1.
USAFIRI.
Moja
ya biashara ambayo inaaminika hasa kwa bara la afrika ikiwa utaifanya kwa
utulivu na ukafata misingi yake ni biashara ya usafiri. Hapa unaweza ukawa na
kampuni yako ya kusafirishia abiria kutoka sehemu moja na kwenda nyingine.
Kwa
sasa hitaji la usafiri bado ni kubwa, kama si mjini hata kijijini. Watu wanataka
kusafiri kila siku na kwa bahati mbaya wengi hawana uwezo huo wa kumiliki
vyombo vya usafiri. Hii ni mojawapo ya biashara ya kuifikiria kuifanya kama
unaweza, kwani itakupa mafanikio sana.
2.
AFYA.
Kama
pia utajikita na kufanya biashara inayohususha mambo ya afya, basi upo
uwezekano mkubwa zaidi wa wewe kufanikiwa sana. Huduma za afya katika maeneo
mengi bado hazijafikiwa kisawasawa na zinahitajika kweli.
Hivyo
kwa kufanya biashara hii, kama ukifungua hospitali au zahati au duka la dawa, utapata
pesa na hapo pia utakuwa imeisaidia jamii. Kikubwa kubali kuzunguka kuangalia
ni wapi ambapo ukifanya huduma au biashara hii wewe itakulipa.
3.
CHAKULA.
Hakuna
mtu asiyekula, hiyo ikiwa na maana ukianzisha biashara ya vyakula na ukaifanya
kwa ufanisi mkubwa utafanikiwa. Hapa unaweza ukauza chakula, lakini si maanishi
uje na picha ile ya mama ntilie ‘pasee.’
Ukiamua
kuja na biashara ya kuuza chakula ifanye kwa ukisasa zaidi. Zipo sehemu bado nyingi
zinazohitaji huduma hii ya chakula safi, mazingira safi, lakini hawaipati kwa
uhakika kwahiyo unatakiwa ujue jinsi ya kuanza ili uanze kupiga pesa.
4. VIWANDA VIDOGO VIDOGO.
Huwezi
kuendelelea sana kama utaendelea kuwa mlanguzi
wa biashara za watu wengine. Changamsha akili na anza mchakato wa kuweka viwanda
vidogo vidogo ambavyo vitasaidia wewe kuweza kukupa kipato kikubwa.
Uzuri
wakuwa na kiwanda kidogo wewe ndio unakuwa mzalishaji wa kwanza kwa hiyo ni
lazima utapata faida kubwa sana. Hapa unaweza ukatengeneza kiwanda chako cha
kutengeneza juisi au unga wa sembe na lishe, uamuzi ni wako.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Friday, November 30, 2018
Thursday, November 22, 2018
KILA MTU NA HAMSINI ZAKE. HAKUNA ANAYEJALI SANA MAISHA YA WENGINE.
Maisha
ya sasa hivi naweza kusema yamekuwa ni kama ya kuishi kisiwani, watu wamekuwa
hawajali sana watu wengine kwa kiasi kikubwa, ukilinganisha na zamani. Kwa sasa
ukipata changamoto kubwa wewe jua hiyo ni changamoto yako tu, inabidi ukomae
nayo hadi utoke.
Kutokana na hili kuendelea kudumu kunafanya maisha yanazidi kuendelea kuwa magumu sana hadi watu wanakosa msaada ambao ungeweza kuwasaidia. Ubinafsi ambao wengi wanao imekuwa ni kichocheo kikubwa sana cha ugumu wa maisha.

KUTEGEMEA CHANZO KIMOJA CHA MAPATO , HUPELEKEA MAISHA KUWA MAGUMU SANA !
Kutokana
na maisha kubadilika na gharama za maisha kupanda karibu kila siku, suala la kutegemea
kipato kimoja, ni moja ya chanzo cha maisha kuwa magumu. Watu wengi wanategemea
kipato kimoja, zaidi kwa wengi ikiwa ni ajira.
Kwa bahati mbaya kipato kimoja hakiwezi kukidhi mahitaji yote hata iweje. Sasa kwa sababu hiyo ya maisha kupanda mara kwa mara, ni lazima tu ugumu wa maisha uonekane. Hata siku moja usitegemee maisha yako yakawa rahisi kama bado una kipato kimoja.

Saturday, November 17, 2018
TABIA YA FEDHA. FEDHA NI ZAO LA HAMASA.
FEDHA ni kama
mchumba mwenye wivu, mchumba ambaye anataka muda wote uwe naye, muda
wote umfikirie yeye tu. Na mchumba huyu akigundua humfikirii na kumjali
yeye anaondoka na kwenda kutafuta wengine wanaomjali na kumfikiria.
Hivi ndivyo fedha zilivyo, kama huna muda nazo hazitakuwa na muda na wewe. kama huzijali na kuzifikiria muda wote zitaenda kwa wale wanaojali na kuzifikiria.
Fedha ni zao la hamasa, chochote ambacho kinakuhamasisha, kile unachopenda kweli, kila ambacho unakifanya muda wote bila ya kuchoka, ndiyo kitu kitakachokuletea kipato kikubwa sana.
Hivyo rafiki, unapofikiria kuhusu fedha, anza kufikiria nini kinakupa hamasa sana, nini unapenda kufanya sasa kisha weka maisha yako yote kwenye kufanya hicho, na fedha hazitakuwa tatizo kubwa kwako.
Tatizo kubwa kwenye hili ni watu huwa wanakosa uvumilivu, wakiona kile wanachofanya kinachelewa kuwaletea matokeo wanayopata, na kuona wengine wakifurahia matunda ya vile wanavyofanya, wanajidanganya kule ndiyo kwenye fedha, wanaacha wanachofanya na kwenda kufanya vitu vingine. Wanahangaika sana, na hawapati fedha walizofikiria kupata. Na hata wakizipata, bado maisha yao yanakuwa na utupu fulani, kwa sababu kile wanachofanya siyo kinachowahamasisha zaidi.

Friday, November 16, 2018
HUDHURIA SEMINA AU WARSHA MBALIMBALI ZA KIBIASHARA UJIFUNZE MBINU MPYA ZA KIMAUZO. DUNIA INABADILIKA KILA SIKU. ACHANA NA MBINU ZA KIZAMANI ZA KIMAUZO.
Inapotokea mbinu zako za kimauzo zimepitwa na wakati huwezi kuendelea
kuwapata wateja wengi. Hapa ndipo maana kampuni kubwa zikaja na kitengo
cha huduma kwa wateja ili kila siku kuweza kumudu kuboresha huduma ili
kuleta mafanikio. Kama kila wakati utaendelea kuwa na mbinu zile zile za kimauzo pasipo kuzibadilisha na kutegemea
muujiza utakaokupa wateja wengi, naomba nikwambie kwenye hilo jambo
lisahau kabisa. Ni muhimu ukabadilika kwanza wewe na wasaidizi wako.
NINI UFANYE ???
Kila mara pata mafunzo ya jinsi ya kuboresha huduma kwa wateja na unaweza kuyapata kupitia semina au warsha mbalimbali za kibiashara. Pia jenga urafiki na wateja ili wakusaidie kupata wateja wengine zaidi na zaidi ili kufikia mafanikio.
Ndimi Mwl Japhet Masatu, Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki.
EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Call: + 255 716 924136 ( WhatsApp ) , + 255 755 400128

HUDUMA MBOVU, HUPOTEZA SANA WATEJA.
Huwezi
kukwepa kukosa wateja kama una huduma mbovu kwa wateja wako. Unaweza usiwe
wewe, hapa wanaweza wakawa ni wasaidizi au wafanyakazi wako ndio wanaokuharibia pasipo wewe kujua kitu
chochote na ukaona uko sawa.
Wengi kwa kushindwa kujua kwamba wanahuduma mbovu ndio wanajikuta ni chanzo cha kuanza kupoteza wateja wengi tena bila kujua. Huduma yako mbovu inaweza ikawa kwenye bidhaa au mazingira au hata jinsi ya kuwahudumia wateja na wakaridhika.
NINI UFANYE ?
Hapa kuwa makini sana na mazingira yote yanayoweza kupelekea huduma mbovu ikatolewa, kama wafanyakzi wako, mazingira na bidhaa unazozitoa. Vitu hivyo unatakiwa kuvihakiki mara kwa mara ili visiwe chanzo cha huduma ya hovyo kwako na kupelekea kukosa wateja.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki
+255 716 924136 ( WhatsApp ) , +255 755 400128

Wednesday, November 14, 2018
KATIKA MAISHA USIBWETEKE NA YALE ULIYOKAMILISHA TUU !!!
Katika MAISHA watu hufurahia zaidi
yale waliyokamilisha pekee huku wakiyasahau kabisa yale ambayo hawajayafanya au
kuyakamilisha.
Pia kitendo cha kuyafurahia yale ambayo umeyafanya na kujiona wewe ni bora zaidi hukufanya uzidi kubweteka na kuachana na yale unayoyakosea katika maisha.
Hivyo NDUGU yangu MDAU wangu katika maisha haya unatakiwa kukumbuka ya kwamba yale uliyoyapanga na kuyakamilisha ni jambo jema sana, ila kama unataka kuwa bora zaidi ya hapo ulipo sasa unatakiwa kushughulika na yale machache yalikuwa ni vikwazo ambayo yamekufanya ushindwe kufanya vizuri zaidi.
Asante sana kwa kusoma , Ndimi MWL JAPHET MASATU , DAR ES SALAAM, TANZANIA, AFRIKA YA MASHARIKI.

Subscribe to:
Posts (Atom)