Tuesday, June 7, 2016

WATAKA SHERIA YA TALAKA KUFUTWA INDIA




 
Image copyright Reuters Image caption Ndoa nchini India 

Wanaume na wanawake 50,000 wamesaini azimio la kushinikiza serikali ya India kufutilia mbali sheria ya kutumia neno Talaq, mara tatu kwa misingi ya kuvunja ndoa.
Kwa sasa wanaume Waislamu wanaweza kuwataliki wake zao kwa kutamka neno hilo Talaq mara tatu. Mfumo huo umefutiliwa mbali katika mataifa mengi ya Kiislamu lakini ungali inakubaliki nchini India.
Kampeini ya kutaka sheria hiyo ya talaka maarufu talaq kwa kiislamu, kufutiliwa mbali, imepata uungwaji mkono nchini India.
Maelfu ya watu wanasaini azimio kuunga mkono kampeini hiyo inayoongozwa na shirika la kina mama nchini India la BMMA, ambalo limeandikia barua kwa shirika kuu la kutetea haki za kina mama likitaka sheria hiyo kufutiliwa mbali.
Shirika hilo limesema kuwa sheria hiyo imeharibu maisha ya kina mama wengi na watoto na mwaka wa 2015 lilitoa ripoti ambayo ilibainisha zaidi kesi mia moja kuhusiana na sheria hiyo iliowalishwa.
Azimo kama hilo pia liliwasilishwa mbele ya mahakama ya juu zaidi nchini humo na mama mmoja ambaye alitalakiwa na mumewe kupitia barua.

 CHANZO  CHA  TAARIFA : BBC  SWAHILI , 01  JUNI, 2016