1. Kuna
mfumo wa kufikiri ambao kutoka ndani yake vitu vyote vinatengenezwa na
ambao kwa uhalisia wake unaruhusu, kupenyeza na kuujaza ulimwengu wote.
2. Fikra kwenye mfumo huu inazalisha ile taswira inayotengenezwa na fikra.
3. Mtu anaweza kutengeneza vitu kwenye fikra zake na kwa kuziweka kwenye mfumo huu wa kufikiri kile anachofikiri kinaumbwa.
4. Ili kufanya hivi, mtu anapaswa kuondoka kwenye fikra za ushindani na kwenda kwenye fikra za ubunifu. Vinginevyo hataweza kuendana na mfumo wa fikra ambao mara zote upo kwenye hali ya ubunifu na siyo ushindani.
5. Mtu yeyote anaweza kuendana na mfumo huu wa fikra kwa kuwa mtu wa shukrani kwa baraka ambazo amezipata. Shukrani inaunganisha fikra za mtu na mfumo wa fikra unaoendesha ulimwengu.
6. Mtu
lazima atengeneze picha ya kifikra ya vitu anataka kuwa navyo na
kuifikiria picha hii mara zote huku akiwa na imani kwamba ataipata na
kushukuru kwamba mfumo wa fikra unamwandalia mazingira ya kupata kile
anachotaka. Tumia
muda wako wa mapumziko kufikiria picha ya utajiri unaotaka kuwa nao na
mfumo wa fikra utaipanga dunia kwa namna ambayo itakuletea kile
unachotaka.
7. Mfumo wa kufikiri unafanya kazi kupitia njia za asili za ukuaji na za kijamii. Kila ambacho kinafikiriwa kwa muda mrefu kwa imani na bila ya shaka, ndiyo kinacholetwa kwenye uhalisia.
8. Ili kupokea kile ambacho mtu anataka, lazima mtu achukue hatua kwa namna fulani ambayo inamwezesha kujaza pale alipo sasa. Lazima
afanye zaidi, lazima atoe thamani kubwa kwa wengine kuliko thamani
anayopokea na lazima akue zaidi na akuze zaidi kile anachofanya.