DUKA LA VYAKULA
NA BIDHAA MCHANGANYIKO
Biashara ya duka
ni biashara nzuri.Inahitaji mtaji
mdogo japo faida
ya biashara hii
ni ndogo sana na
inahitaji umakini na
udhibiti mkubwa ili
uweze kuendelea na
kufanikiwa.Matatizo ya biashara
hii ni :- ushindani
wa kibiashara kwani
watu wengi wanapenda
kuifanya biashara hii , udokozi wa
fedha na bidhaa
toka kwa muuzaji
na mmililki wa
duka, kuchukua fedha dukani
bila kuzirejesha, ukosefu wa
ubunifu , hivyo kufanya
biashara kushindwa kuendelea ,
na kadhalika. Ili kukabiliana
na matatizo hayo
unapaswa kuwa mbunifu.Penye ushindani
mkubwa toa huduma
nzuri kwa wateja.Vile
vile wateja wako
waaminifu unaweza
kuwafungulia daftari na
kuwakopesha walipe mwisho
wa mwezi.Ukiwa umezungukwa
na maduka mengi
ya rejareja , lifanye duka
lako liwe la
mchanganyiko la kuuza
bidhaa kwa jumla
na reja reja , hivyo
hata wale wapinzani
wako wawe wateja
wako. Usichukue vitu na
fedha kiholela toka
dukani, UKICHUKUA KITU CHOCHOTE
AU FEDHA MWAMBIE
MUUZAJI AKUANDIKIE DENI
NA LAZIMA ULILIPE
DENI. Kama UMEJIAJIRI mwenyewe
na wewe ndiyo
unauza hilo duka
JIPANGIE MSHAHARA. Usichanganye
fedha za duka
na fedha zako
za matumizi ya
nyumbani.