Lonnie David
Franklin Junior alipatikana na hatia mwezi uliopita, ya kuwaua wanawake tisa na
msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na mitano katika kipindi cha miaka
ishirini iliyopita.
Franklin junior
alifahamika kama Grim Sleeper kwa sababu alitekeleza mauaji mengine baada ya
miaka kumi na mitatu.
Aliwalenga
wanawake masikini na wasichana wachanga ambao aliwaua na kutupa miili yao
kwenye pipa za taka na mitaro ya kupitishia maji machafu.
Mshukiwa huyo sasa
atakabithiwa hukumu yake agosti mwaka huu.
CHANZO CHA HABARI : BBC SWAHILI , JUNI 07