Thursday, April 22, 2021

FALSAFA : SOMA VITABU , JUA FALSAFA ILA WEKEZA NGUVU NYINGI KUISHI KILE ULICHOSOMA.

Soma Vitabu, Jua Falsafa Ila Wekeza Nguvu Nyingi Kuishi Kile Ulichosoma

UNASUMBUKA NA UFANISI KAZINI ??

Leo nimeamua nikusogezee mada hii kwenye macho yako kwani imekuwa changamoto na kuathiri utendaji kazi wa watu wengi.

 Ukweli ni kwamba akili zetu sisi binadamu ni kitu cha ajabu sana, ni kitu ambacho kina nguvu ya kufanya makubwa kuliko tunavyoweza kutegemea.

Lakini cha kushangaza ni kwamba, mtu anaweza kuitawala akili yake akafanya makubwa, au akatawaliwa na akili yake na kuwa mtumwa maisha yake yote.

kuhusu ubongo wa binadamu ni kwamba una nguvu za ajabu lakini watu wengi hutumia sehemu ndogo sana ya nguvu hiyo.

Asilimia kubwa ya watu huishia kufanya mambo ya kawaida, hivyo hupata matokeo kawaida na kuishi maisha ya kawaida (routine life).

Lakini kundi lingine ni watu ambao ni asilimia ndogo ambao hufikia viwango vya juu vya ufanisi/ nguvu za ubongo wao.

Kundi hili hufanya mambo makubwa na huwa na maisha tofauti na kundi la kwanza.

Tofauti ipo kwenye namna tunavyotumia bongo zetu, uamuzi upo mikononi mwako.

Ujenge au ubomoe.

Uzuri mpaka hapa umeshajua upo kundi gani.

Kama tayari tuendelee…

Ubongo wetu unaweza kutunza taarifa  mbalimbali kwa muda,  ambazo baadae huenda kwenye subconscious mind.

Ili taarifa zivuke kwenye subconscious mind, hupita kwenye mfumo RAS ( Recuticular Activating System) ambapo taarifa huchujwa.

Ili kundi lingine huruhusu vitu vya kimazingira kuingia ambavyo huathiri maamuzi na kisha utendaji.

Kwa bahati mbaya huwezi kufikia viwango vya juu vya ufanisi ikiwa muda mwingi umezungukwa na usumbufu.

Hivyo unapaswa uwe na ufahamu juu ya vitu gani vinavyokuletea usumbufu na kuweza kuvidhibiti mara moja.

Kuna maelfu ya watu walipitia hali kama hii na wakafanikiwa kutoka mimi ni miongoni mwao, hata wewe leo hii unaweza kutoka kwenye hali hii.

Friday, April 16, 2021

USHAURI : KAMA HUWEZI KUFANYA KITU HIKI , FUNGA BIASHARA YAKO MARA MOJA.

Karibu rafiki yangu mpendwa kwenye makala yetu ya ushauri wa changamoto mbalimbali zinazokuwa kikwazo kwa mafanikio yetu.

Kwenye makala ya leo tunakwenda kushauriana kwenye msimamo muhimu mno unaouwezesha biashara kufanikiwa au kufa. Msimamo huo ni misingi ambayo biashara inafuata bila ya kuivunja.

Kila biashara inapaswa kuwa na misingi au miiko yake, ambayo walio ndani na nje ya biashara wanapaswa kuifuata bila ya kuivunja. Walio ndani ya biashara ni wamiliki na wafanyakazi na walio nje ni wateja na wadau mbalimbali wa biashara.




Pale mtu yeyote anapovunja misingi muhimu ambayo biashara hiyo imejengwa basi anapaswa kuondolewa kwenye biashara hiyo. Kwa sababu kama anayevunja misingi ataendelea kuachwa kwenye biashara, biashara hiyo itakuwa dhaifu na kufa.

Hapa ndipo changamoto za biashara nyingi zinapoanzia, watu wanavunja misingi na miiko ya biashara, lakini bado wanaachwa kwenye biashara. Wanaachwa kwa sababu mmiliki wa biashara anaona biashara yake haiwezi kwenda kama atawaondoa watu hao.

Na hapa ndipo ninapokupa kauli hii moja muhimu unayopaswa kuitafakari kila wakati; kama umeanzisha biashara yako binafsi na unashindwa kumfukuza mtu aliyendani (mfanyakazi au mbia) au nje (mteja au mdau) ya biashara basi funga biashara hiyo mara moja. Ifunge kwa sababu unachofanya ni kupoteza muda tu, kama biashara hiyo haina cha kusimamia itaangushwa na chochote.

Kama biashara haiwezi kwenda bila kuwategemea wasioheshimu misingi na miiko ya biashara hiyo, hapo huna biashara, ni swala la muda tu kabla haijafa kabisa.

Kwenye riwaya ya Fountainhead iliyoandikwa na Ayn Rand ambapo Howard Roark anapambana na wajamaa wanaotaka kutumia kipaji chake na kumdhibiti watakavyo, kuna kisa kimoja kinaeleza vyema hili ninaloshauri hapa. Gail Wynand mmoja kati ya wachache waliokuwa wanamuunga mkono Howard alikuwa anamiliki magazeti yenye ushawishi mkubwa. Ellsworth Toohey aliyekuwa anampinga sana Howard alikuwa mmoja wa waandishi na wahariri wa magazeti hayo. Toohey alipanga kuyatumia magazeti ya Wynand kumchafua Howard, kitu ambacho Wynand alikikataa.

Hivyo Toohey alitumia ujanja, wakati ambapo Wynand hayupo, aliajiri wafanyakazi wengi wanaokubaliana na wewe, akashawishi bodi ya wakurugenzi iwe upande wake na hapo akawa amepata udhibiti mkubwa wa magazeti hayo.

Baada ya kujihakikishia udhibiti wa magazeti, alianza kumchafua Howard kupitia magazeti hayo. Wynand aliporudi hakupendezwa na hilo, alimuita Toohey ofisini kwake na hapo Toohey akamwambia wazi kwamba kwa sasa yeye ndiye mwenye udhibiti wa magazeti hayo na hawezi kumfukuza. Wynand alimjibu kwa ufupi; siku ambayo nitashindwa kumfukuza mfanyakazi niliyemuajiri kwenye biashara yangu, ndiyo siku nitakayoifunga hiyo biashara kabisa. Na kweli ilimbidi Wynand kufunga magazeti yake maana Toohey alikuwa ameshakita mizizi.

Kuna mengi sana ya kujifunza kwenye kisa hicho na ushauri huu kwa ujumla. Lazima biashara iwe na misimamo na miiko na yeyote anayeivunja hapaswi kuachwa. Na kama kuondolewa kwake hakuwezekani, basi bora biashara ifungwe.

Kingine muhimu cha kujifunza ni umuhimu wa biashara kuendeshwa kwa mfumo ambapo hakuna mtu mmoja ambaye asipokuwepo basi biashara inakuwa imekufa. Hata wewe mmiliki wa biashara, lazima biashara iweze kwenda bila uwepo wako, la sivyo huna biashara.

Hatua za kuchukua hapa ni kujenga mfumo imara wa biashara yako ambao una misingi, miiko na miongozo ya jinsi ya kuendesha biashara hiyo. Kila anayehusika kwenye biashara anapaswa kuuelewa vizuri mfumo huo na kuufuata. Na pale inapotokea mtu anakwenda kinyume na mfumo basi anapaswa kuondolewa mara moja. Na kama unaona huwezi kumwondoa kwa kuwa biashara haiwezi kwenda, basi bora ufunge biashara moja kwa moja.

JIUNGE   leo  DARASA  ONLINE " ili uweze  KUJIFUNZA   MISINGI  NA  MIIKO   YA  BIASHARA   kujenga biashara imara na isiyotikiswa na kitu chochote. Wasiliana  NAMI   KOCHA   MWL.  JAPHET  MASATU (  WhatsApp + 255 716924136  ) NIKUUNGE   LEO.

Makala hii imeandikwa na Kocha Mwl  Japhet   Masatu  ambaye ni MWALIMU   KITAALUMA, kocha wa mafanikio, mwandiashi na mjasiriamali. 

 

KAMA UNATAKA KUVUNJA TABIA FULANI AU URAIBU , USIJIRUHUSU KUWA KWENYE HALI HII YA KUFANYA KWA MAZOEA.

Siku moja mwandishi wa vitabu Tom Corley alifanya utafiti wa tabia za kila siku za matajiri 233 na pia akachunguza tabia za kila siku za watu maskini wapatao 128.

Alichogundua ni kuwa kulikuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya tabia za maskini na matajiri.  

Katika kipindi cha utafiti wake aligundua kuna karibu mambo 300 ambayo hutofautisha wanaofanikiwa na wale ambao hawafanikiwi maishani.

Mara nyingi ni rahisi sana kufikiri kuwa tofauti ya waliofanikiwa na wasiofanikiwa hutokana na mambo makubwa sana yanayotutofautisha.

Ukweli ni kwamba tabia ina nguvu kubwa ya kuamua hatima yako ufanikiwe au ufeli.

Tabia za kitajiri ni ngumu kuzijenga na ni rahisi kuzivunja, upande wa pili ni kinyume chake tabia za kimaskini  ni rahisi kuzijenga na ni ngumu kuziacha.  

Na hii ni kwa sababu Ujengaji wa tabia huwa unaanzia kwenye akili zetu, hivyo hata kuzivunja lazima kuanzie kwenye akili zetu pia.

Huwa tunaijenga tabia kwa kutumia nguvu ya kufikiri lakini tabia ikishajijenga huwa tunaitekeleza bila hata ya kufikiri(mindless).

Chukua mfano mdogo wakati unajifunza kuendesha baiskeli au gari.

Mwanzoni ulikuwa unafikiria kila unachofanya , hukuweza hata kuongea na mtu wakati unaendesha, maana kila wakati ulikuwa unafikiri kuchochea au kukanyaga mafuta, breki na kubadili gia.

Lakini baada ya kuwa dereva mzoefu, unajikuta unaendesha bila hata ya kufikiria , tena unaweza kuendesha huku ukiwa unaongea na wengine.

Mfano huo unatuonesha jinsi akili zetu zinavyojenga tabia , mwanzo tunatumia nguvu na umakini mkubwa kwenye kufikiri lakini baadaye tunaifanya bila hata ya kufikiri.

Ni hiyo hali ya kufanya bila ya kufikiri ndiyo inayojenga na kufanya uraibu uwe mgumu kuvunja.

Wengi wenye uraibu huwa wanajikuta wameshafanya kile walichozoea bila hata ya kufikiri.

Kwenye teknolojia na mitandao ya kijamii ndivyo pia uraibu unajengeka.

Awali wakati unaanza kujifunza kutumia simu janja au mitandao ya kijamii ulikuwa unatumia nguvu na kufikiri.

 Ila baadae inakuwa rahisi kwako , unajikuta umeshika simu na uko kwenye mitandao ya kijamii bila hata ya kufikiria.

Ili tuweze kuvunja uraibu huu na wa aina nyingine , tunapaswa kutumia akili zetu vizuri, kama zilivyotuwezesha kujenga tabia, hivyo pia zitatuwezesha kuvunja tabia na uraibu.

Kama unataka kuvunja tabia za kimaskini ambazo zinakupotezea muda na zina kurudisha nyuma na huzipendi, huna budi kutumia uwepo wa akili (mindful) , mbinu hii itakusaidia sana kuvunja tabia nyingi mbaya.

Hii ni mbinu ambayo imenisaidia mimi na maelfu ya watu

KARIBU  UJIUNGE   DARASA  ONLINE   UJIFUNZE ZAIDI

 WASILIANA  NAMI--KOCHA  MWL.  JAPHET   MASATU

WhatsApp + 255 716924136  /   + 255 755  400  128