Mshukiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda afurushwa
Marekani
- 27 september 2016
Marekani imemrudisha nyumbani msomi
mmoja wa Rwanda anayetuhumiwa kuwa mtu muhimu katika mauaji ya kimbari ya 1994.
Kufurushwa kwa Leopold Munyakazi
kunajiri baada ya kupoteza kesi ya kupata uhifadhi nchini Marekani.
Anatuhumiwa kwa kuvaa majani ya
mgomba wakati wa mauaji hayo ya kimbari ili kujitambulisha kuwa raia wa kabila
la Hutu,mbali na kupanga mashambulio ya usiku katika nyumba za familia za watu
wa kabila la Tutsi .
Bwana Munyakazi ,aliyewahi kuhudumu
kama profesa wa chuo kikuu amekana madai hayo.
Takriban Watutsi 800,000 na watu wa
kablila la Hutu wenye ustani waliuawa na wapiganaji wa Kihutu katika kipindi
cha siku 100 pekee mwaka 1994.
Mauaji ya kimbari ya mwaka 1994
nchini Rwanda
BBC SWAHILI