Wednesday, June 24, 2015

FANYA MAMBO KWA TOFAUTI. ACHA KUISHI KIMAZOEA



       USIWE  BENDERA  FUATA  UPEPO
 
Kila  siku   asubuhi  tunapoamka  tunafanya  chaguzi  nyingi  sana  kuhusu   maisha  yetu  kwa  siku  hiyo. Huwa  tunachagua  kuoga  au  hapana , kupiga  mswaki  au  la.Huwa   tunachagua  kama  tunywe chai  au hapana.Huwa  tunachagua  tuvae  nguo  gani , na  kwa  akina  mama  tuziweke  vipi  nywele  zetu.Vile  vile, huwa  tunachagua  tupite  njia  gani  kuelekea  kwenye  shughuli  zetu.
  Hebu   jaribu  kujiuliza  kama  huwa  unachaguliwa   au  kuamuliwa  na  mtu   mwingine  yeyote   katika  kufanya  mambo  hayo   unapoamka  asubuhi  nyumbani  kwako.Bila  shaka , wengi  wetu  huwa  tunachagua  wenyewe .Ndugu  yangu   kila  tunachofikiri , tunachofanya  au  kukisema  maishani , huwa  ni  uchaguzi wetu .

JE,  WAJUA   HILI ?  KUFANIKIWA au  KUTOFANIKIWA  maishani  ni suala  la  uamuzi  wetu  wenyewe, kama  vile  tunavyoamua  kuoga  au   kutooga  asubuhi  kabla  hatujatoka  nyumbani  kwenda  kwenye  shughuli   zetu.
Sisi  ndiyo  tunaochagua  maisha  yetu  yawe  vipi. SISI  NDIYO    WAAMUZI.Kwa   sehemu  kubwa , mambo   tunayofanya  ni  matokeo  ya  MAZOEA.Ukishajenga   mazoea  fulani , huwa  unafanya   bila  kujiuliza  na  wakati   mwingine  hujui  kama  unafanya.Hata  pale  unapojua  kwamba  unafanya    na   kujua  kwamba   kufanya  huko  kunakuumiza , unaweza   kushindwa  kujitoa  kwa  sababu  moja tu----MAZOEA.
Kwa  mfano, Mvuta  sigara   anaweza  kujua  kwamba  sigara   inamuumiza   kiafya , mnywaji  sugu  wa  pombe  au  mzinzi  naye  ni  hivyo  hivyo , lakini  kujitoa  inaweza  kuwa   vigumu  sana   kwa  sababu  ya  MAZOEA. Watanzania  wengi  huishi  kimazoea !!
 Kama  tunajitahidi  sana  maishani  bila  Mafanikio, ni  lazima  turudi  nyuma  na  kuanza  kukagua  tabia  zetu  ambazo   zinatokana  na  namna  tulivyoamua  kuyatazama  maisha.Kama  tunachotaka  maishani { mafanikio } hakipatikani , inawezekan  ni  kwa  sababu  tumechagua  aina  ya  maisha  ambayo  haiwezi   kutupa  mafanikio , hivyo  inabidi  tukubali  KUBADILIKA  na KUINGIA  kwenye  KUCHAGUA  aina  ya  maisha  itakayotunufaisha.


     JIFUNZE   SIRI HII :   Naomba  nikueleze   siri  ndugu  yangu, watu  matajiri   na  waliofanikiwa  ni  wale   ambao   hufanya  mambo  kwa tofauti, ni  WANAUME   na  WANAWAKE  mbao  wanaamka  wakati  MASKINI  wanaendelea  kulala  na  kukoroma  katika   maisha  yao. Likiwa   kama  jambo  la  uhakika , watu  matajiri  na  wafanikiwa  wakubwa   ni  watu  wasiolala.Watu  MASKINI  hupenda  kulala   sana !! ACHA  MAZOEA YA  KULALA  SANA!!  Watanzania  wengi  hupenda  USINGIZI  KUPITA KIASI ! NDIO  MAANA  NI  WENGI  NI  MASKINI !
  Ni  ukweli  usiofichika  kwamba, watu  wengi  wameelewa  kwamba, wakati  watu  wanapolala   na   wakati  kila  mahali  pakiwa  kimya  bila  kelele , ndipo  wao   wanapowaza  mawazo  ya  kujenga.
  Cha   kushangaza  ni  kwamba , watu  wachache  tu  ndio  waliofanikiwa  katika    mataifa  mengi   duniani. Nenda  kawaulize  washerekeaji  wa  mafanikio  katika  eneo   lolote  lile, kama vile  biashara  kubwa  ya    ujasiriamali , inayosukuma   na  kushawishi  wengine, watakuambia  kuhusu  ukweli  huu. Ni  wale  wanakaa  macho  wakati  wa  usiku  wakifanya  kazi , kutafakari , wakipanga  mipango  na  kuyafanyia  kazi   matamanio  yao, wanacheka  na   kuchukua  vitu   kirahisi . Siku  inapoisha  wengine   wanahangaika , wakisukumana  na  kufukuzana   katikati  ya  makundi  ya  watu  wanaopiga  kelele  mitaani , katika  maofisi   na  sehemu  za  masoko.


WAKATI  WA  USIKU NI  MZURI  SANA  KUUTUMIA  :  KWANINI ?
MATAJIRI  wengi    wamejikita  zaidi   katika  muda  wa  usiku  ambapo  hakuna  washindani  wengi  zaidi    wakati  hakuna  kusukumana  na  haraka, hakuna  kelele  zitakozozuia  kuwaza  kwao  na nafsi   zao.Watu  wengi  ni  MASKINI  kwa  sababu  wanalala   kupita  kiasi  hawana  muda  wa  kutafakari,na   kupanga  mipango  na  kuyafanyia  kazi   malengo  yao. Tumepewa na  mwenyezi  MUNGU  muda  wa  saa  24  tuutumie  vizuri  ili  kuboresha  MAISHA  yetu !  Watanzania  tubadilike  sasa ! Haina  maana  ya  kwamba  ukeshe  usilale  ndugu   yangu, hapana  ni  kuwa  na  MUDA  WA   KUTAFAKARI, KUPANGA  MIPANGO, KUFANYA  KAZI .Usiku   ni  muda  mzuri  kutokana  na  UTULIVU  ULIOPO  tofauti  na   mchana.Na  wewe  ndugu  yangu Mtanzania   tumia  muda  wa  usiku   KUFANYA  MAMBO  TOFAUTI  YA  UBUNIFU ! Sisi  binadamu  tunapaswa  kuwa  wabunifu kwahiyo  tunahitaji  muda  wa  ziada  ili kuwekeza    nguvu  zetu, mali  zetu , na  muda   wetu   kwenye   ubunifu  wetu.Tuutumie  USIKU  kwa kutafakari  mambo  yetu  ya  ubunifu !

NENO   LA  HEKIMA : “ Kama  ni  lazima  upate  amana  ya  pesa  na  kuwa  na  pesa  zisizo  na  mpaka, jifunze   kutumia  nyakati  zisizo  za  kawaida  kwa  ajili   ya  kuwaza  uzalishaji

 

KWA  WANAFUNZI : Akili  ya  binadamu  huhitaji  utulivu na  ukimya  wakati  wa  kujisomea. Usiku ni muda  mzuri sana kwa  mwanafunzi  kujisomea.Hakuna kelele  za  aina  yoyote , watu  wamelala !!KANUNI INASEMA  Ili uamke  usiku kujisomea  unahitaji  “KULALA  MAPEMA  ILI  UAMKE MAPEMA”  Ukiwa  unalala  kwa  kuchelewa  zoezi  la  kuamka usiku ili  ujisomee  litakushinda   mwanafunzi  wangu! Kama  unahudhuria  prep.  Lala  saa  4  usiku,amka  saa 10 . Kama  huudhurii  prep.   Lala  saa  1 au  saa  2  usiku na  amka  saa saa  9  usiku! Uwe  na muda wa  kupumzika kila  dakika  45  au  saa  1. Muda  wa  saa 2 au  3 kwa  kusoma  unatosha sana.
Siyo  lazima usome  usiku, pia  inategemea  wewe  mwenyewe  mwanafunzi   ni  wakati  gani mzuri  kwako  kwa  kujisomea ?  je, ni   asubuhi, mchana au  jioni !  USISOME   KIMAZOEA !usifuate  mkumbo , wenzako  wamefanya  hivi , na  wewe waiga ! wenzako  wanapiga  stori   darasani muda  wote  nawe   wajiunga ! ACHA  HIYO !  kuwa  wa  tofauti jali  muda wako  kimasomo  zaidi. Na  utafanikwa ! HESHIMU  RATIBA  YAKO  BINAFSI, RATIBA  YA  SHULE, WAHESHIMU  WAZAZI/ WALEZI  WAKO,NDUGU ,MAJIRANI, WALIMU  WAKO  SHULENI , WANAFUNZI  WENZAKO, WASIOJIWEZA/ YATIMA nk.
Kanuni  inasema, “ If  you  wake  up early ,  you  need  to  go   to   bed   early. If  you keep  up   late, you  need  to   wake  up  late.   maana  yake   Kama  unataka  kuamka  mapema, nenda  ukalale    mapema. Na  kama  unataka kuamka  kwa  kuchelewa , kalale  kwa  kuchelewa !
Tafadhali mwanafunzi   potezea  mambo ambayo yatakupotezea  muda  kama   masuala  ya  mapenzi, disko, kuangalia  video/tv, kulala kupita  kiasi, kunywa  pombe,kupiga  stori, n.k.
 Siku   zote  usikubali kuwa  mtu  wa  kawaida. FANYA  YALE   YA  TOFAUTI. USIISHI  KIMAZOEA   KAMA  WATU  WENGINE !!  BADILIKA , KUWA  WA  TOFAUTI, MAFANIKIO  NI  YAKO !! USIWE   BENDERA   FUATA  UPEPO !
Kwa  mfano ,   mimi  binafsi  huwa  naandika  makala  zangu hizi   wakati  wa  usiku wakati  watu   wengine   wamelala. Huwa napenda   kujisomea  usiku ! Kwangu   binafsi  usiku  naupenda  sana  kwa   kufanya  masuala  yangu  ya   kiubunifu ! Huwezi ukatumia  muda  wa  MCHANA  pekee  kufanya  mambo  yote , ni  lazima  pia  uutumie  USIKU  kama  kweli  unapenda   kupata   MAFANIKIO  MAISHANI !!
 

USINGIZI  HULETA   UMASKINI ! Utalala  hadi   lini   ewe mtanzania goi  goi ?  Lini  utazinduka  kutoka  katika  usingizi  wako ? “ Bado  kulala  kidogo, bado  kusinzia  kidogo, bado  kukunja  mikono  upate  usingizi.Hivyo  UMASKINI  wako  huja  kama  MNYANG”NYANYI  na  uhitaji  wako  kama  mtu  mwenye  silaha.” { MITHALI  24:33,34 }.
   MITHALI  26:13  inasema : “Mtu  mvivu  husema, simba  yuko  njiani.Simba  yuko  katika  njia  kuu .” Ni  nini  asemacho  mtu   mvivu ? Hujitoa  kwenye  majukumu  yake. Anapenda  kukaa  nyumbani   na  kukifanya    kitanda   kuwa  rafiki  yake.Mtu   mvivu  si   mbunifu.Huogopa  kuthubutu. Hupenda   kukaa  na   kujifariji.

       USHAURI  WANGU !  Kama   una  nia  ya  kutengeneza  PESA , hunabudi  KUPIGANA  NA  UZEMBE. Usiufanye  USINGIZI  kuwa   rafiki  yako  kwani  huwezi   kutengeneza   PESA  kitandani.WEWE    NI   MASKINI  KWA  SABABU  UNALALA .UKWELI  NI  KWAMBA  , USINGIZI  umewakaba  watu wengi  na  kupoteza  HATIMA  zao. Watanzania  wengi  ni  wavivu , wazembe , wanapenda  kulala  kupita  kiasi. Maandiko  matakatifu  yanasema  “ Ukipenda  Usingizi    utakufa   Maskini “  Yaani  KULALA  KUPITA KIASI. Mwili  huhitaji  saa  8 ili    kuendelea   kufanya   kazi  yake  kama  kawaida .Ukilala  pungufu  ya  hapo , ni  lazima  utalipia  usingizi  uliobaki  popote  pale  haijalishi  upo  wapi ! Hii  ni  suala  la   kimaumbile  zaidi .
 
Mungu anamchukia   mtu  mvivu   ndugu yangu ! “ Uvivu  humtia  mtu  katika  usingizi  mzito, na  nafsi  yake  MVIVU  itaonja  njaa” { MITHALI  19:15 }. Mungu  anatutarajia  tuwe  tunaamka  mapema  na   kufanya  kazi   kwa  bidii  popote   pale  alipotuagiza.Kwahiyo   ndugu  yangu  mtanzania , usifuate  mambo  yaliyozoeleka  na  ya  kawaida.Tuache  kuishi   kimazoea. CHAGUA  KUWA  TOFAUTI !! JITIISHE  MWENYEWE  KUWA  TOFAUTI. INAWEZEKANA, NA  UNAWEZA  KUFANIKIWA !


NENO  LA  HEKIMA “ Lazima  uwe  tofauti !  Utofauti  wako  ndio  ushawishi    wako, Ushawishi  wako  ndio  Utajiri  wako “  {  Greg  O. lyoha }.

    Kama  tunaamka   asubuhi  na   kuchagua  kwamba  siku  itakuwa  ngumu   na  mambo  hayataenda  vizuri , ni  wazi  huo  ndio  uchaguzi  wetu   na  ni  kweli   itakuwa   ya  hovyo  kwetu  kumbuka   tunapata  kile  tunachochagua.Tukiamka  na  kufikiria   kinyume  na  hayo  , ni  wazi  mambo  yatakuwa  kinyume , yaani  yatakuwa  mazuri. 

        Asante  msomaji wangu, HUJACHELEWA , UNAWEZA  KUFANIKWA. Endelea kutembelea  blog  yako hii  kwa  kujifunza  zaidi   ! Mungu akubariki  sana !

Makala  hii  imeandikwa  na  MWL.  JAPHET   MASATU.Ni  mwelimishaji  na  mhamasishaji    katika  masuala   ya  maisha  na  mafanikio ,Saikolojia , biashara / ujasiriamali . Anapatikana  kwa   + 255 716 93 4236 / + 255  755  400 128.
 japhetmasatu@yahoo.com