KATIKA maisha ya
BINADAMU ya kila
siku kuna MATARAJIO , MIPANGO , KUKATA TAMAA
na KUJIPA MOYO.
WATAALAM WA ELIMU
NAFSI wanayagawa MAISHA
YA BINADAMU katika
hatua TANO kuu
za mabadiliko ya
MTAZAMO na MATARAJIO.
Katika hatua
zote hizo kwa
mfano , kutoka umri
wa miaka 16
hadi 18 , 18
hadi 23 , 23 hadi
28 , na kuendelea , binadamu hubadilika
katika mambo kadhaa ,
hadi anapofikia UMRI
WA UZEE NA
KUFARIKI. Katika hatua
hizi zote TANO , hatua inayotajwa
kuwa na misukosuko
mingi ni ile
ya KATIKATI , ambayo ni
ya umri wa
mika kati ya 38
hadi 45.
Licha ya
kwamba katika umri
huu , na hasa
kuanzia miaka 35
mtu huanza kugundua
kwamba anaelekea UKINGONI
MWA MAISHA YAKE
hapa ndipo anapogundua
UHALISI WA KIFO. Ugunduzi huu
wenye kumfanya ajione
kama mwenye muda
mfupi wa kuishi
humpa shinikizo la
kutaka KUFANYA MAMBO
MENGI KWA WAKATI
MMOJA. Hii ikiwa ni
kutafuta MAFANIKIO katika
shughuli zake za
kufikia lengo fulani
maishani.
MTAALAM MWANASAIKOLOJIA , BWANA DANIEL
LEVINSON anabainisha katika
utafiti aliofanya , kwamba
katika kipindi hiki
Watu hujali , kuzingatia
kujitambulisha na shughuli
zao , mahusiano yao na
wengine na kujali
sana juu yao
wenyewe ( kwa kujiuliza ,
MIMI NI NANI
? NA NIMEFUATA
NINI DUNIANI ? )
Katika kipindi
hiki cha umri
( 38---40 ) , kunakuwa
na WASIWASI KUKOSA
MSIMAMO NA UIMARA.
Utafiti wa
BWANA LEVENSON unaonyesha
kwamba, katika UMRI huu
wa KATI watu
wengi huuona au
kuuhesabu kama “
NAFASI YA MWISHO” , katika kufikia
MALENGO yao. Mara kwa
mara tumewasikia watu
wakisema , “ KAMA MIAKA
AROBAINI HUJATENGENEZA PESA ,
BASI TENA “. Ingawa
ni maneno ya
mzaha , yana ukweli
wa aina fulani
ndani. ASILIMIA 75
ya wale ambao
hushindwa kufikia MALENGO
yao katika kipindi
cha umri huo ( 38---40 ) , huwa
hawayafikii tena.
MAFANIKIO
ambayo tunayazungumzia hapa
ni yale yenye
kuhesabiwa kama ufunguo
kwa maendeleo au
ustawi wa mtu. Kwa
mfano , mtu kuwa
mkuu kazini kwake
kama vile UMENEJA , UHASIBU MKUU, UHARIRI
MKUU , MBUNGE , mtu kuanza kuingiza
pato fulani ambalo
ni kubwa , kupata
UPROFESA , UWAZIRI,
MAFANIKIO KAIKA BIASHARA
na nyingine za
aina hiyo.
Kwa watu
waliofanikiwa kufikia MALENGO
haya , maisha katika umri
huu yanakuwa na
kashkashi ,vurugu zake ,
lakini yenye KUCHUKULIKA
au KUVUMILIKA. Hali ikiwa
na maana kwamba
hata kunapokuwa na
MAFANIKIO , bado umri
huu unabaki kuwa
wenye mashaka. Baadhi ya
waliofanikwa kimapato wanakuwa
bado wanadhani kwamba
, pamoja na MAFANIKIO
hayo , shughuli walizokuwa
au wanazozifanya siyo
kufu yao, siyo stahili
yao.
Lakini kwa
upande mwingine , ni kwamba ,
katika umri huu
watu hujenga MATUMAINI
kwamba huenda maamuzi waliyoyachukua au
wanayoyachukua kimaisha ni
sahihi. Hujawa na
matuymaini ya MAFANIKIO. Kuna kuridhika
kwamba MATUMAINI ya
awali ya MAFANIKIO
Fulani ni jambo
lisilowezekana.
Mara nyingi
inasemwa kwamba katika
umri huu kuna
ugumu wa mtu
kuweza “ KUYARUDISHA
MAJESHI NYUMA“ na
kuanza kuanza MAPAMBANO.
Ndiyo maana mtu
anapoporomoka kimaendeleo kwenye
umri huu , anaweza kufuatiwa
na tabia zenye
kuonyesha KUKATA TAMAA
kama vile ULEVI ,
UZINZI , UTUMIAJI WA MADAWA
YA KULEVYA na
nyingine za aina
hiyo. Kwa wale
ambao wanaweza kujaribu
kuzirekebisha tabia hizo
, inawachukua zaidi
ya miaka 10
kumudu kufanya hivyo.
Ni wazi
umeshashuhudia watu wengi
wa umri huu ,
ambao baada kuona
kwamba WAMESHINDWA KUFIKIA
MALENGO , huwa wanatumia
maneno kama , “ YA
NINI KUHANGAIKA SAA
HIZI , TUNATAFUTA KULA YETU
TU BASI…….” Hii
ikionyesha kwamba wanaamini
kuwa baada ya
umri huo endapo
mtu HAKUFANIKIWA , ni
vigumu kwa mtu
huyo kuweza KUFANIKIWA
MAISHANI mwake. Pia
huonyesha ni jinsi
gani katika umri
huu mtu huwa
ANAUONA UHALISI WA
KIFO.
ANGALIZO: Jamii yetu
mara nyingi hufikiri
ya kwamba UMRI
sahihi wa kupata “ MAFANIKIO” au “
KUUKATA” kama Waswahili
wanavyosema ni kati
ya 24 na
40 na unapofikisha
UMRI wa miaka
50 MAFANIKIO ndio
basi tena , Kwaheri. ‘SI KWELI
KABISA NDUGU YANGU “
TAMBUA UKWELI
HUU : MAFANIKIO
yanawezekana katika UMRI
wowote. UMRI si
kitu bali ni
numba tu ndugu
yangu usikate tamaa !
NI DHAMBI KUBWA SANA
MACHONI MWA MUNGU. Cha
msingi unatakiwa uwe
na FIKRA SAHIHI ( right attitude /
positive attitude ) na
siyo FIKRA MBOVU ( negative attitude ).
MFANO: Mark Zuckerberg alianzisha
mtandao wa FACEBOOK
mwaka 2004 akiwa
na umri wa miaka 19
tu. Ameleta mapinduzi makubwa
katika mawasiliano kimtandao.Na
sasa ni tajiri
mkubwa .
Baraka Obama
raisi wa 44
wa MAREKANI , kabla
ya kuwa raisi
alikuwa ni mwandishi. Alipokuwa na
umri wa miaka 43
aliandika KITABU , “
DREAMS FROM MY
FATHER “. Kitabu hiki
kilipendwa sana nchini
MAREKANI , kilimpatia mamilioni ya
shilingi na kuwa
tajiri mkubwa.
Nelson
Mandela baada ya
kutumikia kifungo kwa
miaka 27 katika
gereza lililokuwepo katika
kisiwa cha ROBBEN ,
CAPE TOWN baadaye alitoka
kifungoni na kuwa raisi
wa AFRICA KUSINI ,
akiwa na umri
wa miaka 76.
Namnukuu mchezaji
maarufu wa mpira
wa miguu wa Ghana
ABEDI AYEW PELE ,
“ SUCCESS IS
NOT AN ACCIDENT. IT
IS HARD WORK , PERSEVERANCE ,LEARNING ,, STUDYING ,
SACRIFICE AND MOST
OF ALL , LOVE OF
WHAT YOU ARE
DOING OR LEARNING
TO DO.” (
Mafanikio siyo ajali. Ni
kufanya kazi kwa
bidii , kuwa mvumilivu , kujifunza
, kujitoa kikweli na
kubwa zaidi penda
unachofanya au unachojifunza ).
Asante mdau
wangu kwa kusoma
makala hii nzuri
, usisahau kumshirikisha
mwenzako na endelea
kusoma kila siku
ili ujifunze katika
blogu yako hii
ya kipekee.
Mwandishi wa makala hii
ni MWL. JAPHET
MASATU , ni mwanafunzi wa
CHUO KIKUU HURIA
TANZANIA , KINONDONI REGIONAL
CENTRE ,(2015) anapatikana kwa
: Call / WhatsApp
+ 255 755 400 128 / + 255
716 924 136. EMAIL: japhetmasatu@yahoo.com.