Saturday, September 28, 2019

KOSA KUBWA UNALOFANYA KWENYE MSHAHARA WAKO UNAOPOKEA KILA MWEZI

Kwa mshahara au kipato chochote unachopokea, iwe ni malipo ya kazi zako binafsi au faida unayotengeneza kwenye biashara, kuna kosa moja kubwa umekuwa unalifanya. Kosa hilo ni KUMLIPA KILA MTU NA KUJISAHAU WEWE MWENYEWE.

Hebu fikiria unapopata fedha unaanza na nini? Kulipa madeni, kulipa bili, kununua vyakula, kununua nguo, kulipia starehe na mapumziko mbalimbali. Baada ya siku chache za kupata fedha unakuwa umeimaliza yote, huku wewe ukibaki mtupu kabisa.
Sasa rafiki, jua kwamba huwezi kuwa huru kifedha kama utaendekeza utaratibu huo wa kuwalipa wengine na kujisahau wewe mwenyewe. Kwenye kila kipato unachoingiza, mtu wa kwanza kumlipa unapaswa kuwa wewe.

Monday, September 23, 2019

UWEZO WA KUJUA KAMA TUTAKUFA MASKINI TUNAO ----------NA MUNGA TEHENAN

TUNA UWEZO MKUBWA TUNAOSHINDWA KUUTUMIA-----------NA MUNGA TEHENAN

PIGA HATUA MOJA KWA WAKATI---ISHI KWA MUJIBU WA KANUNI YA MAFANIKIO----------NA DR. KAZUO INAMORI

MAZUNGUMZO NA DR . KAZUO INAMORI KUHUSU KANUNI YA USHINDI

A Simple System To Transform Any Business From A Cash-Eating Monster To A Money-Making Machine

MSHAHARA NI MADAWA YA KULEVYA , JIFUNZE JINSI YA KUEPUKANA NA MADHARA YAKE


Nassim Taleb anatuambia kuna vitu vitatu vyenye uraibu mbaya, madawa ya kulevya(unga), vyakula vya wanga (sukari) na mshahara wa kila mwezi. 

Ukishauzoea mshahara, ni vigumu sana kuweza kufanya kitu kikubwa kwenye maisha yako. Kwa sababu maisha yako yanakuwa ya mipango ya mwisho wa mwezi tu. Kwamba mwisho wa mwezi huu nitafanya hiki au kile.
Mshahara ukitoka unakuwa na mipangilio mingi kuliko kiwango chake, hivyo ndani ya siku mbili unakuwa umeisha. Na hapo unafanya nini? Unajua vyema, unaanza kukopa kwa sababu unajua mshahara ujao utalipa. Na hapo ndipo uraibu unapojenga mizizi.
Kuondokana na uraibu huu wa mshahara, lazima uanze kujijengea msingi wa kipato nje ya mshahara. 

 TEMBELEA BLOGS   ZA   MWL.   JAPHET   MASATU , JIFUNZE   ,  JIUNGE   NA   DARASA  LA   MAFUNZO  KILA   SIKU   NA  UCHUKUE HATUA , MAISHA   NA  WEWE !



Tuwasiliane  kwa  Call / Message /  ( WhatsApp + 255716924136 )/   + 255 755 400128  /   +255 688 361 539