Friday, June 5, 2015

NIPATEJE PESA NYINGI ZA KUNITOSHA ?



 
   
Ieleweke  ya   kwamba  pesa  ni  nzuri   kwa  sababu   PESA   NI   MALI  YA  MUNGU. SHETANI  amewaingia   watu   na  kuwafanya   waamini  ya  kwamba   PESA  NI  MBAYA  na   hata  kuwafanya   watu  kuichukia.
Ukiwa   na   fedha  utanunua  chochote   ukitakacho  katika   maisha   yako.Utakula   utakavyo, utavaa  utakavyo , Utaishi  nyumba  utakayo , Utamiliki  gari  utakalo , Utakwenda    popote  utakako n.k !!

“Fedha  ni  mali   yangu ,  na  dhahabu  ni  mali  yangu ,  asema   Bwana  wa   majeshi “   -Haggai  2: 8.

“…..Na  fedha  huleta  jawabu  la  mambo  yote “.   ----Mhubiri   10:19

  MUNGU  anapenda  uwe  na  FURAHA , AMANI , AFYA  NJEMA  na   UFANIKIWE  katika  mambo yako  yote  katika  maisha.

“Mpenzi , naomba  ufanikiwe  katika   mambo  yote   na  kuwa   na  afya  yako ,  kama   vile  roho  yako  ifanikiwavyo.   ---3  Yohane  2

Fedha haidondoki  mikononi  mwako  toka   Mbinguni  au   huwezi    kuamka   asubuhi    na  kuikuta  chini  ya   mto   wa  kitanda  chako
.Unasali ,ndiyo , unakiri  na  unawaza   vema ,  sawa  , Unamtumikia  Mungu  kanisani ,  unakesha  kuomba  utajiri , umeokoka  ! Unatoa   fungu   la  kumi , Unatoa  sadaka vizuri  sana , Unaimba  sana  kwaya , unawakumbuka  maskini ! Haya  yanafanywa   na  watanzania  wenzangu   wengi  kwa   kukesha   kanisani    wakiamini watapata  fedha  kwa  KUSALI  PEKEE !!   haya  yote   ni  mazuri  na  yanastahili  kufanywa  bila   kuachwa  lakini  kuna  jambo   lingine  la  msingi   unatakiwa  ufanye  ili  uweze  KUPATA PESA  YA  KUTOSHA. Badilika  Mtanzania. Wapo   waliofanya  hayo  tu  wakaishia  kuwa  Maskini  wa  kutupa.

 




SASA   SWALI ,  FEDHA  ITAINGIAJE  MIKONONI MWANGU ? Ili  upate   FEDHA  unapaswa  kutoa  BIDHAA  au    HUDUMA  fulani   katika   eneo  la  kusudi  la  MUNGU  juu  ya  maisha  yako.Mungu  alikuleta  duniani  kwa  ajili  ya  kusudi maalumu   na  upo  mpango  mkamilifu  juu  ya  maisha  yako. Mtanzania   mwezangu  karibu  duniani  tufanye  tulichokusudiwa  kufanya.Fedha   ni   nyenzo  ya  mabadilishano  ya   BIDHAA  na  HUDUMA.
Fedha  iko  mikononi  mwa  watu , unapaswa  kuelewa   BIDHAA  au  HUDUMA  gani  ya  kuwapa  WATU WA  MUNGU  ili   uivute  fedha   hiyo   toka   kwao  kuja  kwako. PESA  hutokana  na  BIDHAA  unazozalisha   au  HUDUMA  unayotoa.  Unaona   Ukweli  huu !   Ikiwa  huna  BIDHAA   wala  HUDUMA  yoyote   unayotoa  sahau    habari  ya kupata   FEDHA.
Unapaswa  kutoa   BIDHAA  na  HUDUMA  bora  ndipo  utakapopata  PESA.  Mtu  aliyeajiriwa  anatoa  HUDUMA  fulani   pale  kazini  kwake  hivyo  mwisho  wa  mwezi  anapewa   FEDHA. Hali  kadhalika     WAFANYABIASHARA , MADAKTARI , WANASHERIA , MAASKARI ,  WALIMU  n.k.  hutoa    HUDUMA   au  BIDHAA  zinazo  wafanya    Wapate   Fedha.
Kutoa   BIDHAA  au  HUDUMA ni   chaneli  au   njia  ya    kutiririsha  UTAJIRI  toka  Kwa  WATU  WA   MUNGU    kuja  kwako.

SWALI :  HATA  SIJUI  NITOE  BIDHAA  AU  HUDUMA  GANI  !!  Kuwa   MBUNIFU {creative } mtanzania   katika  maisha  yako.  Waza   na  fikiri  kwa  usahihi  kabisa  watu  wana  shida  gani  hapa , wanahitaji  nini  hapa. Nini  hawana ?  Ni  bidhaa  au  huduma  gani  naweza  kuwapa  au  kuitoa  ili  kutatua  matatizo  yao ? Baada  ya  kuwaza   fanya  utafiti !  Utafiti  kwanza  !  Kujua   watu  wana  shida  na  nini  ? HAYA  CHANGAMKA  MTANZANIA !  Hata  kama  utatumia  miezi , miaka  katika  utafiti wako.Hakika  utakachofanya  hapo  baada  ya  utafiti , watu  watakubali ,  watakuheshimu.  USIKURUPUKE  tu  kwa   kuiga.  Fulani  alifanya  hivi  akapata  pesa , nawe  unaingia.  Mhh !! Hatari  ndugu  yangu .
------Buni  shughuli   inayotatua   matatizo  ya  watu :  PESA  ZITAKUKIMBILIA.
------Epuka  shughuli  zisizotatua  matatizo   ya  watu :  UTAPOTEZA  MUDA.
------Tafiti  kwa  usahihi  watu   wanahitaji  nini :  UTAJUA  CHA  KUFANYA.
------Usiige  bila   utafiti :  UTAKWAMA

Ndugu   Mtanzania  acha  uvivu.  Lazima   utoe  BIDHAA  au  HUDUMA  iwapo  unataka  FEDHA  ije  kwako. Tuko  katika  ulimwengu  wa   FEDHA  kwani  kila  kitu   hununuliwa  kwa  FEDHA . Bila   FEDHA   utaumia .

     Angalia   ni   nini  kinahitajika  kufanywa  na  fanya  hicho. MUNGU  hapendezwi  na  wewe  kukaa  muda  mrefu   sana  ukitafuta  WAZO  la  BIDHAA  au  HUDUMA  ya  kutoa.Mara  zote  kuna   kitu  cha  kufanya  japokuwa  kinaweza  kisiwe  kikubwa  sana.  Kinaweza  kuwa  kidogo  UNACHOKIDHARAU. USIDHARAU  MWANZO  MDOGO  TAFADHALI   NDUGU  YANGU. 
   KANUNI  YA  MAFANIKIO inakutaka  uwe  tayari  kuanzia  padogo.Kila  ukionacho  kikubwa  leo  kilianza   kidogo  jana.Kubali  kuanzia  mahali  fulani  na  panda   juu  ukitokea  hapo. Kubali   kukamilisha  kitu  kimoja  baada  ya  kingine , usiwe  na  pupa  ya  kumaliza  mambo   mengi {yote}  kwa mara  moja. Watu  wengi  wanapenda  kuangalia  vinvyong"aa  na   kushangilia ,  hawa  ndo     WANAOONDOKA  DUNIANI  BILA  KITU .  Kwani  hujui  kwamba  ukiona   vyaelea  vimeundwa  ? Kila  Mafanikio  unyoyaona leo  kuna  uwekezaji  wa  kutosha  uliofnyika  siku  nyingi  zilizopita.
    MSWAHILI  anasema  ,  ndondondo  si  chururu ,  kidogo  kidogo  hujaza   kibaba, na  chembe  na  chembe  mkate  huwa. Watu  wako  katika  saizi /  maumbo / vimo  mbalimbali ,  vilevile  MAISHA  yako katika  viwango / madaraja  mbalimbali.
   Yeyote  anayeudharau  mwanzo  mdogo   hatauona   mwisho  mkubwa.

   "Maana  ni  nani  aliyeidharau  siku  ya  mambo  madogo ?-- ZEKARIA 4:10

                      USIKATE   TAMAA ,  UNAWEZA   KUFANIKIWA


Makala  hii  imeandikwa  na  MWL  JAPHET   MASATU , DAR  ES  SALAAM , TANZANIA , Mwalimu  wa  Elimu  ya  Maisha na   Mafanikio , Saikolojia , Biashara /  ujasiriamali  ,   anapatikana  kwa  namba     +  255  755  400  128 { WhatsApp }  /  + 255  716  924 136   /  + 255 785  957  077