Monday, May 12, 2025

MAKALA : UMASKINI UNAUTAKA WEWE MWENYEWE , USILALAMIKIE WATU , NDUGU WALA SERIKALI ? ANZA NA BUKU ( TSHS 1000 ) KUWEKA AKIBA .----------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

 

Kaka, dada, hebu tuambiane ukweli…

‎Umechoka kuishi kwa mlo mmoja?

‎Au kila mwisho wa mwezi ni stress tupu?

‎Mishahara inapita kama upepo.

‎Biashara haieleweki.

‎Kuna hela, lakini haikai.

‎Unafanya kazi kama punda, lakini mfuko ni kama gunia la mbolea mashimo kila kona.

‎Unajituma, lakini mafanikio yako kama ndoto ya mchana.

‎Kaka, hiyo siyo laana.

‎Ni mfumo mbovu wa maisha.

‎Ni kukosa maarifa sahihi.

‎Tazama wenzako wanaoanza na elfu moja,

‎Leo wanamiliki vibanda, magari, hadi mashamba.

‎Wewe bado unatafuta mtu wa kukukopesha buku la kula.

‎Ni aibu.

‎Lakini sio kosa lako kabisa.

‎Ni kwamba wakati unakuwa uliaminishwa kuwa*Ukiwa na hela nyingi, ndo unaweza kuwekeza.*

‎Na Wewe Ukaamini.

‎Ulimwengu unabadilika, lakini mtazamo wako umebaki kuwa ule wa miaka ya 70.

‎Upo kwenye mduara wa mateso pesa inaingia na kutoka bila faida.

‎Kila mwezi ni kama kuanza maisha upya.

‎Mpaka lini?

‎Watu wengi hudhani kwamba ili uanze kujenga utajiri, lazima uwe na mamilioni.

‎Hapo ndo tunakosea.

‎Ukweli ni huu:

‎Hela kidogo ndiyo mwanzo wa hela nyingi.

‎Tatizo si kwamba huna pesa.

‎Tatizo ni kwamba hujui namna ya kukitumia kile kidogo ulichonacho.

‎Huna mfumo.

‎Huna maarifa.

‎Unakula mtaji, unaua ndoto zako.

Usingoje mshahara mwingine ukufikishe kwenye msongo tena.

‎Usingoje upate milioni ndo uanze.

‎Anza na hiyo buku  YAANI  TSHS  1000

‎Buku yako ya leo inaweza kuwa sababu ya uhuru wako wa kesho.

 ENDELEA  KUSOMA    KILA     SIKU   "  MAISHA     NA  MAFANIKIO  BLOG "  UTAJIFUNZA  MENGI  NA  SIRI    NYINGI  ZA  MAISHA   NA  MENGINEYO  DUNIANI  --- ONGEA  NA   KOCHA    MWL.  JAPHET  MASATU-----CALL  /  SMS   /  WHATSAPP  +  255  716  924 136