Matokeo ya michezo ya UEFA iliyochezwa usiku wa leo
- 15 Septemba 2016
Wachezaji wa Madrid
wakishangilia ushindi
Ligi ya klabu bingwa barani ulaya
imeendelea kutimua vumbi usiku wa kuamkia leo ambapo kulikuwa na michezo tisa
ikipigwa katika viwanja tofauti.
Manchester City wakiwa nyumbani
wameibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach, hatrick
ya Kun Aguero na goli moja la Kelechi Iheanacho yalitosha kuipatia Man City
alama tatu na kuwa timu ya pili kwenye msimamo wa kundi C ambalo linaongozwa na
Barcelona.
Tottenham Hotspurs ikiwa nyumbani ilikubali
kipigo cha 2-1 dhidi ya Monaco ya Ufaransa ambayo inaongoza ligi kuu nchini
humo.
Lakini usiku wa kuamkia leo ilikuwa
ni kicheko kwa wachezaji na washabiki wa Leicester City, wakiwa ugenini
waliipiga Club Brugge ya ubelgiji jumla ya magoli 3-0 huku Riyad Mahrez
akifunga mara mbili.
Huu ni mchezo wa
kwanza kwa Leicester City UEFA
Borussia Dortmund ikiwa ugenini
iliidhalilisha Legia Warszawa ya Poland kwa dozi ya 6-0.
Na katika mchezo uliowastaajabisha
wengi ulikuwa ni mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Sporting CP Lisbon ya
ureno ambapo Madrid iliibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Sporting Lisbon ilikuwa ya kwanza
kuandika goli kwenye dakika ya 48 goli lililodumu hadi dk ya 89 ya mchezo
ambapo C.Ronaldo aliisawazishia timu kwa mpira wa adhabu ndogo maridadi kabisa
uliyoenda moja kwa moja kimiani, sekunde chache kabla mpira kumalizika Alvaro
Morata aliiandikia Real Madrid goli la pili akiunganisha krosi ya James
Rodriguez.
Sergio Aguero kwa sasa
ana magoli 9 katika michezo tisa ya msimu huu
Matokeo mengine
Bayern 04 Leverkusen 2-2 CSKA Moscow
FC Porto 1-1 F.C. Copenhagen
Juventus 0- 0 Sevilla
Lyon 3-0 Dinamo Zagreb
BBC SWAHILI
BBC SWAHILI