Mtandao wa Twitter unafanyia
marekebisho sheria zake ili kuwarahasishia kazi watumiaji wake na kuufanya uwe
wa kuvutia kwa wale wanaojiunga nao kwa mara ya kwanza.
Wanachama wa mtandao hao sasa
wataweza kuongeza kile wanachochapisha kwenye mtandao huo, zikiwemo picha na
video bila ya kuathiri kiwango cha sasa cha maneno 140 ambayo mtu anastahili
kuandika.
Twitter pia itafanya marekebisho
kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao.
Twitter
imekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa
kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia.
Mwanzilishi mwenza wa Twitter na
mkurugenzi mkuu Jack Dorsey, aliiambia BBC kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa
wakati watu wanapoutumia unaonekana kuwa ulio na maana.
Mdadisi mmoja anasema kuwa hatua
hizo zinaashiria mwelekeo mwema, lakini akaongeza kuwa wameangazia suala moja
tu ambalo ni kuongeza watumiaji wake.
Licha ya mtandao huo kutumiwa sana
katika masuala yanayohusu habari mwaka uliopita, umekuwa na wakati mgumu
kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio
katika kuutumia.
Twitter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana
katika mtandao.
Brian Blau, ambaye ni mchambuzi
kutoka shirika la Gartner, anasema matatizo yanaoikumba Twitter kuwapata
watumiaji wapya hayawezi kutatuliwa na mabadiliko hayo.
Anasema kuwa tatizo kuu ni kuwavutia
watumiaji wapya na kuwafanya wawe wazalendo kwa mtandao. Anaendelea kusema kuwa
bado Twitter haijalishughulikia hilo.
CHANZO CHA TAARIFA: BBC SWAHILI, 25, MEI, 2016