Saturday, September 14, 2019

KWA NINI BAADHI YA BINADAMU NI WABUNIFU NA WENGINE SI WABUNIFU ? -------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

TUWE WABUNIFU KWA KIWANGO GANI ? -------------------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "

VIRUTUBISHO 04 VINAVYOHITAJIKA KWENYE UBUNIFU -------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

KWA NINI WASTAAFU WENGI HUFELI KWENYE BIASHARA ? JINSI YA KUFANYA BIASHARA BAADA YA KUSTAAFU.---------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

KUACHA WOSIA NA MIPANGO YA MALI ZAKO BAADA YA KIFO CHAKO -----------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

Friday, September 13, 2019

MIPANGO YA MAISHA INAPASWA KUJA KABLA YA MIPANGO YA BIASHARA.

Ni rahisi sana kuweka malengo na mipango mikubwa ya kibiashara, lakini unapokaa na kujiuliza kwa nini unataka kufikia malengo hayo makubwa unakosa jibu la uhakika.

Watu wengi wamekuwa wanapotea kwenye biashara kwa sababu wanaweka malengo ya biashara kabla hawajaweka malengo ya maisha. Wanataka kuwa mabilionea kupitia biashara zao, na hilo linawataka kuweka maisha yao yote kwenye biashara na kusahau vitu vingine vyote. Wanaweza kufikia lengo hilo, lakini maeneo mengine ya maisha yao kama afya na mahusiano yanakuwa yameathirika sana.

Kabla hujaweka lengo kubwa la biashara, anza kwanza na lengo kuu la maisha yako. Jua unataka kuwa na maisha ya aina gani, jua maisha ya mafanikio kwa upande wako yana maana gani.

Ukishajua kwamba unataka nini kwenye maisha yako, hapo sasa unaweza kuitumia biashara yako kuwa na maisha unayoyataka wewe. Lakini ukianza kufikiria unachotaka kwenye biashara pekee, utaishia kuwa na maisha mabovu sana.