Anza Mwaka
2016 kwa kuandika Mipango
Yako, ndiyo ramani kuu ya Mafanikio .
Umewahi kujiuliza mtu
anayetembea njiani , hapajui
anakokwenda na hivyo
haijui njia.Akifika njia
panda akamkuta mtu , atamuuliza “ NIFUATE
NJIA IPI ?” Ni lazima
naye atamuuliza “ UNATAKA
KWENDA WAPI ? “ Akijibu
“Sijui”, uwe na uhakika
yule anayetegemewa kuelekeza
atajibu “ CHAGUA NJIA YOYOTE
UIPENDAYO KATI HIZI
NNE ITAKUFIKISHA POPOTE”. Huyu hana
MAONO kwahiyo ni lazima
atajikuta katika matatizo
tu ! HAJITAMBUI ! Kundi
hili ni kubwa
sana katika jamii
yetu wengi wao ni wale
wasio na MAONO
maishani mwao.Wanaishi tu
kwa hapa na
sasa.Hawana ndoto,malengo wala
kitu mbeleni. Hawajatimiza NDOTO
zao wala nini , bali
wapo tu !! Ndio wale
husherehekea MWAKA MPYA
kwa fujo sana kwa
kuchoma mipira, kupiga baruti ,
kufanya fujo , wizi n.k. bila
kujiuliza MASWALI YA
MSINGI.
Mtu
unapaswa KUJITAMBUA-----WEWE NI
NANI ? UMETOKA WAPI ?
UNAKWENDA WAPI ? KUFANYA
NINI ? NA KWANINI ? UKO WAPI ? UNAFANYA NINI ? KWA
NINI UNAISHI . Na siyo
kuishi tu bora
upo au bora
liende ! HAPANA BADILIKA
NDUGU YANGU .
Katika
SAFARI YA MAISHA
YA MAFANIKIO, MAONO
NA MALENGO vina
nafasi kubwa sana katika kuwa na mwelekeo
maalumu wa utendaji ,bila hivyo hutafanya lolote
bali utabaki kulalamika
kila mwaka unaopita
na mwisho wa
siku utajikuta hueleweki. Inakuwa sawa
na gari bila
usukani. Gari hii haiwezi
kuekekea mahali kunako
takiwa,itapoteza mwelekeo .Wakati MAONO
yakiwa kama DEREVA
mwenyewe , MALENGO kwa upande
wake ni USUKANI.Hukuongoza na
kukupeleka unakokutaka.
Ufanye lipi miongoni
mwa mengine. Bila MAONO
kasha MALENGO hautafanya
jambo la maana.
MAONO----DEREVA MALENGO----USUKANI
ANGALIZO: Bila
MAONO kisha MALENGO
hautafanya jambo la
maana ndugu
yangu.
Ndugu yangu kukosa
MAONO maishani ni
hatari. Hata maandiko
matakatifu ,imeandikwa hivi ;
“Pasipo
maono , watu huacha kujizuia “
Mithali 29:18a ,
maana yake Pasipo
maono , watu hushindwa
kujizuia katika mambo
yasiyofaa kama ulevi , wizi , zinaa n.k. ambapo mwisho
wa siku utajikuta
matatizoni. watu hufanya mambo
kiholela , hawana kitu cha
kuwawekea mipaka , hawana chochote
cha kuwasukuma kulifuatilia
jambo kulitekeleza mpaka
wakalifikikisha mwisho wake. Kama
hauna MAONO katika
maisha yako hata
MAISHA yenyewe yatakuwa
hayana msimamo.
Kuna msemo wa
Kiingereza unasema “An idle
brain is the
devil workshop” maana yake
AKILI isiyojishughulisha ni
karakana ya SHETANI.
“Hakuna kitu
kikubwa hapa duniani
kilichofanyika bila maono
na shauku”. ---Georg Wilhelm
Friedrich Hegel.
Watu wengi wanafeli
maishani si kwa
sababu ya kukosa
uwezo au ubongo
au hata UJASIRI
bali ni kwa
sababu hawajakusanya nguvu
zao katika MALENGO.”----Elbert Hubbard.
MAONO NI
NINI ?
MAONO (VISION) kwa maneno mengine
tunaweza kusema NDOTO
ni picha au
matazamio anayokuwa nayo
mtu, shirika au taasisi
juu ya ufanisi
katika jambo fulani.
NINI TOFAUTI
YA MAONO NA
MALENGO ?
Wakati MAONO yakiwa ni
jumla ya picha
ya MAFANIKIO, MALENGO
kwa upande wake
ni kiwango/ kiasi cha
mafanikio ayatakayo
mtu / taasisi ndani ya
kipindi fulani. Tofauti
na MAONO ambayo
kwa kawaida huwa
hayawekwi katika kiwango
na MUDA maalumu ,
MALENGO huwa katika
kiwango na MUDA
maalum. Kwa mfano , unapanga kwamba
katika kipindi fulani nataka
niwe sehemu fulani katika
jambo fulani.Hayo ndiyo
MALENGO. KWA MFANO , MALENGO yako
yanaweza kuwa--------“nataka kuwa
na magari saba
ya biashara ndani
ya miaka mitano “.
Hapo MAONO ni
kuwa na magari (
bila shaka mengi tu )
ya biashara. Lakini MALENGO
ni kuwa nayo
saba ndani ya miaka mitano.
.”
NI HATARI
SANA hivi ndivyo
alivyo mtu ambaye
anategemewa KUFANIKIWA lakini
hana DIRA /MUELEKEO----yaani hana
MALENGO.
ANGALIZO:
Kama huijui NJIA
ya unapokwenda , hakikisha
unayo RAMANI YA
NJIA unayotakiwa kuipita , mikononi mwako. RAMANI ni
dira ya safari .
Inaweza kukuongoza mpaka
mwisho wa safari
yako kama ukifuata
jinsi inavyoelekeza au
jinsi ulivyoipanga WEWE MWENYEWE. MALENGO ni
DIRA ya mtu.Ni
dira ya huko
ankotaka kufika. Ni lazima
uwe na MALENGO
au DIRA kabla
hujaanza SAFARI YA
MAFANIKIO. Kwa kawaida , MALENGO
yote huwekwa mwanzoni
mwa safari.
Watu wasipokuwa na MAONO
kisha MALENGO , hawawezi
kuwa na MWELEKEO
wa kiutendaji. Hawawezi kujipa
NIDHAMU YA UTENDAJI
maana hawana na
hawajui wanapokwenda.
UNAFIKIRI nini kitawasukuma
kufanya BIDII ili
hali hawajui umbali
wanaotakiwa kusafiri kabla
ya muda fulani na
kwa ufanisi kiasi
gani ? Na je !
Lini watajua wamefika
? Watapimaje ufanisi
wenyewe ?
NAMNA YA
KUWEKA MALENGO
Jambo
linalopelekea wengi wetu
kutofanikwa ni kukosa
kuweka MALENGO yanayoeleweka na
yanayotekelezeka kulingana na
MAZINGIRA, MUDA, NYENZO , n.k.
Kuna mambo ya
kuangalia/ kuzingatia kabla hujaamua
kuweka malengo.Unapaswa kutulia
katika hili kwani
hayo ndiyo MAISHA
yako.
Zipo dondoo kadhaa
katika namna ya
kuweka MALENGO ili
uweze kupata ufanisi
katika SAFARI YA
MAFANIKIO kama ifuatavyo :--
(1).LENGA ENEO
NA SHUGHULI MAALUM. Shughuli
na maeneo ya
kufanikiwa ni mengi
mno.Mambo ni mengi
.Huwezi kushughulika na
kufanikiwa yote.Lenga jambo
moja au mawili tu.Kama ni
biashara basi jikite
huko.Baadhi ya maeneo
ya kufanikiwa ni
kama vile Sanaa ,biashara , Michezo, Uvumbuzi katika
teknolojia ya matumizi
ya kompyuta na
mawasiliano ya mtandao
n.k.
(2).WEKA MALENGO
MAALUM NA YANAYOPIMIKA. Ili uweze
kufanikiwa vyema, unatakiwa kuweka
MALENGO yanayoeleweka ,
maalum na yanayopimika
kiasi kwamba unaweza
kwa wakati wowote
kupima / kutambua umeyafikia
na kiasi gani.
(3).WEKA MALENGO
MAKUBWA KIASI KWAMBA
UKISHINDWA KUYAFIKIA BADO
UWE UMEFANIKIWA: Hii
inasaidia ubongo kuwaza
sana na kujishughulisha kwa
kiwango cha juu
zaidi ambapo mara
kadhaa hupelekea mafanikio. Utafiti unaonyesha
kuwa kadri unavyopania / kulenga jambo
kubwa ndivyo akili
yako inajiweka katika
KUFIKIRIA na KUTENDA
kikubwa zaidi.
(4).WEKA MUDA
MAALUMU KATIKA MALENGO
YAKO:
Kumbuka kuwa MALENGO
huenda na MUDA. Bila
kujiwekea MUDA hautapata
msukumo wa kutenda
kwa WAKATI. Pasipo na
MUDA hautaweza kujitathmini---kuona nini
umekifanya / kukipata katika
kipindi Fulani. Kuweka MALENGO
YA MUDA MREFU
na MALENGO YA
MUDA MFUPI kama
mwaka mmoja. JIPANGIE MUDA , JIBANE na
JISIMAMIE WEWE MWENYEWE.
SIFA ZA
MALENGO MAZURI
----Lengo ni lazima
liwe MAALUM na liwe linaelezeka. Mfano lengo
la kuwa daktari
bingwa wa watoto.
----Lengo
lililowekwa vizuri siku
zote huwa LINAPIMIKA.
---Lengo zuri lazima
liwe LINATEKELEZEKA.
----Lengo lazima liwe
LINAFIKIKA.
-----Lengo zuri ni
lazima liwekewe MUDA
wa utekelezaji.
VISION—An idea or
picture in your
imagination.
GOAL---Something
that you hope
to achieve.
Makala hii
imeandikwa na MWL
JAPHET MASATU , Mwandishi,
mwelimishaji, , mhamasishaji
katika masuala ya kimafanikio, ujasiriamali ,biashara na
mambo ya kimaisha kwa
ujumla .Anapatikana kwa namba
: Call / WhatsApp +255 755 400 128 / +255 716 924 136. E-MAIL :
japhetmasatu@gmail.com.
01/01/ 2016 Ijumaa.