KUMBI ZA STAREHE/SHEREHE/HARUSI/MIKUTANO
Biashara ya
ukumbi wa starehe /sherehe/ harusi/mikutano
ni biashara nzuri
kwani kutokana na
maendeleo ya sayansi
na teknolojia, mahitaji ya
kumbi za starehe /sherehe/starehe /mikutano
yameongezeka sana. Biashara
hii inahitaji mtaji
mkubwa kuifanya na
ubunifu ili kufanikiwa. Ili ukumbi
uweze kuvutia wateja
unatakiwa uwe na
nafasi kubwa yenye
sakafu , kuta zipigwe rangi, upambwe kwa
maua, uwe na
kaunta ya vinywaji
na ikibidi uwe
na huduma za
vinywaji, uwe unaingiza hewa
safi , uwe na mapanga boi
au kiyoyozi na
pia uwe na
vivutio vingine kama
michezo ya “darts”
“pool table” uwe
na luninga , muziki wa
disko na uwe
na huduma ya
vitafunio na vyakula. Ukumbi unapaswa
kutangazwa ili ufahamike. Vile vile
mmiliki wa ukumbi
unaweza kuingia mkataba
na bendi za
muziki au vikundi
vya sanaa viweze
kufanya maonyesho na
kuvutia wateja. Ukumbi unaweza
kuendesha matamasha ya
burudani kuanzisha kikundi
cha sanaa au bendi ya
muziki kufanya maonyesho
ili kuvutia wateja.
Mapato ya ukumbi
hupatikana kutokana na
viingilio vinavyolipwa mlangoni
kuingia ukumbini na
kuingia mikataba na
bendi za muziki
au vikundi vya
sanaa kufanya maonyesho
ukumbini.
Matatizo ya
biashara hii ni
kushindwa kudhibiti mapato
kwa watu kuingia
ukumbini lakini mapato
yote hayawasilishwi kwa
mmiliki wa ukumbi , kukosekana kwa
wateja kama ukumbi
hauvutii , uchafu kwenye ukumbi
na vyooni ,
uchakavu wa ukumbi
na kukosekana ubunifu
toka kwa mmiliki
wa ukumbi.Ili kukabiliana
na matatizo haya
mmiliki wa ukumbi
anatakiwa kuwa mbunifu
na azingatie mambo niliyoeleza
hapo mwanzoni kuhusu
uendeshaji wa biashara hii, awape
motisha wafanyakazi wake
ili wamfanyie kazi
yake vizuri.Pia aweke
sanduku la Maoni
kupata maoni ya
wateja na autangaze
ukumbi wake na
kuingia mikataba na
vikundi vya muziki na
sanaa.