ligi ya mabingwa ulaya kuanza kutimua vumbi leo
13 septemba 2106
Image copyright Google Image caption
Nembo ya ligi ya mabingwa ulaya
Michuano ya ligi ya mabingwa barani
ulaya inaanza kutimua vumbi leo kwa jumla ya viwanja vinane kuwaka moto.
Katika kundi A miamba wa soka la
Ufaransa, Paris St Germaine watakua nyumbani kuwaalika Arsenal toka England,
huku Basel wakichuana na Ludo Razgrad.
Michezo ya kundi B Wareno wa Benfica
watashuka katika dimba lao la Estádio da Luz kuwakabili Besiktas toka uturuki,
Dynamo Kiev nao watapambana na Napoli.
Fc Barcelona watashuka dimbani Camp
Nou kukipiga na Celtic,matajiri wa Manchester City wataanza kusaka heshima
kwenye michuano hiyo kwa kucheza Wajerumani wa Borussia Monchengladbach.
Michezo ya kundi D Bayern Munich
watakua nyumbani kucheza na Fc Rostov huku Waholanzi wa PSV Eindhoven wakicheza
na Atletico Madrid.
BBC SWAHILI