INGAWA sisi ndio
tunaoishi , kama tunavyoweza
kukumbuka, ni bayana kwamba
tuna UFAHAMU mdogo
sana kuhusu MAISHA
yetu kuliko wanavyofahamu marafiki
au maadui zetu wakubwa.
Hawa wanaweza
kujua vizuri kasoro
ya ufahamu wetu; wanaweza kutathmini
udhaifu wetu kuliko
sisi wenyewe ; wanafahamu
kwa usahihi zaidi
uwezo wetu ulivyo ,
wakati sisi wenyewe
tunaweza kujisifia kwa
viwango vsivyo vya
kweli.
Hatua ya
mwisho katika kuishi
vizuri ni kuhakikisha
tunajifanyia tathmini sahihi. SAIKOLOJIA inasaidia
kufahamu hayo—hutupatia DARUBINI
ya ufahamu ambayo
si tu inatuwezesha KUJIFAHAMU
wenyewe kama wengine
wanavyotufahamu , lakini pia
KUFAHAMU WAZI NGUVU
NA UDHAIFU WETU, KISHA
kutuonesha uwezo na
mapungufu yetu.
JUNG
ameainisha ubinadamu katika
makundi mawili , LA
WATU WASIRI na wale WALIO WAZI.Misamiati hii
miwili ina maana
gani ? Misamiati hii
miwili ina maana
gani ? Kwa ufafanuzi
wa haraka haraka ,
WATU WASIRI wanaangalia ndani ;
WATU WA WAZI
huangalia nje . Picha nzuri
zaidi inapatikana kwa
kuwa na aina
zinazotambulika.
WATU
WASIRI hupenda kujisomea , wana uwezo
mkubwa wa KUFIKIRI , HUEPUKA MAKUNDI
YA WATU, HUPENDA UPWEKE ,
HUPENDA KUFIKIRI FIKIRI , KULIKO VITU. Ni
wepesi sana kufikiri
na kuchukia , lakini mara
nyingi huepuka kuchanganyika na
wengine. KUNDI HILI HUPENDA
VITABU KULIKO WATU , NI
WAFIKIRIAJI SANA , WANA AIBU
NA HUPENDA KUJIFICHA.
Kundi la WALIO
WAZI ni kinyume
na WASIRI ; HUPENDA KUJIAMINI
na KUTUMIA NGUVU ,
HUPENDA KUFURAHI , HUPENDA
KUWAPONGEZA WENGINE , HUPENDA KUCHANGANYIKA NA
WENGINE , HUEPUKA UPWEKE,
HUPENDA MAKUNDI YA
WATU ,HUPENDA ZAIDI VITENDO
KULIKO KUFIKIRIA NA
VITABU. Hawapendi kuficha hasira
zao wakichukia na
hupenda zaidi KIJIKWEZA
kuliko KUJISHUSHA.
Je,
unayatambua makundi haya ?
Wewe upo katika
kundi lipi ? Bila kusema
kuwa unaweza ukawa
pande zote mbili , isiwe vigumu
kuamua upande ulio
na uzito zaidi.
Hapa , sasa, kuna somo
la kujitathmini mwenyewe. Tulia na
uamue iwapo wewe
ni MSIRI au
MUWAZI , ndipo ufahamu
utakaoupata utakupatia faida
mbili.
KWANZA , utakuwa na
uwezo wa kusahihisha
uwiano , yaani , kama
wewe ni MSIRI
, unaweza kuanza kupenda kuwa
karibu zaidi na
vitu pamoja na
watu kuliko kujipenda
mwenyewe ; kama wewe ni MUWAZI, unaweza
kuanza kuchambua rasilimali
ulizo nazo. Kwani tabia
yenye uwiano ndiyo
inayoweza kukubalika kwa
makundi yote mawili.Faida ya
ziada ni kwamba, huweza kukupatia
ufahamu wa upinzani
mdogo dhidi ya
baadhi ya majukumu.
Kwa mfano, mtu
MSIRI ana FURAHA
katika uwezo wa
kazi.Hiyo haimaanishi kuwa
kundi moja haliwezi
kufanya kazi nzuri
ambayo tabia ya
kundi linguine hufaa
zaidi. Kwa namna yoyote
ile, lakini kwa
UFAHAMU, kwa mfano , kama
wewe ni MSIRI ,
KWAMBA unatakiwa kuonesha
viwango vya mchanganyaji mzuri, itakuwezesha kufahamu
umuhimu wa kuongeza
jihudi ili kupata
MAFANIKIO.
Hivyo, ni
vyema ufahamu kundi
ulilomo ndugu yangu. UFAHAMU utakaoupata
una manufaa sana
kwako.
Asante kwa
kusoma makala hii ndugu
yangu usisahau kumshirikisha mwenzako
AJITAMBUE.
Makala hii
imeandikwa na MWL
JAPHET MASATU. Anapatikana kwa E-MAIL
, japhetmasatu@yahoo.com + 255 716
924 136.