Watu
wengi hujiuliza , “ SIRI YA
UTAJIRI NI NINI ? “
Je ni mbinu
gani zinaweza kumsaidia
mtu kupata UTAJIRI ?
Siri kubwa ya
UTAJIRI ni kuwa
MBUNIFU, unabuni njia mbalimbali
za kuingiza kipato
yaani unatega MITEGO / MIRADI. Kadiri unavyotega mitego
ndivyo unavyo nasa FEDHA zaidi .
Lazima
ubuni kitu chochote
kinachoweza kutoka kama
BIDHAA au HUDUMA.Unapotoa bidhaa
unapata FEDHA kwa
kadiri ya bidhaa
uliyotoa.Na unapotoa huduma
utalipwa na inawezekana
ukalipwa kwa masaa, siku , wiki na
hata kwa mwezi.
TAMBUA HILI : Fedha
haina mwenyewe , wala upendeleo, si
za watu wa
kabila au taifa
fulani , tabia mojawapo ya
fedha ni kwamba
hufuata MTEGONI AU
MRADI uliobuni. Hivyo jifunze
kutega mitego mbalimbali
ambayo mwisho wa
siku , mwezi au mwaka
utasema umepata fedha. Fedha
zipo kila mahali
yaani mijini na
mashambani. Hutembea huku na
kule zikifuta mahali imewekewa
MTEGO.
Fedha
hufuata mbunifu ! hutoroka
mvivu ! hutembea huku na kule ,hupenda mwerlevu , n.k. hufuata
na kuingia kwa Yule
anaye
zitengenezea njia na mahali
pa kuingia.
HAKUNA MUUJIZA
WA KUAPATA FEDHA
!! Usidanganyike kwamba
utapata muujiza wa fedha
ukuangukie kama palachichi , pesa zinatafutwa
zinategewa mitego , zinaweza kutoka
kwa mteja, ndugu , rafiki , au
Mungu akatumia mtu
yeyote kukupa fedha, kitendo ambacho
tunakiita muujiza , na wala
sio mtu anakaa
hafanyi chochote, ati anangojea
muujiza wa fedha, ndio
maana wengi hawana
kitu.
ACHA UVIVU : Usiwe mtu wa
kukaa bila kufanya
kitu, hata kama
huna kazi tafuta
kazi ambayo itakupatia
kipato bila kusahau
KUWEKA AKIBA ,asilimia 20
ya kipato chako
usitumie yote hata
kama mshahara ni
mdogo kiasi gani. Usijali
muda,usiwe na haraka . Baada ya miaka kadhaa,unaweza kuwa
na MTAJI mkubwa
wa kuanzisha shughuli
yako yoyote , iwe ni
biashara au vinginevyo .
Tumia hicho kipato
kuanzisha kitu chako. Wewe
acha sababu zisizo
za msingi ambazo
wengi hujifariji nazo
na kumbe ni
WAOGA na wasiotaka
KUTHUBUTU kufanya jambo,
Mtu mvivu
husema , simba yuko nje, nitauawa
katika njia kuu.
{ MITHALI 22:13
Wengi wana
sababu nyingi hasa
vijana wanasingizia serikali
haitaki kuwapa AJIRA !!!
Vijana dunia ya
sasa ni UJASIRIAMALI
SIYO AJIRA YA
SERIKALI. Walioko katika AJIRA
YA SERIKALI wanapata
shida sana kwa
kutegemea mshahara !! Hautoshi !!! CHUKUA KARATASI
NA KALAMU TUFANYE MAZOEZI
MAWILI TOFAUTI TUUONE UKWELI
WA MAMBO !!
Hebu
chukua karatasi na
uandike orodha ya mahitaji
yako mfano kutoa michango
ya arusi ,msiba n.k. kulipia umeme ,kugharamia chakula
kila siku ,kumlipa mshahara
mfanyakazi wako wa
ndani , kununua vocha za
simu , kununua nguo/mavazi ,
kulipia nauli/ usafiri , kulipia / kununua maji ,
kutengeneza nywele saluni,
kugharamia huduma za
internet , kutoa sadaka,
zaka na
changizo mbalimbali kwenye
dini zetu , kuhonga—unacheka hiyo
ipo , kulipia matibabu, n.k.
Orodha
ni ndefu sana
ya mahitaji yetu
ndugu zangu watanzania. Fanya zoezi
la pili chukua karatasi na
andika Orodha ya
vyanzo vya mapato YAKO yaani MIRADI / MITEDO YA
FEDHA !! Vipi mbona
washangaa ANDIKA !!!! HAKUNA !!
BASI SAHAU SUALA
LA KUWA TAJIRI
KAMA HAUTACHUKU A HATUA !!!
Unaona
sasa Mishahara haiwezi
kutosheleza mahitaji yet
hata kidogo !!
USHAURI WANGU :
Wewe uliye
na kazi zako
au za watu
yaani waajiriwa ,
jitahidi sana uwe
na shughuli zako
ambazo zitakuingizia kipato
cha zaidi. Jitahidi hata
kama una shughuli
zako kama ilikuwa moja, ziwe
mbili, tatu au zaidi. Tumia
kipato cha mshahara
wako KUWEKEZA.
JE,
WAJUA ?
Kila
shughuli au kazi
yoyote utakayoibuni ujue
mna faida , hivyo huna
budi kuifanya kwa
moyo mmoja ukijiua
kupitia hiyo shughuli
au kazi ndiyo
itakayo kuletea Mafanikio
ya kifedha.
Katika kila
kazi mna faida , bali
maneno ya midomo
huleta hasara tu.
{ MITHALI 14:23 }.
WENGI WANASEMA
HAWANA MTAJI WA
BISHARA . NDIYO SABABU YA
KUTOFANIKIWA KIMAISHA. JE, NI
KWELI ? Cha msingi
ni kuwa na nia ya
kufanya kitu, . MTAJI sio
tatizo , tatizo ni kutokuwa
tayari na kukosa
ubunifu wa kufanya
kitu. Unapokuwa na nia
mtaji utapatikana maana
PENYE NIA PANA
NJIA. MTAJI unaweza kupatikana
toka kwa wale
walio karibu nawe, ndugu,
marafiki au taasisi
za kifedha. Uoga wa
kuthubutu , Kutojitambua , uvivu , kukosa
maarifa , ujuzi, elimu
sahihi ya biashara na
mbinu za kutafuta
fedha ni miongoni
mwa mambo yanayotufanya na
kutukwamisha tusifanikiwe. Nitaeleza
kwa kirefu njia
mbalimbali za kupata
MTAJI katika makala
yangu yenye kichwa NI VIPI
UPATE MTAJI ? ndani ya
blogu hii . MAISHA NA MAFANIKI
BLOG
NINI TOFAUTI
YA MASKINI NA
TAJIRI ?
Tofauti kati
ya MASKINI na
TAJIRI iko katika
kuchukua hatua. Tajiri hujifunza
mambo ya kumwendeleza
na KUCHUKUA HATUA AU KUTHUBUTU
kwa kutekeleza kwa
vitendo yale anayojifunza
na anayoyaona yanaweza
kumuinua kiuchumi.MASKINI huwa anajifunza
mambo na kuyaacha
kichwani bila kuchukua
hatua au kuyafanyia
kazi aliyojifunza na
hivyo FURSA ya
KUPATA UTAJIRI inampita hivi
hivi.
Siri
kubwa ya UTAJIRI
ni kujifunza elimu
ya kutafuta mtaji , kuwekeza kwa
busara kwa namna
ambayo daima panakuwa na
ziada na faida.
Kwa bahati mbaya
sana, elimu hii haifundishwi
darasani ila wanayo
wafanyabiashara wachache na
kila anayefanikiwa kuifunza
siri hii huwa
TAJIRI na huendelea
kuificha.
NJIA ZA
KUKUWEZESHA KUWA TAJIRI
{1}.Wataalamu
na Watafiti
wa masuala ya
fedha wamegundua njia rahisi ya kupata UTAJIRI ambayo haihitaji
uwe na kipato
kikubwa, kama unafanya
kazi na Kipato
chako ni kidogo anza
LEO kujenga tabia ya kuweka AKIBA ya
T.shs 1,000 kila siku
sawasawa na TShs
30,000 kwa mwezi , matokeo yake
ni kwamba kama
utaweka AKIBA yako
kwa kipindi cha
miaka 65 ila
riba yoyote utakuwa
na AKIBA ya
Tshs 23,725,000 { Milioni Ishirini
na Tatu Mia
Saba Ishirini na Tano
Elfu }. Kama utawekeza fedha
hiyo na kuapata
riba ya asilimia
10% kwa kila
mwaka itazaa na
kukuletea Tshs 2,750,000,000 { Bilioni Mbili
na Milioni Mia
Saba Hamsini }.
{2}. Unaweza
kurithi mali na
fedha kutoka kwa
wazazi wako. Hii ni
njia ya kubahatisha
kwani watu matajiri
siyo wengi na
hivyo watoto wenye
bahati kama hii
ni wachache pia. Nikiwa kama
mwalimu na
mwelimishaji huwa nawaambia wanafunzi
wangu wasome kwa bidii
sana wafaulu mitihani
yao na kuendelea
mbele kielimu , wasitegemee sana
mali na fedha
za wazazi wao . Katika
familia zetu hizi
za kitanzania suala hili
haliko sawa huleta
migogoro sana kuhusiana
na mali na
fedha za wazazi . Watoto hugombana
sana mpaka kupelekana
mahakamani . Katika familia zetu
hizi watoto ni
wengi , mali ni chache . Katika familia
zenye ndoa za
mitara, tatizo hili
kubwa sana . Haliwezekani kabisa. Zipo
familia chache sana
waliofanikiwa kuwarithisha watoto
wao fedha na
mali bila migogoro
miongoni mwa watoto.
Kwa wenzetu
nchi zilizoendelea inawezekana
kumrithisha mtoto fedha
na mali kutoka
na mifumo yao
maisha ipo vizuri.
Familia zao zinajali
sana kuhusiana na
idadi ya watoto
wanaozaliwa huku kwetu
Afrika hatujali sana kuhusiana
na uzazi wa
watoto na matunzo
yao . Huku kwetu urithi
wa mtoto no elimu
tu.
{3}.Unaweza
kusomea ujuzi au
utaalamu katika fani
yenye malipo mazuri
na KUJIAJIRI mwenyewe. Kwa
mfano , unaweza kusomea fani
kama UANASHERIA , UHASIBU,
UDAKTARI,UFAMASIA , UFUNDI , UALIMU,
SANAA, UFUNDI WA VIFAA VYA
ELEKTRONIKI, n.k. Unaweza kuanza
kwa kuajiriwa kwenye
ofisi inayotoa huduma
ya fani yako
ili upate uzoefu
na siri ya
biashara au kazi
hiyo. Kisha tafuta
kuanza taratibu kufanya
kazi zako binafsi. Ukiona biashara
yako inaenda vizuri
acha kazi na
uende kufanya biashara
yako kwa juhudi
na maarifa yako
yote na UTAFANIKIWA.
Tafadhali
sana msomaji wangu
kama ni wewe
au ndugu yako
au rafiki yako
usimshauri kuacha kazi
ya kuajiriwa haraka
!!! Wanafunzi ambao wapo
vyuoni , mashuleni huwa
nawaambia ukweli njia
ya uhakika na
nzuri ni kusomea
ujuzi au utaalaamu
na kuwashauri KUFANYA
JUHUDI KATIKA MASOMO
YAO ILI WAFAULU
VIZURI !!
{4}.Kuwa na BIASHARA
yako na
kuiendesha ili kupata ziada na
faida kubwa. Anza kufanya UTAFITI
kuona utafanya biashara
gani.
{5}. Unaweza
kutunga VITABU juu
ya suala lolote
unalolijua.Kwa mfano Unaweza
kutunga kitabu kuhusu
suala lolote ambalo
linaweza kuelimisha jamii
au kuburudisha jamii. Kwa
mfano unaweza kutunga
kitabu cha hadithi
na unaweza kueleza
jambo lolote linalogusa
jamii. Au Kama wewe
ni mtu uliyebobea
katika masuala ya
muziki unaweza kutunga
kitabu kinachofundisha namna
ya kuwa mwanamuziki. Watunzi wengi
wa vitabu ni
Matajiri wakubwa. Hii Ni
kazi unayoweza kuifanya
kwa shida mwanzoni
na mara moja lakini
ukavuna matunda yake
kwa muda mrefu.
{6}.Unaweza
kuwa MBUNIFU na
kuanza kuuza mawazo
yako au kutumia
chombo ulichokibuni kukuingizia
fedha.
{7}. Unaweza
kuendeleza VIPAJI vyako
na kuwa mwanamichezo
au msanii wa
kulipwa. Usidharau kipaji chako
chaweza kukutajirsha sana . Kwa
mfano kipaji cha
ualimu , uimbaji , ususi , uchoraji , uimbaji, kupiga vyombo
vya muziki , kucheza mpira
wa miguu , n.k. Kila
mtu –kila mtu hata
wewe msomaji wangu, umepewa kipaji
na mungu .Hakuna mtu
asiye na kipaji. Wengi
wetu tuna tuna
vipai zaidi ya
kimoja{ multigifted}.Nitaeleza
kwa vizuri na
kirefu kodogo katika
makala yenye kichwa
KITUMIE KIPAJI
CHAKO KIKUTAJIRISHE
{8}. Unaweza
kucheza bahati nasibu
na kushinda.Watu wengi wanapenda
kucheza michezo ya
kubahatisha . Hiki ni kitu
cha kubahatisha uwezekano wa
kutajirika kwa njia
hii ni mdogo
sana.Hivyo nawashauri wasomaji
wangu kuachana kabisa
na njia hii
ya kutafuta UTAJIRI.
{9}. Kama
wewe ni Mwajiriwa
, kipimo chako cha
Mafanikio kiwe ni
kujiuliza swali, kama utaacha
kazi yako ya
Mshahara utaweza kuishi
kwa kutumia kipato
chako cha pembeni
kwenye biashara yako
kwa muda gani ? Mafanikio yako
yatakuja pale utakapoweza
kutumia kiapto chako
cha ziada bila
kutegemea mshahara , na
hapo ndipo unaweza
kuacha kazi na
kwenda Kuimarisha biashara
zako au kuendelea
na kazi huku
pia ukijiaamarisha kibaiashara.
{10}.Panga
malengo ya muda
wa mwaka mmoja , miaka
mitano na miaka
ishirini ili kuhakikisha
kwamba unajikomboa kiuchumi. Malengo yako
makuu yawe n :--
Kuwa na AKIBA
ya fedha za
kutosha katika akaunti
yako , kuwa na biashara
yako , na VITEGA UCHUMI
VYA AINA TOFAUTI
ambavyo unaweza kuvisimamia
vizuri.
{11}. Jifunze
mbinu za kutafuta
fedha. Njia rahisi na ya uhakika
ya kukuwezesha kufanikiwa kiuchumi
katika maisha ni
kutafuta MSHAURI AU
MTAALAMU anayejua mbinu
za uongozi wa
biashara ili akushauri
vizuri juu ya
yale unyonuia kutekeleza. Pia SOMA
VITABU VYA BIASHARA
ili uweze kupata
maarifa mapya !! Ndugu Msomaji
wangu MAARIFA NI
NGUVU.
Kwa
kuhitimisha nasema fedha
ni chombo cha
muhimu sana kwa
kila mtu anayeishi
chini ya jua au dunia
hii kwa kukidhi
mahitaji muhimu ya
kibinadamu. Ni chombo kinachotumika kuhalalisha
mambo baina ya
pande mbili yaani
kwa MTOAJI na
MPOKEAJI katika kulinganisha
mapatano yaliyofikiwa katika
hali ya kununua
au kuuza.Ni chombo
ambacho kila mtu
anahitaji kuwa nacho.
Neno la mungu
linasema fedha na
dhahabu ni mali
ya MUNGU na
wala sio ya
shetani. Kama fedha ni
mali ya mungu
na sisi tu
watu wake basi
tunayo haki ya kumiliki
na kuwa nayo
katika hali ya
utele.
Fedha na
mali yangu na
dhahabu ni mali
yangu, asema BWANA wa
MAJESHI { HAGAI 2:8 }
Makala hii
imeandikwa na MWL
JAPHET MASATU , anapatikana
kwa namba + 255 716 924 136 /
+ 255 755
400 128 / + 255
785 957
077. Kama
una lolote unataka
kuchangia mawazo , ushauri kuhusiana
na mada yetu
hii SIRI YA
UTAJIRI . Karibu sana.
Kama unataka
kuniuliza swali kuhusu mada
yetu hii uliza
!!!