Monday, September 2, 2019

HATUA 05 ZA KUCHUKUA ILI KUTOKA KWENYE AJIRA MPAKA KUJIAJIRI ----------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "

MAMBO 20 YA KUFANYIA KAZI ILI KUTOKA KWENYE AJIRA NA MADENI NA KWENDA KUJIAJRI NA KUWA NA UHURU WA KIFEDHA--------------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "

UNAPOJIAJRI , UNAPASWA KUFIKIRI TOFAUTI NA WALE WALIOAJIRIWA.

Unapojiajiri, unapaswa kufikiri tofauti kabisa na wale walioajiriwa. Kwa sababu kuna vitu ambavyo watu walioajiriwa hawajisumbui navyo sana, kwa sababu wameahidiwa vinafanyiwa kazi, mfano bima ya afya, mafao ya uzeeni na mengineyo. Unapoachana na ajira na kuamua kujiajiri moja kwa moja, mambo hayo utapaswa kuyahangaikia mwenyewe, lazima utafute bima yako na familia yako na pia lazima uwekeze ili kujiandaa kwa siku zijazo. Kwa sababu hakuna anayekuandalia mafao, unapaswa kutengeneza uwekezaji wako mwenyewe, ambao miaka mingi ijayo utaweza kukuingizia wewe kipato hata kama hufanyi kazi moja kwa moja.