BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE. JIFUNZE ---ELIMIKA --CHUKUA HATUA---FANIKIWA
Thursday, May 15, 2025
MAKALA : USILAUMU WAZAZI , SI KOSA LAKO HATUKUFUNDISHWA KUHUSU ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA NA MAUZO---JIFUNZE UINUKE---BIASHARA NI AKILI NA MAARIFA------------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
*Siyo Kosa Lako, Hujafundishwa TU!*
Kakaa/Dadaa..
Unajua kuna watu wanawacheka wajasiriamali wadogo?
Huku wakiwasema vibaya:...
*Mbona kila biashara unayoanzisha haifiki miezi mitatu?*
*Unapenda kulalamika sana!”
*Wewe huwezi fanikiwa kamwe!*
Na huwa naumia nikisikia haya maneno.
Kwa sababu…
Watu hawajui mateso yanayomfanya mtu aamue kuuza maandazi saa 12 asubuhi bila hata chai.
Hawajui…
Maumivu ya kutafuta mtaji wa elfu 20 kwa kuazima mia mia.
Kunyanyaswa na maneno ya jamaa zako:
“Kama ni biashara ya maandazi si kila mtu anafanya?”
Kukesha ukitengeneza sabuni halafu asubuhi mvua inanyesha, hakuna mtu hata mmoja kununua.
Sasa leo nakuambia ukweli:
Siyo Kosa LAKO.
Haujafundishwa TU!..
Tatizo Si Wewe, Ni Mfumo Wetu.
Shule zetu hazikufundisha namna ya kuuza.
Hazikufundisha namna ya kujua faida.
Hazikufundisha namna ya kumshawishi mteja.
Tulifundishwa 1+1=2.
Lakini hatukufundishwa jinsi ya kutengeneza buku kwa kuuza karanga.
Ukatoka shule ukiwa na degree.
Au ukiwa form four.
Au hata bila cheti.
Lakini wote mko sokoni mnaanza biashara kama vipofu wanaovuka barabara.
Na Ndio Maana…
Unajikuta unafungua duka la vocha,
Unaanza kuuza na sabuni tano, pipi za mchina, na airtime ya mia.
Mwishoni mwa mwezi…
Umeuza elfu 50.
Umebakiwa na 10.
Na hata hujui imepotelea wapi.
Wewe si mzembe.
Wewe si mjinga.
Wewe ni mtu jasiri lakini hujapewa silaha.
Sasa Sikiliza Hii:
Kabla hujaanza biashara yoyote…
Unahitaji kujua vitu vitano tu vya msingi:
1. Shida ya watu ni ipi?
Watu hawataki bidhaa, wanataka suluhisho.
2. Unawauzia kina nani?
Hakuna biashara ya “kila mtu”
3. Unawafikiaje?
Kama hawaitwi hawaji. Kama hawajui hawanunui.
4. Bei yako inasemaje?
Bei nzuri haimaanishi rahisi inamaanisha INAOANA na thamani.
5. Faida yako iko wapi?
Si pesa inayoingia, ni pesa inayobaki baada ya gharama.
Stori Ya Kweli Ya Dada Zawadi Wa Gongo La Mboto....
Zawadi alikuwa anafua nguo kwa watu.
Kila siku jua likitoka, anajitwika ndoo, anazunguka mtaani akitafuta wateja wa kuwafulia hadi jioni.
Analipwa elfu mbili elfu tatu.
Anaondoka na macho mekundu, mikono iliyochubuka,
Lakini hana hela hata ya sabuni.
Siku moja alihudhuria semina ya biashara.
Akaambiwa kitu kimoja tu:
*Fungua huduma yako. Uisajili. Toa package. Weka namba zako mitandaoni.*
Leo Zawadi haendi nyumba hadi nyumba.
Anapokea simu.
Wateja wanamfuata.
Anatoza elfu kumi hadi elfu ishirini kwa huduma ya kitaalamu.
Na bado anafua nguo.
Lakini kwa akili.
Tunaambiwa tukomae. Lakini hatuambiwi namna.
Tunaambiwa tufanye kazi kwa bidii. Lakini bidii bila maarifa ni kama kukata mti kwa kijiko.
SULUHISHO?
Sihitaji nikuambie uache biashara.
La hasha.
Nakuheshimu.
Ninachokuambia ni hivii…:
Chukua hatua ya kutafuta elimu ya msingi ya biashara.
Elimu inayoeleweka.
Elimu ya mtaani.
Elimu ya kweli.
Kabla hujapoteza muda tena,
Kabla hujakataliwa tena,
Kabla hujachoka kujaribu jifunze.
Kwa Nini?
Kwa sababu:
Huwezi kufanikiwa kwa kukurupuka.
Na
Siyo kosa lako kuwa hujui.
Lakini litakuwa kosa lako ukikataa kujua.
Kama makala hii imekuongelea wewe, huna haja ya kujionea aibu.
Kila shujaa alianza akiwa hajui.
Lakini waliamua KUJIFUNZA.
Nataka nikupe silaha mbili za siri.
Ni silaha za kumtokomeza ujinga,
Silaha hizo ni Elimu Ya Msingi Ya Biashara na CHUO CHA MAUZO, Kwa Mtu Wa Mtaa.
#SioKosaLako
#JifunzeUinuke
#BiasharaNiAkiliNaMaarifa
Tuesday, May 13, 2025
KITABU 338 : JIFUNZE BIBLIA TAKATIFU --( 08)----AGANO JIPYA --( 08 )---YESU---NAMNA INJILI ZILIVYOTUNGWA , INJILI ILIVYOANDIKWA NA MATHAYO , MARKO , LUKA , YOHANE , INJILI ZA SINOPTIKI , HABARI ZA UTOTO WA YESU , NDUGU ZA YESU ,NYARAKA KWA WATU WOTE NA UFUNUO , ZABURI , ---FULL NUKUU---NA PADRE J. BOUQUET DEUS CHAUX . M. Afr.----TANZANIA----( PDF )---CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Monday, May 12, 2025
KITABU 340 : 101 WAYS TO MAKE MONEY IN AFRICA---FULL BOOK---LUCRATIVE BUSINESS IDEAS , INSPIRING SUCCESS STORIES , AND INTERESTING BUSINESS OPPORTUNITIES FOR FORWARD THINKING ENTREPRENEURS----BY JOHN AUL LWUOHA & HARNET BOKREZION PHD-----FIRST EDITION , NOVEMBER , 2014-----CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
MAKALA : UMASKINI UNAUTAKA WEWE MWENYEWE , USILALAMIKIE WATU , NDUGU WALA SERIKALI ? ANZA NA BUKU ( TSHS 1000 ) KUWEKA AKIBA .----------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Kaka, dada, hebu tuambiane ukweli…
Umechoka kuishi kwa mlo mmoja?
Au kila mwisho wa mwezi ni stress tupu?
Mishahara inapita kama upepo.
Biashara haieleweki.
Kuna hela, lakini haikai.
Unafanya kazi kama punda, lakini mfuko ni kama gunia la mbolea mashimo kila kona.
Unajituma, lakini mafanikio yako kama ndoto ya mchana.
Kaka, hiyo siyo laana.
Ni mfumo mbovu wa maisha.
Ni kukosa maarifa sahihi.
Tazama wenzako wanaoanza na elfu moja,
Leo wanamiliki vibanda, magari, hadi mashamba.
Wewe bado unatafuta mtu wa kukukopesha buku la kula.
Ni aibu.
Lakini sio kosa lako kabisa.
Ni kwamba wakati unakuwa uliaminishwa kuwa*Ukiwa na hela nyingi, ndo unaweza kuwekeza.*
Na Wewe Ukaamini.
Ulimwengu unabadilika, lakini mtazamo wako umebaki kuwa ule wa miaka ya 70.
Upo kwenye mduara wa mateso pesa inaingia na kutoka bila faida.
Kila mwezi ni kama kuanza maisha upya.
Mpaka lini?
Watu wengi hudhani kwamba ili uanze kujenga utajiri, lazima uwe na mamilioni.
Hapo ndo tunakosea.
Ukweli ni huu:
Hela kidogo ndiyo mwanzo wa hela nyingi.
Tatizo si kwamba huna pesa.
Tatizo ni kwamba hujui namna ya kukitumia kile kidogo ulichonacho.
Huna mfumo.
Huna maarifa.
Unakula mtaji, unaua ndoto zako.
Usingoje mshahara mwingine ukufikishe kwenye msongo tena.
Usingoje upate milioni ndo uanze.
Anza na hiyo buku YAANI TSHS 1000
Buku yako ya leo inaweza kuwa sababu ya uhuru wako wa kesho.
ENDELEA KUSOMA KILA SIKU " MAISHA NA MAFANIKIO BLOG " UTAJIFUNZA MENGI NA SIRI NYINGI ZA MAISHA NA MENGINEYO DUNIANI --- ONGEA NA KOCHA MWL. JAPHET MASATU-----CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136