( 1 ). kuandika kuhusu kazi au biashara yako. Hapa unaandika nakala za mauzo,
zinazowavutia watu kwenye kazi au biashara unayofanya na kuwashawishi
kuja kununua kile unachotoa. Kadiri unavyoweza kandika vizuri, ndivyo
unavyoweza kuwavutia wengi na kuuza zaidi.
( 2 ). kuwaandikia wengine. Popote pale ulipo, kuna watu wana bidhaa au huduma
nzuri sana, zinazoweza kuwasaidia wengine kupiga hatua zaidi kwenye
maisha yao, lakini hawajaweza kuwafikia watu wengi. Hapo kuna fursa ya
wewe kuijua vizuri bidhaa au huduma hiyo, kisha kuandika nakala za mauzo
na kila anayenunua bidhaa au huduma kupitia nakala zako, basi mtu huyo
anakupa wewe kamisheni. Angalia ni bidhaa au huduma zipi unaweza
kuzifanyia hivyo, ingia makubaliano na wahusika na anza kuandika nakala
za mauzo.
( 3 ). kuwa mwandishi na kuuza kazi zako za uandishi. Unaweza kuwa mwandishi
kwenye eneo lolote unalochagua, na kwa kujifunza njia bora za uandishi
wenye ushawishi, ukaweza kuwavutia watu kusoma kazi zako na hata
kuzinunua pia. Hapa unaweza kuwa na vitabu, kozi au huduma nyingine kama
za ushauri ambapo utawavutia watu kuzipata kupitia uandishi wenye
ushawishi.
Rafiki,
hapo ulipo sasa, unaweza kutumia uandishi wa nakala za mauzo kama
sehemu ya kuingiza kipato cha pembeni. Jifunze na kuwa mwandishi bora,
andika sana na kuwa na mpango bora wa kutengeneza kipato kupitia
uandishi wako.