Ni wazo la
kiwendawazimu nyakati hizi
kuyakuza mambo yasiyo
na umuhimu au
kuangalia mambo yetu ambayo
hayakuwa na MAFANIKIO
kana kwamba ni
MAJANGA yasiyoweza kurekebika.
Tunayakuza matatizo
yetu binafsi na ya kijamii
kiasi ambacho tunakata
tamaa kwamba hatuwezi
kuyatatua tena. Tunaishi katika
zama zenye nafasi
zisizo na mipaka , lakini WANAWAKE
na WANAUME wanaishi
katika maisha yenye
vikwazo kwa sababu
ya mawazo ya
kitumwa.
Leo tunasisitiza kuendelea
kutegemea MAJARIBU , KUKATA TAMAA
na MATAKWA YETU , hali
tukiacha KUZINGATIA BARAKA
NYINGI ZINAZOTUZUNGUKA.
Tunaomboleza kwa
sababu ya KUPANDA
KWA GHARAMA ZA
MAISHA na KUSAHAU
MWANGA WA JUA ,
HEWA SAFI , na UZURI WA
BAHARI, bado vinapatikana bure.
Tunalalamikia bei ya
hiki na kile , huku
tukidharau mwito mzuri
wa milima ya
kifalme na mwito
mtamu wa bahari , vyote hivyo
vikituhakikishia USALAMA dhidi
ya USUMBUFU na
nguvu mpya ya
kutuwezesha kuishi.
Lazima manung”uniko yawepo
kama tunataka kuzuia MADHARA , hakika manung”uniko
ni halali , lakini kitu
gani kinachoweza kuhalalishwa katika
hali ya hasira
pekee , bila kujali hazina
ambazo si za
kwetu , hazina ambazo haziwezi
kupunguza UMASKINI.
Ni
watu tunaopenda mambo
ya ovyo na
yasiyoridhisha , badala ya kuwa
watu wanaojiamini na
kufahamu kuwa ni
watoto wa falme , na
kwamba , hata kama sisi
ni MASKINI kiasi gani , bado tunamiliki
NYUMBA yenye hazina
ya UTAJIRI WA
KIROHO pasipo sisi
wenyewe kufahamu.
HESABU MAFANIKIO
yako ambayo mara
nyingi hudharauliwa ; ni ya
UWEZO WA KUONA , AFYA
na NGUVU , UWEZO MKUBWA
KIAKLI na KUFAHAMU
mambo mengine ambapo
hayaonekani kwa macho.
FURAHI kuwa
wewe ni HAI , kwani
kuwa HAI ni
kuwa na kila
kitu. UHAI ni zana
ambayo itakuwezesha kujenga
PARADISO au MAKAZI
ya kawaida.
Kama una
UHAI , una kila kitu ,
kwa sababu kama
una uhai unaweza
kukabiliana na mipaka , pia unaweza
kuamua MWELEKEO WAKO
UWE UPI.
NYOSHA MGONGO
WAKO NA TABASAMU.KABILIANA NA
MAPIGO YA MAISHA
KWA TABASAMU , ingawa si
kila wakati unaweza
kuzuia MACHOZI kutoka
katika macho yako.
Ni kweli
kwamba kuna mambo
mengi magumu , kiasi cha
kumfana mtu awe
na HUZUNI , LAKINI
kama tutaendelea kuyaangalia
hayo tu , tutakosa MAFANIKIO.
NI HERI KUTABASAMU
NA KUTOYAJALI MATATIZO.
Inaweza isiwe
rahisi KUTABASAMU wakati
unakabiliwa na kipigo , lakini ngumi
inaweza kumtoa mtu
kwenye mashindano iwapo
hawezi kuinuka juu , na
hakuna idadi maalumu
ya nyakati za
kuinuka na kurudisha
mapigo.
INUKA NA
PIGANA , usifanye hivyo
kwa manung”uniko , lakini kwa
moyo wa FURAHA
ambao unakufanya uwe
na nguvu maradufu
na kuimarisha uwezo
wako.
PUMUA HEWA NZURI
KWA NGUVU LEO. Angalia juu
kwenye NYOTA. Isikilize
sauti yako ndogo. Inakuhimiza UINUKE
na KUPIGANA. Kabiliana na
MAISHA kwa KUJIAMINI
kwamba utaweza
kufanya ONESHO ZURI , na
kwamba utakuwa MSHINDI.
Kwani ROHO yako
itakuwa na MAFANIKIO , hata kama
kuna TATIZO lolote
unaloliona kwa macho.
ROHO NI
YA PEPONI , HAINA MWISHO , hupumua hewa
ya mbinguni na
haiwezi kutekwa na
uharibifu au NAFASI
au HATARI , labda
kama umeamua kutoipa
UHAI. INUKA , KISHA CHAJI
NGUVU ZAKO .NENDA KWA
USHINDI. MUNGU AKUBARIKI SANA
NDUGU MSOMAJI.
Makala imeandikwa
na MWL JAPHET
MASATU , anapatikana kwa
EMAIL , japhetmasatu@yahoo.com. WhatsApp
+ 255 755 400128 / +255 716
924 136.