina nguvu kubwa ya ushawishi.
- Kuwa na kitu cha tofauti ambacho kinapatikana kwako tu na mteja
hawezi kukipata kwa wafanyabiashara wengine, na mweleze wazi kwamba
atakipata kwako tu.
- Uza viti vya thamani kubwa, ambavyo upatikanaji wake siyo rahisi.
- Tengeneza mwonekano mzuri wa kile unachouza, ikiwa ni pamoja na unavyopakia kile unachouza. Mwonekano mzuri unaongeza mauzo.
- Weka majaribio ambapo mteja anaweza kujaribu kitu kabla hajakinunua.
Njia ambazo unapaswa kuziepuka sana kuwashawishi watu kununua ni
kupunguza bei au kutoa zawadi zenye thamani kubwa. Kwa kufanya hivi
utapunguza faida na pia utavutia wateja ambao baadaye watakuwa wasumbufu
sana kwako.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
Rafiki, kwenye eneo la fedha, ukuaji unapimwa kwa ongezeko lako la
kipato. Na ongezeko siyo la mwaka, bali la mwezi. Kila mwezi, inabidi
kipato chako kiwe kinaongezeka.
Kama kipato chako kinabaki pale pale kila mwezi, kama ilivyo kwa
waajiriwa na hata wafanyabiashara wengi, siyo kwamba unabaki pale pale,
bali unarudi nyuma kwa upande wa kipato.
Kwa sababu kila siku gharama za maisha zinaongezeka, hivyo kipato kisipoongezeka, unazidi kurudi nyuma.
Njia pekee ya kuongeza kipato chako kila mwezi ni kutoa thamani zaidi
kwa wengine. Kama upo kwenye biashara hilo ni rahisi, uzia wateja wengi
zaidi kila mwezi, hata kupata mteja mmoja wa ziada kila mwezi ni hatua
nzuri. Wauzie wateja ulionao zaidi kila mwezi, na pia ongeza bidhaa na
huduma ambazo wateja wako wanahitaji pia.
Kwa walioajiriwa, pia unaweza kuongeza thamani zaidi kwenye kazi yako
au nje ya kazi yako na ukaongeza kipato chako. Kama una utaalamu
fulani, tumia utaalamu huo nje ya kazi yako kwa kutoa huduma za utaalamu
huo. Unaweza kutoa huduma za ushauri kulingana na utaalamu ulionao na
watu wakalipia msaada ambao unakuwa umewapatia.
Chochote unachofanya, hakikisha kila mwezi kipato chako kinaongezeka
zaidi. Na hivyo ni muhimu kila mwezi ukapiga hesabu za kujua kipato
chako ni kiasi gani.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com