Huku wafanyikazi kote duniani wakiadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, nchini Tanzania, wafanyikazi wanakila sababu ya kutabasamu.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaongezea wafanyikazi wote nchini humo asilimia mia mbili 2% mishahara.Katika hotuba ya kuadhimisha siku ya wafanyikazi, bw Magufuli alitangaza kupunguzwa kwa kodi ya mapato PAYE kutoka asilimia 11% hadi asilimia 9%.
Hii inamaanisha kuwa kila mfanyikazi atapata ongezeko la mapato yake kwa asilimia 2%.
Magufuli alitangaza kauli hiyo kufuatia ombi la wafanyikazi kupitia kwa katibu mkuu bwana Nicholus Mgaya la kutaka wanusuriwe makali ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu.
Aidha rais Magufuli alisema anatimiza ahadi aliotoa kwa wapiga kura wakati wa kampeini kuwa endapo watamchagua angefanya kila jitihada kuwapunguzia mzigo wa kodi wafanyikazi wa Tanzania.
Kuhusu ongezeko la mshahara wa chini zaidi atakaolipwa mtanzania bwana Magufuli amewasihi wampe muda kidogo akomeshe rushwa na kuimarisha uchumi wa taifa kisha atatoa tangazo.
''Pamoja na uamuzi huo, Rais Magufuli pia amewaahidi wafanyakazi kuwa baada ya kupunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi, serikali yake itafanyia kazi mapendekezo ya kuongeza mishahara''
''aidha, amewataka wafanyakazi kuunga mkono juhudi za kuwafichua wanaozalisha wafanyakazi hewa, huku akibainisha kuwa mpaka kufikia jana tarehe 30 Aprili, 2016 jumla ya wafanyakazi hewa waliobainika walikuwa 10,293 ambao kwa mwezi mmoja tu wamelipwa shilingi bilioni 11.6.''
Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, ikulu Dodoma Gerson Msigwa ilisema.
CHANZO CHA HABARI : BBC SWAHIL, Jumapili, 01 mei, 2016.