“There
is virtually no other skill that can make you as much money as
copywriting. Nearly all internet millionaires know this secret: more
than their product, more than their traffic generation techniques, more
than their email campaigns, more than who their joint-venture partners
might be, it’s their copywriting that has made them rich.” – Ray
Edwards.
Upo
ujuzi mmoja ambao umezalisha mamilionea wengi dunia kuliko ujuzi
mwingine wowote ule. Ujuzi huo ni uandishi wa nakala za mauzo
(copywriting). Kama umewahi kuona tangazo la bidhaa kwenye tv, redio au
gazeti na likaingia kwenye fikra zako kiasi cha kuwa unafikiria tangazo
hilo muda mwingi basi jua kuna watu walikaa chini na kuandika tangazo
hilo, ili kukulenga wewe.
Kama
umewahi kusoma maelezo ya kitu fulani na ukatoka ukiwa na hamasa na
kuchukua hatua mara moja, basi jua hapo kuna watu wamekaa chini kaundika
kitu kinachokulenga wewe, wakiwa wana hatua ambayo wanataka wewe
uchukue.
Uandishi
wa nakala za mauzo, ni moja ya ujuzi ambao unalipa zaidi duniani, hasa
pale mtu anapoweza kufanya kwa ubora wa hali ya juu. Jifunze uandishi
wenye ushawishi kama tulivyojifunza kwenye kitabu cha juma hili na
utaweza kuongeza kipato chako maradufu.