BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Sunday, May 4, 2025
KITINI-----STADI ZA KAZI / ELIMU UJUZI / AMALI ----DARASA LA SITA ( STD 6 )----" UFUNDI BOMBA " ----MABOMBA YA PLASTIKI , KUFANYA MATENGENEZO YA MABOMBA YA PLASTIKI , UTANDIKAJI NA UUNGAJI WA MABOMBA-----FULL NUKUU----KWA SHULE ZA MSINGI---TANZANIA----( PDF )-----CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Friday, May 2, 2025
KITINI----STADI ZA KAZI / ELIMU UJUZI / AMALI----DARASA LA SITA ( STD 6 )--- "KILIMO NA UFUGAJI "----USTAWISHAJI WA MIMEA YA MAZAO YA CHAKULA---MPUNGA , MTAMA , UWELE , MIHOGO , VIAZI MVIRINGO , VIAZI VITAMU , MAHARAGE , KUNDE , MBAAZI----UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA WANYAMA---UTENGENEZAJI WA VYOMBO VYA WANYAMA WAFUGWAO---UFUGAJI WA NGURUWE & KUKU WA MAYAI---KWA SHULE ZA MSINGI---TANZANIA----( PDF )------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Thursday, May 1, 2025
KITINI---STADI ZA KAZI / ELIMU UJUZI / AMALI ----DARASA LA NNE ( STD 4 )---( 19 )---UPISHI ----KANUNI ZA USALAMA NA USAFI KATIKA UPISHI , UKAANGAJI WA VITAFUNO , UPISHI WA CHAPATI , UPISHI WA BISI , UTAYARISHAJI WA VINYWAJI MOTO CHAI NA KAHAWA----FULL NUKUU---KWA SHULE ZA MSINGI----TANZANIA-----( PDF )-------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Wednesday, April 30, 2025
KITABU 338 --- TUJIFUNZE BIBLA TAKATIFU ---( 04 )-AGANO LA KALAE---( 04 )---JARIBIO ---UTANGULIZI , DHAMBI YA ISRAELI , MANABII , ISAYA , YOSIA NA MATENGENEZO YA DINI , YEREMIA NA JARIBIO KUBWA , EZEKIELI , MAANDIKO MENGINE YA WAKATI ULE---MWANZO I--II , ISAYA YA II----FULL NUKUU----NA PADRE J. BOUQUET DES CHAUX , M.Afr.-----TOLEO LA PILI ---1997---CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
MAKALA : UNASEMA HUNA MUDA ?? JE , RATIBA YAKO YA KILA SIKU INASOMAJE ?? KULALA , KULA , KUONGEA UMBEA , KULALAMIKA ?? KUCHATI MITANDAONI ? TUMIA MUDA VIZURI KUINGIZA KIPATO -----NA MWL. JAPHET MASATU-------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Rafiki, kila siku unasema, *sina muda* , kumbe ni wewe tu hujui namna ya kuutumia.
Haupo peke yako.
Kila siku unajiambia “sina muda”,
...lakini unatumia masaa mengi (masaa manne kwa siku) kwenye mitandao ya kijamii (WhatsApp, Facebook, Instagram, TikTok).
Unasema unataka kufanikiwa, lakini ratiba yako inasoma: kulala, kula, kuskrolu kwenye mitandao, kulalamika.
Unajua ni nini kinauma zaidi?
Ni kuona mtu ambaye alikuwa hana chochote, alikuwa anakunywa chai kavu na maandazi ya mia tano, leo hii anaingiza laki kwa siku,
... na bado wewe uko pale pale.
Tofauti si akili, si bahati, ni jinsi mtu alivyoamua kutumia muda wake.
Wengi wameaminishwa kuwa mafanikio ni kwa watu waliobahatika, au waliotoka familia nzuri.
Lakini ukweli ni huu: kila mtu ana masaa 24.
Elon Musk ana masaa 24.
Wewe pia una masaa 24.
Ukitumia saa 1 kwa siku kuboresha maisha yako, hayo ni masaa 365 kwa mwaka.
Nani anakuzuia?
Zifuatazo Ni Mbinu 3 Za Kuchukua Hatua Leo:
1. Saa Moja Tu Kila Siku:
Jifunze kitu kimoja kinachoweza kukuingizia kipato (kama Copywriting, content creation).
Simu yako iwe zana, sio toy.
2. Panga Muda Kama Mzigo Wa Gari:
Jua dakika zako zinaenda wapi.
Tengeneza ‘to-do list’ ya kweli, sio ndoto.
Fanya vitu 3 vya maana kila siku kabla ya saa tano asubuhi.
3. Tafuta Mtandao Wa Watu Wenye Malengo:
Unakuwa kama watu 5 unaotumia nao muda mwingi.
Kama wote ni wasumbufu, utakua msumbufu pia.
Hii hapa ndiyo ile hadithi ya kweli ya Kelvin wa Tandika:
Jamaa alikuwa mtaani, hana kazi rasmi.
Aliamua kujifunza jinsi ya kuuza bidhaa za watu wengine kupitia WhatsApp na Instagram.
Kila siku aliweka saa moja kujifunza na kupost.
Mwaka mmoja baadaye, ana duka la perfume na ameshaandika eBook inayoingiza hela kila mwezi.
Alianza na muda, si mtaji.
Usilale na “kesho nitaanza.”
Anza leo.
Kumbuka; Muda haukupi second chance, ila wewe unaweza kuamua kuanza upya leo.
MAKALA : KUWA NA NIDHAMU NA PESA ZAKO !! ANZA KUWEKEZA BUKU ( SH 1000 ) KILA SIKU UJENGE UTAJIRI WAKO WA KESHO ----NA MWL. JAPHET MASATU---------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Mpendwa Rafiki,
Watu wengi wanaamini kuwa ili uanze kujenga utajiri, lazima uwe na hela nyingi ,milioni tano, kumi, au hata zaidi.
Wengine wanasema, *Mimi ni wa mshahara wa chini, siwezi kufika mbali.*
Lakini ukweli ni kwamba watu wengi hawajui kitu kimoja muhimu: nguvu ya *buku* moja tu.
Buku ambayo unaitumia bila mpango kila siku, inaweza kuwa tiketi yako ya kutoka kwenye umaskini hadi kwenye uhuru wa kifedha.
Ni mara ngapi umetumia buku kununua soda, chipsi, vocha, au kitu usichohitaji halafu ukaishia kusema, *Ah ni buku tu*?
Halafu mwisho wa mwezi unakuta umekopa, umeshindwa kuwekeza, hata akiba huna.
Inasikitisha, siyo? Sasa fikiria, kama kila siku unapoteza buku moja tu, ndani ya mwezi umepoteza buku 30.
Mwaka mzima? Hiyo ni buku 360,000!
Na kama ungezitumia kuanzisha biashara ndogo au kuwekeza, ungekuwa mbali.
Hiyo ndiyo nguvu tuliyo nayo lakini hatuitumii.
Wengi tulifundishwa kwamba hela nyingi ndiyo hujenga utajiri.
Tukaanza kusubiri *mshahara mkubwa,* *tenda kubwa za kibiashara," au *mjomba wa Dubai.*
Lakini hizo ni hadithi.
Angalia Uhalisia : Hela hujengeka kwa nidhamu na mpango, siyo kiasi.
Watu matajiri hawakuanza na mamilioni.
Walitumia kile kidogo walichokuwa nacho kwa akili.
Walitunza, wakawekeza, wakaendeleza.
Kwa hiyo, tukiachana na dhana ya *nitakapoanza kupata hela kubwa,* tunaweza kuanza safari ya utajiri hata leo,
Kwa ile buku tuliyonayo mfukoni.
Sasa hebu tuweke wazi, unataka kujenga utajiri kwa kutumia buku?
Hizi hapa ni hatua 3 rahisi lakini zenye nguvu:
a. Weka akiba ya buku 1 kila siku:
Tafuta kopo, lipachike mahali salama. Kila siku, kabla ya kutumia hela yoyote, tengeneza tabia ya kuweka buku moja pembeni.
b. Anza kuwekeza kidogo:
Baada ya mwezi mmoja, utakuwa na zaidi ya buku 30.
Tafuta biashara ndogo, lipia kozi fupi, au nunua bidhaa za kuuza mitandaoni.
c. Wekeza kwenye maarifa:
Buku moja inaweza kununua data. Tumia hiyo kusoma makala, kuangalia video za elimu ya fedha, au kusikiliza podcast. Maarifa ni mtaji.
Kuna jamaa yangu mmoja anaitwa Mussa,
Alikuwa na mshahara wa laki na 20 kwa mwezi.
Alikuwa na majukumu mengi lakini alianza kuweka buku moja kila siku.
Miezi sita baadaye, alikuwa na buku 180.
Akanunua kahawa na kuanza kuuza kikombe ofisini kwao, faida yake ilikuwa buku 2 kwa kila kikombe.
Siku moja akaniambia,
*Bro, ile tabia ya kuweka buku moja kwa siku ilinibadilishia maisha.
Sasa hivi nina biashara mbili na bado naendelea kuweka akiba!*
Ukweli ni huu:
Buku moja inaweza kuwa mtaji wa maisha yako mapya.
Usidharau kile kidogo, ndani yake kuna nguvu kubwa sana ya kifedha.
Anza leo, anza sasa.
Usisubiri mshahara mkubwa, anza na buku!
Kumbuka; Buku yako ya leo, ndiyo utajiri wako wa kesho.
MAKALA : MSHAHARA HAUJAWI KUMTOSHA MTU YEYOTE DUNIANI ??? HUJUI PESA YAKO INAPOTELEWA WAPI ?? MATUMIZI NI MAKUBWA KULIKO KIPATO UNACHOPATA ???!!!---- -----NA MWL . JAPHET MASATU---------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Basi Sikiliza Hii Siri Ya Wale Wanaofanikiwa Na Kipato Kidogo!…
Mpendwa Rafiki,
Wengi wetu tunasoma, tunahangaika, tunachapa kazi usiku na mchana,
...lakini hela inavyopatikana si sawa na inavyopotea.
Kule shule waliwahi kukufundisha (compound interest), lakini hawakuwahi kukufundisha kutokutumia hela hovyo wiki ya mshahara.
Ujuzi wa fedha ni uwezo wa....
Kujua hela yako inaingia wapi na inatoka vipi,
Kujua muda gani ni wa matumizi na muda gani ni wa kuweka akiba,
Kuweza kupangilia matumizi kabla mshahara haujalala kwenye simu.
Na ukweli mchungu ni huu:
Si kiasi cha hela unachopata kinachokufanya uwe vizuri, ni vile unavyotumia hiyo hela.
Ebu Niambie, Wewe Uko Wapi?
Hebu kuwa mkweli...
Umewahi kupata mshahara, halafu wiki ya pili unakopa kwa mpesa?
Umewahi kuwa na hela nzuri mkononi, ukajisikia *bosi* – halafu baada ya wiki mbili ukawa broke kama mwanafunzi wa form one?
Umewahi kujiambia, *Mwezi huu nitapanga matumizi vizuri,* lakini siku ya tarehe 5 mshahara ushakwisha?
Kama jibu lako ni *ndiyo* hata mara moja,
... basi wewe si mgeni kwenye kasheshe hili la kukosa ujuzi wa fedha.
Waliokudanganya Kwamba…
Hela inaisha tu bro, hakuna jinsi ya kuizuia.
Maisha ni magumu kwa kila mtu, hakuna anayefanikiwa bila kuibia watu.
Weka hela benki? Hela ya matumizi si ya kuwekwa tu!
Hizi ni kauli tunazojidanganya nazo kila siku.
Lakini ukweli ni huu....
Hela yako haitoshi si kwa sababu hujui kupata, ni kwa sababu hujui kuitunza.
Na hakuna mtu atakayekuja kukuokoa hadi uanze kujifunza wewe mwenyewe.
Na Hii Ndio Njia....
Ujuzi wa fedha sio somo gumu kama hesabu za algebra.
Ni mambo madogo sana ambayo ukiyajua, unabadilika kama saa.
Zifuatazo Ni Njia Tatu (3) Rahisi Unazoweza Kuanza Kuzitumia.
1. Tenga asilimia 10 ya kipato chako mara tu inapopatikana.
Hata kama ni buku tano, anzia hapo.
2. Andika matumizi yako ya kila siku.
Ukishangaa unavyonunua vinywaji vya 3,000 kila jioni, utajua hela zako zinapotelea wapi.
3. Jifunze njia za kuongeza kipato bila kuongeza kazi.
Huu ndio wakati wa kujua kutumia maarifa yako, sio nguvu zako tu.
Chukua Hatua....
Bro, Dada, ukikaa unasema ‘nitabadilika tu muda ukifika’, muda wenyewe haufiki.
Muda upo, ila wewe ndo hujaamka.
Kumbuka;
Maisha yako ya kesho yanatengenezwa na maamuzi yako ya leo, si mshahara wako wa mwezi ujao.
Friday, April 18, 2025
KITINI---STADI ZA KAZI---DARASA LA NNE ( STD 4 )---ELIMU UJUZI / AMALI----( 16 )----" USUSI "-----UTENGENEZAJI WA VIFAA KWA KAMBA---USOKOTAJI WA KAMBA ZISIZO ZA RANGI ( MAFUTO ) NA ZA RANGI------UTENGENEZAJI WA NGATA ZA MEZANI---UTENGENEZAJI WA MAZULIA MADOGO----FULL NUKUU----KWA SHULE ZA MSINGI----TANZANIA-----( PDF )------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Friday, April 4, 2025
Wednesday, April 2, 2025
KITABU 339 : " RHAPSODI YA UHAKIKA " ---FULL KITABU---KITABU CHA KILA SIKU------NA PASTOR CHRIS OYAKHILOME-----2024---BY LOVEWORLD PUBLISHING------" Katika hali ya SALA ( MAOMBI ) tumia kitabu hiki cha kila siku na orodhesha malengo yako kwa ajili ya kila mwezi " -----CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Sunday, March 30, 2025
JIFUNZE BIBLIA TAKATIFU--( 02 )---AGANO LA KALE---( II )---AHADI NA AGANO---WAKATI WA MABABU---HABARI ZA KUTOKA NA ZA AGANO ----MAANA YA " THEMES " AMA " DHAMIRA '----FULL NUKUU---NA PADRE J. BOUQUET DES CHAUX , MAfr,----TOLEO LA PILI---1997-----TANZANIA----( PDF )-------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Saturday, March 29, 2025
JIFUNZE BIBLIA TAKATIFU--( 01 )---AGANO LA KALE-- ( 1 ) : UTUNGO WA VITABU VYA AGANO LA KALE---BIBLIA NI VITABU GANI ? -----VITABU VYA AGANO LA KALE VILITUFIKIA VIPI ? -----VITABU VYA BIBLIA VYOTE NI VYA AINA MOJA ? ----VITABU VYA AGANO LA KALE VILIANDIKWA LINI ? ---MWANGAZA WA ROHO MTAKATIFU ( INSPIRATION }-------NA PADRE J. BOUQUET DES CHAUX , MAfr.----TOLEO LA PILI , 1997------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Friday, March 28, 2025
Thursday, March 27, 2025
Saturday, March 8, 2025
KITABU----334---STADI ZA KAZI / ELIMU UJUZI / AMALI-----13---DARASA LA TATU ( STD 3 )----KITABU CHA MWANAFUNZI----FULL NUKUU ZA SOMO / NOTES---PICHA , CHAPA , MAUMBO NA MAPAMBO , SANAA ZA MAONYESHO , USUSI , USHONI WA NGUO , MUZIKI , KILIMO NA UFUGAJI----KWA SHULE ZA MSINGI---TANZANIA------( PDF )-------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136 ---USIKOSE KITABU HIKI
Friday, March 7, 2025
KITABU 333----STADI ZA KAZI / ELIMU UJUZI / AMALI---11------DARASA LA PILI ( STD 2 )----KITABU CHA MWANAFUNZI----FULL NUKUU ZA SOMO / NOTES---TUCHORE PICHA , TUFINYANGE VIFANI , TUSUKE UKILI . TUSHONE , SANAA ZA MAONYESHO , MUZIKI-----KWA SHULE ZA MSINGI----TANZANIA----( PDF )------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136------USIKOSE KITABU HIKI
KITABU 332---STADI ZA KAZI / ELIMU UJUZI / AMALI 10---DARASA LA KWANZA ( STD 1 )----KITABU CHA MWANAFUNZI-----FULL NUKUU ZA SOMO / NOTES---TUCHORE PICHA KWA KUTUMIA VIGEZO , TUTENGENEZE RANGI , TUTENGENEZE PICHA , TUCHAPE MAPAMBO , TUPAMBE KWA KUCHORA , TUTENGENEZE MAUMBO , TUFANYANGE VITU , TUSUKE UKILI , MUZIKI , TUIMBE , TUIGIZE & TUCHEZE NGOMA , TUCHEZE MICHEZO----KWA SHULE ZA MSINGI----TANZANIA----( PDF )----CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136-----USIKOSE KITABU HIKI