NI RAHISI , NI SUALA LA UAMUZI TU !
Tabia ni kitu cha
ajabu sana.Wanasaikolojia wa
tiba na afya
wanashauri kwamba ni
sawa na mtu
kutwanga maji ndani
ya kinu kwa
kujaribu kurejesha afya
iliyodorora bila kubadili
TABIA zenye
kupelekea afya hizo
kuwa mbaya.
Bila shaka
umeshawahi kuona mtu
mwenye hali mbaya
kiafya kutokana na
pombe au sigara
lakini akaendelea kutumia
vitu hivyo kama
kwamba havimzuru kwa
chochote.
Tabia au
mazoea yamepelekea watu
wengi sana kupoteza
maisha yao huku
wakiona.Huenda mtu akadhani
kwamba mazoea maana
yake ni kufanya
mambo yenye athari
mbaya kwa afya
ya binadamu.Lakini mazoea
yanaweza pia kuwa
ni mtu kuacha
kufanya mambo ambayo
angetakiwa kuyafanya ili
kuboresha afya yake.
Huenda ni
vizuri nikataja mambo
ambayo mtu akiyajengea mazoea ,ataweza kurefusha
umri wake.Kulingana utafiti
uliofanywa huko ALAMEDA
CALIFORNIA,
MAREKANI miaka ya 1970, Ilionyesha kuwepo
kiwango kikubwa cha
tofauti iliyokuwepo katika
umri wa kuishi
kati ya waliokuwa
na mazoea hayo
mazuri , na wale
ambao hawakuwa nayo. Mazoea
hayo ni haya
ndugu yangu msomaji soma hapa kwa
makini na yafanyie
kazi :--
KIFUNGUA KINYWA : Kuna watanzania
ambao huwa
hawajui kwamba kifungua
kinywa ni muhimu
sana kwa afya
ya mtu.Mtu mwenye
mazoea ya kupata
kifungua kinywa asubuhi
anayo sababu ya
kuamini kwamba siku
zake za kuishi
zimeongezeka angalau kwa
asilimia tano.
KULAKULA: Kulakula hovyo ,
hapa na pale
ni tabia mbaya
sana.Mtu anayemudu , au mwenye
mazoea ya kujizuia
kula hapa na
pale na badala
yake kula kwa
kufuata utaratibu maalum.Hana
sababu ya kutoamini
kwamba ataishi hadi
kuzeeka kabisa.
USINGIZI: Inatakiwa mtu
awe na mazoea
ya kulala kwa
kati ya saa
saba hadi nane
kwa usiku mmoja.Kama
mtu ana matatizo
ya usingizi hana
budi kutafuta ufumbuzi
wa tatizo hilo
ili kupata usingizi
huo. Ni vema
mtu kulala saa
4.00 usiku na
kuamka saa 11.00
au 12.00 alfajiri.
UZITO: Ni
vema kwa mtu
kujali sana uzito
wa mwili wake
kulingana na urefu
alionao.Kwa kawaida mtu
anatakiwa kuwa na
uzito wenye kutofautiana
na urefu kwa
sentimita 100 au
110.Kwa mfano , mtu akiwa
na urefu sentimita
165 , uzito wake
unatakiwa usizidi kilo
50 hadi 65.Kimkokotoo ni
urefu kwa sentimita
kutoa uzito kwa kilo, ambapo baki
haitakiwi kuwa chini
ya 100 au
zaidi ya 110. PIMA UZITO MARA KWA MARA .
KUVUTA : Uvutaji wa
sigara ni mazoea
ya hatari sana
ndugu yangu.Katika sigara
mna dawa ijulikanayo
kama “ NICOTINE”.Dawa hii ina
madhara na ulevi
wa aina yake.Ndugu
yangu msomaji kama
mtu atakuwa na
mazoea ya kukwepa
moshi wa sigara
kwa kadiri awezavyo
, hayo ni mazoea
muafaka. ACHA KUVUTA SIGARA.
POMBE:Mazoea ya kunywa
pombe kupita kiasi
ni ya hatari
kwa maisha yetu ndugu yangu
mtanzania. Katika pombe mna
dawa iitwayo “ALCOHOL”.
Dawa hii
ni mbaya sana
ina athari kubwa
sana mwilini.Mtu ambaye
anaweza kujenga mazoea
ya kunywa kidogo
au kutokunywa kabisa , huyo
ana uhakika wa kuishi zaidi maisha
marefu zaidi. ACHA KUNYWA
POMBE KUPITA KIASI.
MADAWA YA KULEVYA: Madawa ya
kulevya huweza kudhuru
afya ya mtu
kutokana na njia
zile mlevi anazochagua
za kutumia madawa
hayo. Kwa mfano baadhi
ya wale wanaochagua
njia ya kujipiga
sindano wenyewe huandamwa
na matatizo ya
magonjwa ya ini
kutokana na kushindwa
kwao kudumisha hali
ya usafi unaoridhisha
katika vifaa vile
wanavyotumia kwa kusudi
hilo.Hali hii hupelekea
kifo ini linaposhindwa kufanya
kazi .Ikumbukwe kwamba ulevi
wa madawa ni
wa hatari zaidi
kuliko ule wa
pombe. Baadhi ya vijana
wanaolewa madawa akili
zao huharibika kabisa
na kuwafanya wenda
wazimu maisha yao
yote.
Madawa ya
kulevya yapo ya
aina nne kubwa :----
-----Aina ya kwanza
ni yale madawa
ya kulipua moyo{yaani yale
yanayoondoa usingizi, uchovu n.k.
}, hutumiwa na madereva , walinzi ,n.k.
-----Aina ya pili ni
yale yanayotia usingizi, madawa haya
hutumiwa na vijana
wengi mitaani mwetu
tunamoishi , mahospitalini
hutumika kwa shughuli
maalumu n.k.
-----Aina ya tatu
ni yale yanayopooza
moyo { yaani yale yanayoleta
utulivu na kupunguza
wasiwasi , kiwew n.k }
----Aina ya nne
ni yale ya kuleta
mabadiliko ya ufahamu
kuhusu nafsi, na ukweli
wa mambo.
EPUKA MADAWA YA KULEVYA , YANA ATHARI KUBWA SANA !
MAZOEZI: Kwa bahati
mbaya sana , Watanzania wengi
hawana mazoea ya
kufanya mazoezi.Ukweli ni kwamba,
mazoezi ni jambo
kubwa na muhimu
sana kwa maisha
ya mtu.Mtu asiyefanya
mazoezi mara kwa mara, kwa
kawaida ni goigoi
kimwili na hata
kiakili. Maisha yake pia
hupungua kwa kiasi fulani.
TUFANYE
MAZOEZI MARA KWA
MARA KWA AJILI
YA AFYA ZETU
WATANZANIA WENZANGU.
Kwa kumalizia ndugu
msomaji wangu naweza
kusema ya kwamba
hizi siyo tabia
pekee zinazohitajika katika
kufanya maisha yawe
marefu , zipo nyingine kadhaa. Kwa
mfano , MTU KUPATA MUDA
WA BURUDANI , KUWA MWANGALIFU
NJIANI { MAGARI } na KUTOPENDA
MATATA { UGOMVI }, UZINZI
{NGONO ZEMBE } na
nyingine.
ASANTE MSOMAJI
WANGU KWA KUSOMA MAKALA HII USICHOKE
KUTEMBELEA MAISHA NA
MAFANIKIO BLOG. MUNGU AKUBARIKI !
Makala hii imeandikwa
na MWL JAPHET MASATU
anapatikana kwa +255 716 924 136 / +
255 755 400
128, DAR ES SALAAM , TANZANIA.