Saturday, June 2, 2018

WEWE UNAANZIA WAPI ? TATUA MATATIZO YA WATU YALIYOSHINDIKANA NA WATAKUWA TAYARI KUKULIPA !

4 comments:

  1. Kila mtu anapenda kufanikiwa, kila mtu anatamani kufanikiwa.

    Lakini mwisho wa siku, wachache sana ndiyo wanaoishia kufanikiwa. Wengi waliotamani kufanikiwa wanaishia kuwa kawaida na hata wengine kushindwa kabisa.

    ReplyDelete
  2. Katika wale wanaoshindwa, siyo wote ambao hawajakazana, wapo ambao wamekazana na kujitoa sana, lakini bado wanakuwa hawafanikiwi. Hawa ndiyo wanaoishia kufikiri kwamba huenda mafanikio ni bahati na kwao haikuwa bahati.

    Ukweli ni kwamba, mafanikio siyo bahati, na kama bahati inachangia kufanikiwa, basi inakuwa ni matokeo ya maandalizi kukutana na fursa. Mafanikio hayaanguki tu kwa mtu aliyelala na kutamani mafanikio yatokee. Bali mafanikio yanatokea kwa yule anayetaka kufanikiwa, anajua kanuni za mafanikio, anajua ufunguo muhimu wa mafanikio na anaweka juhudi kupata mafanikio hayo.

    ReplyDelete
  3. Watu wana shida, watu wana uhitaji, watu wana changamoto na watu wanapenda maisha yao yawe bora zaidi. Mambo ambayo yanafanya maisha ya wengi kukwama ni magumu, ambayo yanawasumbua sana. Kwa jinsi mambo hayo yalivyo magumu, watu hao wanakuwa tayari kulipia suluhisho linalofanya maisha yao kuwa rahisi zaidi.

    ReplyDelete
  4. Ufunguo muhimu wa MAFANIKIO ni KUTATUA MATATIZO MAGUMU NA YALIYOSHINDIKANA.

    ReplyDelete